Parliament of Tanzania

Contributions By: Hon. Ally Abdulla Ally Saleh

All Contributions

Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017

MHE. ALLY SALEH ALLY: Hayupo, ndiyo maana nikaomba nafasi hiyo nichukue mimi. Hayupo Dodoma.
MWENYEKITI: Hayupo Dodoma. Umejipangia wewe mwenyewe, haya.
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, sikujipangia, nimekuletea ombi la ruksa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ahsante. Tukitazama utekelezaji wa mpango wetu kwa muda wa miaka mitano iliyopita na hata mwaka mmoja uliopita, hatupati picha yenye kutia moyo. Ingawa umetekelezwa lakini kuna upungufu mwingi, ambapo kwa mfano kwenye umeme hatukuweza kufikia kiwango ambacho tulikuwa tumejiwekea cha zaidi ya megawati 4000. Kwenye barabara hatukuweza kufanikiwa ni chini ya asilimia 50, kwenye reli kilometa 174 au 75 zilizoweza kukarabatiwa. Pia kwenye irrigation ambapo jana kuna mtu mmoja alitoa taarifa, nilikuwa sijui kama tuna potentiality ya 20 million lakini kitu ambacho kimefanywa katika target ya milioni moja, tumefikia only 23%, pia Deni la Taifa limeongezeka katika miaka hii kutoka tisa mpaka 19.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, kama Wabunge na kama Serikali tunatakiwa tujiulize wanatupa moyo gani au wanatupa hope gani ya kuweza kutekelezwa kwa mpango huu unaokuja, wakati Mpango ambao umemalizika ulikuwa very much under-performed.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimefurahi kwamba Serikali wame-mention baadhi ya changamoto katika ukurasa wa 13 wa hotuba ya Mheshimiwa Waziri na wamekuja na solution katika ukurasa wa 14, katika baadhi ya changamoto zile imezungumziwa pia sekta binafsi kwamba ni solution mojawapo ambayo inaweza ikasaidia ikiwa suala zima la funding litafanywa kwa uhakika yaani ugharamiaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niiombe Serikali kwamba, wakati wakija na Mpango kamili hapo baadaye, waje na andiko ambalo litaelezea hii sekta binafsi itachangia vipi katika Mpango huo ili kuhakikisha kwamba funding inapatikana ya kutosha ndani lakini pia kutoka nje, baada ya kuwa na andiko ambalo litaonesha namna gani sekta binafsi itaweza kuchangia katika Mpango wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, ningependa pamoja na vile vipaumbele pale vilivyowekwa ambavyo ni vinne, ningependa suala la utawala bora lingewekwa kama mtambuka, kwa sababu tunalo tatizo kubwa la utawala bora ambalo huko mbele tutalizungumzia zaidi lakini katika hatua hii nataka niseme kwamba, sasa hivi Tanzania inadaiwa kuwa kuna suala kubwa la rushwa, inaidaiwa kwamba kuna tatizo la utekelezaji hata wa maagizo kutoka Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, lakini pia kuna madai mbalimbali ya wananchi kunyanyaswa katika sehemu mbalimbali. Kwa hivyo, ili Mpango uwe endelevu na unaoweza kuwa wa uhakika, ningependa katika vipaumbele hivi pia suala la utawala bora lingewekwa katika umuhimu mzuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimevutiwa na Mpango wa Serikali wa kuweka katika yale mambo ya vipaumbele, kuweka miradi ya flagship, miradi ambayo hiyo itakuwa ni miradi kielelezi. Hili ni wazo zuri na ningefurahi kama katika wazo hilo katika mradi mmojawapo ambao unaweza kuwekwa au katika miradi ambayo itafikiriwa suala la Zanzibar liwe incoperative.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu mimi ni Mtanzania lakini nampigia kura Rais wa Tanzania, lakini pia kuna Wazanzibar ambao wanatumikia Serikali, sioni sababu gani Serikali ya Muungano haina specific project Zanzibar zaidi ya zile za kukagua kodi tu au za immigration ambapo kuna jengo kubwa. Hata hivyo, ningependa nione Serikali, inachangia kwa kuwa na mradi maalum (specific) ambao ni wa kutoka Zanzibar, ili Wazanzibar waone kwamba Serikali yao inawajali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo katika miradi ambayo ni ya flagship, ningependa tuweke mradi, eneo letu ni dogo la ardhi, miradi ambayo inaweza ikaweka; nilisema juzi mama Waziri ulikuwepo, nilikwambia suala silicon veiling tunahimiza katika eneo lile la miradi wezeshi, habari ya TEHAMA. Ni vizuri, tukili-consider suala la silicon veiling, Tanzania ina urafiki mzuri na Bill Gates, tungeweza kutumia ushawishi wetu wa kuleta mradi kama huu wa silicon veiling ambao hauhitaji eneo kubwa sana lakini inaweza ikazalisha eneo kubwa. Mpaka sasa katika eneo letu lote la kanda hii hakuna mahali ambapo pana silicon veiling. Kwa hivyo, kwa wazo hilo ningependa tulitumie vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, ningependa kuona kuwa tunatumia bahari yetu. Tuna masafa ya bahari ya kilomita 1,400 kutoka pembe mpaka pembe ya chini. Nchi kama Seychelles nchi ndogo kabisa ambayo ina watu laki moja. Ambayo ina eneo inaingia ndani ya Tanzania zaidi ya mara 2000 wao ndiyo wanaongoza duniani kwa uvuvi, wa pili kwa uvuvi wa samaki aina ya Tuna, sisi tuna bahari hapo hatujaweza kuitumia vya kutosha. Kwa hivyo hili, ningependa lifanyiwe mkazo kwa sababu tuna uwezo mkubwa sana wa kuvuna kutoka baharini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kitu kingine ambacho ningependa tukitumie kama alama ya Tanzania ni excellence in education. Tunaweza tukajipanga vizuri, tukaweza ku-specialize katika maeneo maalum, zamani nakumbuka niliwahi kusikia, katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam masuala ya maji Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilikuwa kina-save almost kanda yote hii hapa. Mtu yeyote akitaka kuja kusoma maji anakuja Tanzania. hata katika East Africa zamani ilikuwa kuna mgawanyiko, ukitaka kwenda kusoma kurusha ndege unakwenda Soruti, ukitaka kufanya kitu gani unakwenda sehemu gani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, ningependa hili tuli-concentrate, nchi kama ya Cyprus nimekwenda Northern Cyprus, uchumi wake mkubwa unategemea education wamejenga vyuo wame-specialize katika maeneo maalum wamejitangaza dunia nzima, wamejitangaza katika kanda mbalimbali, kwa hivyo wao wanavuna sana kutokana na suala zima la education.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, nataka kuzungumzia, nilisema pale nitarudia kwenye suala la utawala bora. Nataka nirudie hili la Zanzibar, kwanza nafadhaishwa sana kuona Mawaziri wetu hapa Waziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa Ulinzi wanakataa, wanakana kama hakuna suala la mazombi na masoksi Zanzibar, inaniumiza moyo sana. Labda kwa sababu ndugu yake, labda kwa sababu jamaa yake, au kwa nafasi yake yeye hajawahi kukutana na mazombi wakamdhuru au wakamfanyia vitu vingine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati haya yakitokea tunakwenda katika Uchaguzi wa Zanzibar ,tunaambiwa kama unarudiwa, lakini ningependa Serikali itazame upya, itazame implication za kurudia uchaguzi huo, socially implication, 2001 siyo mbali, watu 4000 walikimbia nchi hii wakaenda Somalia. Tutazame economic implication, ikiharibika Zanzibar hakuna uchumi Bara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jana alikuwa anazungumza mwenzangu mmoja anasema baada ya uchaguzi hapa hatuji hapa kujadili mpango, tutakuja hapa kujadili namna ya kujitoa kiuchumi. Kukiharibika Zanzibar, mtalii haji Ngorongoro, kwa sababu mtalii anaji-program kuja Ngorongoro kisha anakuja Zanzibar. Kuna security implication, ikiharibika hali ya Zanzibar hapatakuwa salama katika Tanzania, kuna stability implication, hali ya Zanzibar ikiharibika pia hapatakuwa stable hapa. Mnapotupeleka sasa hivi kama watu hawapati nafasi yao, uhuru wao, kupitia kwenye Katiba watatafuta kwa njia nyingine. Hizo njia nyingine ndiyo ambazo tunataka kuziepuka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, ni negative public relation, hivi Tanzania inajijengea sifa gani kwa dunia. Tanzania imekuwa mfano wa dunia, kwamba ni nchi ambayo inaheshimu demokrasia, ni nchi ambayo inaheshimu haki za binadamu, inaheshimu uchaguzi. Kwa nini tunalazimisha kwa Zanzibar, tulazimishe uchaguzi ambao hauna hata mantiki moja. Unarejea uchaguzi ili iwe nini, Tume ile ile, kwa maana ya marefa wale wale, ma-linesmen wale wale waliokufungisha mabao manne halafu unarudia uchaguzi ule ule, mnarudia uchaguzi ili iwe nini, tupate suluhu gani?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri kuna haja ya Serikali kukaa kwa maana ya uchumi, kwa maana ya stability, kwa maana ya security implication, tukae chini tutazame suala la Zanzibar. Kama mnataka kumwokoa Dr. Shein awe Rais lazima utafute njia nyingine. Ahsante sana. (Makofi)

Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016/2017 – 2020/2021

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza hakuna mwenye nia mbaya, sote ni wananchi na sote hii ni nchi yetu. Tunachofanya ni wajibu wetu kuikosoa Serikali na kuishauri Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nianze kwanza kwenye deni la Taifa. Jana wakati wa presentation ya Mheshimiwa Mama Hawa hapa, wakati ilipozungumzwa na Kambi ya Upinzani kwamba deni ni kubwa na kwamba kuna haja ya kufanya auditing ili tunapoingia katika Mpango huu ambao utagharimu Shilingi trilioni 107 tujue deni letu kabisa kabla hatujaingia huko, Mheshimiwa Mama Hawa alijaribu ku-defend akatoa vigezo vingi vya kuonesha kwamba deni hili bado ni manageable. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nataka kusema kwamba, wenzetu wengine pia walisema madeni yao ni manageable. Bolivia wana mafuta, walisema deni lao ni manageable, lakini baadaye wakaingia kwenye matatizo makubwa! Argentina wana uchumi mzuri na ndiyo wanaoongoza kwa uchumi wa ng‟ombe duniani, walifikiri deni lao ni manageable na waka-collapse! Hali kadhalika na Greece!
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naungana kwanza na Waziri Kivuli wa Fedha wa Kambi ya Upinzani kwamba ni vizuri Bunge hili likatoa Azimio au tukazungumza kwamba kuna haja ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutufanyia auditing ili tujue tunasimama wapi. Katika hizo Shilingi trilioni 107 za kuendesha Mpango, maana yake pia tutakopa. Tumefika hapa kwa ajili ya mikopo ambayo hairudishwi. Kwa hiyo, ni bora wananchi wetu wajue tuna madeni kiasi gani kabla hatujasonga mbele na vipi tutaya-manage madeni hayo. Hilo ni la kwanza! (Makofi)
Mheshimiwa Spika, la pili ni kuhusiana na kipato. Tumeambiwa kwamba sasa hivi kipato chetu kwa Mtanzania ni wastani wa Dola 1,006. Kipato hiki tunaambiwa kwamba, ndicho ambacho Mtanzania anapata. Tumekuwa tukisema hapa kwamba kipato hiki hakionekani kwa Mtanzania wa kawaida, ni pesa za makaratasi zaidi; na tunaambiwa kwamba, tunaelekea kwenye kipato cha Dola 3,000, ndiyo lengo letu!
Mheshimiwa Spika, kama mwananchi, napenda tufikie huko na nchi iingie katika kipato cha kati, lakini Mpango haukueleza base kubwa zaidi; haujapanua base kubwa zaidi ya namna ya kuelekea kwenye kipato hicho kwa kuamini tu kwamba, viwanda ndiyo vitatuletea kipato, lakini ziko sehemu nyingine nchi hii hazihitaji viwanda wala Watanzania wote hawatafanya kazi kwenye viwanda. Kwa hiyo, rai yangu ilikuwa ni kupanua base.
Mheshimiwa Spika, kwa mfano, naambiwa katika Wilaya ya Lushoto au Mtanzania yeyote anajua kwamba wao wanaongoza kwa mazao ya kilimo, mfano mmoja. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Lushoto wanatoka Wakomoro wanakuja pale wanachukua bidhaa wana-pack kabisa wanazipeleka Comoro na pengine zinafika mpaka Ufaransa! Sasa kwa nini tuwaachie Wakomoro wafanye kazi hiyo badala ya kuimarisha wananchi wetu tukawapa fedha wakaweza kufanya vitu kama vile tuka-add value katika bidhaa zetu za kilimo ili kufikia masoko kama hayo? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, la pili, tumeacha area moja kubwa sana katika nchi yetu; area ya uvuvi. Uvuvi wetu ni wa ndoana, wa hapa karibu karibu. Uvuvi wetu haujawa mkubwa wa kutosha. Nimesema katika Kikao kilichopita kwamba tunashindwa na nchi ndogo ya Seychelles ambayo ina watu 100,000 lakini wanaongoza kwa uvuvi wa jodari! Kwa duniani wao ni wa pili!
Mheshimiwa Spika, tuna ukanda wa bahari wa kilometa 1,400 hatujautumika vya kutosha. Jana nilisikia hapa kwamba kuna taarifa kwamba kwenye benki kuna dirisha la kilimo katika mambo ya ukopaji, napenda nione tunafungua Benki ya Uvuvi, iwe specifically located kwa sababu tuna sekta kubwa sana, uvuvi wa kutoka maziwani mpaka kwenye bahari kuu. Kwa hiyo, napenda Serikali ilizingatie hili ili tu-take fursa ambayo inaweza ikapatikana.
Mheshimiwa Spika, kingine ambacho nataka kusema, ni kuhusiana na Mtwara Corridor au sehemu ya Kusini. Kusema kweli, ingawa hapa Bungeni kwa observation yangu, mara nyingi watu wanajivutia Kikanda.
Mheshimiwa Spika, watu wanazungumzia habari ya Reli ya Kati na utaona wengi wanaozungumzia Reli ya Kati maana yake ni watu ambao wanatokea upande wa huko. Kwa fikra yangu nahisi Mtwara is the next big thing in Tanzania, really! Yaani kwa kanda ile kule! Hivi sasa kuna gesi, viwanda vinakuja na capital chemicals nyingi kutokana na LNG ambayo ukitoa gesi maana yake unapata LNG na viwanda vya aina nyingi.
Mheshimiwa Spika, pia, juzi juzi nimesoma kwamba yamegunduliwa madini ya graphite. Madini haya hivi sasa waliotangaza kugundua ni kampuni ya Marekani na mmoja katika Board Members (Stith) ni mtu ambaye alikuwa Balozi wa Tanzania…
MHE. ALLY SALEH ALLY: Anaitwa Stiff, anasema graphite iliyogunduliwa Tanzania inaweza kuwa ya pili baada ya China duniani, lakini pia inaweza kuwa ya kwanza kuliko hata China. Kwa hiyo, ina maana kuna potential kubwa sana.
Mheshimiwa Spika, jana Waziri mmoja alituambia hapa kwamba kuna mpango wa kilimo cha mihogo ya tani milioni 200 kinakuja na soko lipo, lakini sioni uwekezaji unaofanana; kwa communication, unaofanana na rasilimali zilizoko Mtwara. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa hivi tumefungua Corridor ya Kusini kwa Uwanja wa Songwe. Tuna Uwanja wa Kilimanjaro. Kuna haja sasa hivi ya kuwa na Uwanja wa Kusini wa Kimataifa ili uelekee upande mwingine, tufungue Corridor nyingine, katika kila kona ya Tanzania tuwe tuna uwanja ambao unafanana na uwezo na hali tunayosema tunataka tuwenayo. (Makofi)
Kwa hiyo, nashauri kwamba the next big thing kuitazama ni Corridor ya Kusini, tujipange vizuri tuweze kuitumia vizuri ili tuweze kufaidika na gesi na vitu vingine ambavyo vinaambatana na mambo hayo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kingine ninachotaka kuzungumzia ni kuhusu Shirika la Ndege la Tanzania. Actually mpaka tulipofika hapa ilikuwa ni aibu sana kwamba nchi hii tumekubali Shirika letu la National Carrier kufa na hatukuweza kulitengeneza, mpaka hivi sasa tunataka kutengeneza kwa kuwa na ndege mbili. Tunasema kwamba tunatarajia kuwa na watalii wengi kwa sababu tutakuwa na ndege mbili. Actually kuwa na ndege ni kitu kingine na kupata watalii ni kitu kingine. Unaweza kuwa na ndege, lakini kama huna routes zinazofaa na kama hujapata kununua route kwa watu wengine na kama hujaweza kuiuza nchi upya, bado utalii hauwezi kukusaidia. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, pamoja na kuwa na ndege mbili, ambazo sifikiri kama itakuwa ni kitu kikubwa sana, lakini kwa maana ya kuanzia angalau tumeanza, nashauri pia, kama tunataka kufufua Shirika la ATC, mbali ya kwamba tunatakiwa tufagie ATC yote, lakini pia tutafute strategic partners ambao wanaweza kutupa routes nyingine ambazo tutaweza kuzitumia.
Mheshimiwa Spika, hivi sasa humu ndani routes zetu nyingi tumeshaziuza, tumempa Fast Jet kwa routes za ndani. Sasa utashindanaje na Fast Jet wakati ameshaweza kuji-establish kwa muda wa miaka mitatu ambayo yupo hivi sasa na wewe unakuja na ndege mpya? Kwa hiyo, ni lazima tuingie na Mashirika, tuwe na strategic partners ambao wataweza kutusaidia kutufungulia njia nyingine.
Mheshimiwa Spika, pia tutafute model nzuri ya kuwa na Shirika la Ndege. Ethiopia pamoja na kwamba walikuwa katika kipindi cha Haile Selassie, vita, udikteta, lakini bado ni shirika ambalo lilikuwa haliguswi na ndiyo maana limebaki kuwa shirika la mfano kwa Afrika na linafanya kazi na limekuwa likienda vizuri. Kwa hiyo, tusione aibu kuazima management au kuchukua management ikaja kutuwekea sawa mambo ili Shirika lile liende katika hali inayoweza kufaa na ikatusaidia sote kama nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho nataka kusemea ni suala la usalama na utawala bora. Nina mifano michache sana ya nchi ambazo zimeweza kufanikiwa katika kuingia kuwa nchi za viwanda ambazo zimekuwa hazina utulivu au zimekuwa zikiendeshwa na madikteta. Nchi chache kama Singapore na Lee Kuan Yu mfumo wake wa uongozi ulikuwa ni wa kubana lakini ilifanikiwa.
Kwa hiyo, hili ni eneo ambalo hatuwezi kuliachia hivi hivi. Hatuwezi kuwa na chaguzi ambazo kila mara sauti ya wananchi haisikiki, hatuwezi kuwa na chaguzi ambazo Serikali inapeleka majeshi na inalinda chama kimoja halafu tutarajie kwamba tutapiga hatua katika maendeleo. Kwa hiyo, suala hili ni muhimu sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho ningependa ku-cut across the board ni suala la disability, watu wanaoishi na ulemavu. Hili ni eneo ambalo Mbunge yeyote humu ndani halizungumzi kama vile siyo kesho yeye litamtokea.
Mbunge yeyote hazungumzi, kama vile hatuna asilimia 12 ya Watanzania ambao wana ulemavu wa aina moja au aina nyingine. Kwa hiyo, napenda program yote ya Serikali tusiseme tu katika UKIMWI, lakini pia katika disability, ika-cut across kote ili tuweze kutengeneza mazingira na tuweze kufanikisha ili kuona watu wenye ulemavu wanaweza kuchangia na wanaweza kupata fursa za aina nyingine yeyote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, cha mwisho nataka kusemea juu ya kile ambacho Waziri Simbachawene alikitolea taarifa hapa juu ya mshahara wa Rais. Actually aliye-raise suala la mshahara wa Rais ni yeye mwenyewe Rais. Ame-raise mshahara wa Rais yeye mwenyewe kwa sababu pengine alitaka liwe publicity stunts kwamba yeye ni Rais ambaye anapunguza mshahara na kwamba yuko pro-people na hivi na hivi. (Makofi)
Kwa hiyo, hili suala limekuja hapa siyo kwa sababu sisi tumelianzisha, ni kwa sababu yeye alianzisha. Kama itakuwa ilikosewa, ni kwamba waliomshauri walikuwa wamwambie kumbe hawezi kubadilisha mshahara wake akiwa yeye katika madaraka, lakini wanaofuata wanakuwa na madaraka. Pamoja na kazi nzuri inayofanywa lakini wakati mwingine wananchi wanajua wapi pana publicity stunts na wapi ni sifa ya kweli. Ahsante sana.

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Unapotazama bajeti hii lazima takuwa-impressed na takwimu hasa kwenye kipato ambacho nchi hii inapata. Lakini utakuwa unajiuliza kama mwananchi kwa sababu utakuwa na matumaini kwamba tunaweza kutoka kwa mali ambayo tunayo katika nchi hii, mbali ya mali nyingine za misitu na bahari na kitu gani. Picha ya utajiri tulionao katika nchi kwa upande wa madini haionekani katika picha kubwa ya Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, unaamini kwamba madini yangeweza kututoa kwa sababu wako watu wana madini au wana resource moja, mbili na wametoka na nchi zao zimekwenda mbele sana. Sasa sisi kama nchi ukitazama katika kitabu hiki unaona kuna mapato mengi, lakini unaweza ukajiuliza is this our level best, have we done our best katika suala la madini au la gesi? Kwa sababu siyo tu kuna room to improve, lakini naona kama kwamba unajiuliza, tatizo ni nini? Ni sera, ni mipango, ni utekelezaji, ni kitu gani? Kwa sababu zipo nchi ambazo zimeweza kutoka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Angola ilikuwa na vita kwa muda mrefu, lakini baaa ya kutoka kwenye vita wamejipanga, sasa hivi wana kipato kizuri kinachopita dola 8,000 kwa kila mtu. Botswana nchi ndogo, ina GDP ya 38 au 39 billion dollars. Sasa hivi Mbotswana anapata dola 18,000 per capita yake na resource yao ni chache, uranium kubwa kabisa na vitu vingine vidogo vidogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sisi Tanzania tunayo madini ambayo mtu mwingine katika Nchi nyingine angeweza kujiuliza why are you poor? Tusifananishwe na nchi kama Congo ambayo inautajiri mkubwa. Lakini Congo wana tatizo moja kubwa katika suala la utawala bora, lakini sisi tuna utulivu wa kutosha. Kwa hiyo, pamoja na uzuri wa kitabu hiki lakini ukisoma vitabu vingine viwili vya Hotuba ya Kamati na Hotuba ya Upinzani unaona kwamba kumbe tuna mengi ya kufanya ili tuweze ku-realise utajiri ambao Mungu ametujaalia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, na Mungu ametujaalia utajiri ule, ameuleta kwa sequence. Kila baada ya muda tunavumbua kitu kingine ambacho ni kizuri zaidi kuliko kitu kingine. Tulikuwa na almasi tangu miaka ya boers, imeondoka almasi ikaingia dhahabu sasa hivi Mungu katujaalia kuna madini makubwa zaidi ya graphite, tuna uranium inakuja lakini tunajipangaje katika hivi? Sasa mimi najiuliza, kwa mfano, tuna uranium na graphite ambayo ni madini very strategic, lakini je, tunayo sisi wenyewe strategic mineral policy?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tunavyojua madini yanatumika yanakwisha lakini tunajipangaje madini haya yawe ya kututoa. Je, tunatengeneza sovereign fund kutokana na madini haya? Madini yatakwisha lakini nchi itabakia. Nchi inajitayarisha kwa mfuko ule ambao utaweza kuwa akiba kwa siku za mbele?
Mheshimiwa Mwenyekiti, Qatar kweli ina gesi, Angola kweli ina petroli na vitu vingine lakini wana sovereign fund ambayo wanaweka akiba kwa ajili ya baadae. Sasa utajiri wote ambao tunao hivi sasa tunaojivunia, hatutawekea vizazi vyetu huko mbele lakini pia hatutoweza kufanya uwekezaji wa uhakika kwasababu kama nchi hatuna mfuko wa sovereign fund. Jambo hilo nimelisema hapa kabla na ninalisema tena kwa sababu mtu yeyote anaye study Qatar, Norway na wengine wamefaidika katika hilo. Sasa nilisema ukisoma hotuba ya Waziri, soma na vitu vingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, twende kwenye REA. REA tunasema fedha zake zinajulikana zinapatikana njia gani na zimetengewa sheria kwamba lazima zitumike kwa njia ile. Jana tumeambiwa hapa kwamba shilingi bilioni 73 hazikutumika inavyopaswa. Unajiuliza kama shilingi bilioni 73 hizi zingetumika tungepata umeme kiasi gani kwa vijiji vyetu? Na kwa nini hazikutumika na zimekwenda wapi? Kama ambavyo wamesema watu wengine pia ningependa kumuuliza Bwana Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, makaa ya mawe ya Mchuchuma, Liganga kila mtu Tanzania amekuwa akiisikia. Kama nchi tuliwahi kujitayarisha kutumia sisi wenyewe ndani? Tumekuwa na mkakati wa kuongoza nchi kwamba hatuwezi kutumia makaa ya mawe? Makaa ya mawe haya kwa maana nyingine yapo lakini ni kama, kule Zanzibar wanasema kama joka la mdimu, yapo hayatusaidii kitu. Tumekaa nayo, hatuyauzi nje wala hatutumii hapa ndani kwetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni madini. Kama nilivyosema pale mwanzo, tuna madini ya kutosha, kumekuwa na malalamiko mengi hapa. Hata ile alama ya Tanzania (Tanzanite) bado hatuitumii inavyopaswa. Lakini mbali ya hayo, madini mengine mengi ambayo tunayo katika nchi yetu, hatujayatumia kiasi cha kutosha. Mimi naamini kama tungekuwa tumejipanga basi haya yangeweza kututoa. Tumeambiwa katika report ya Kamati kwamba kipato kwenye madini kimeshuka kwa asilimia 19, unajiuliza kitashukaje kwa sababu madini bado yapo kama kuna mikakati mizuri na mipango mizuri ya kutosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwahivyo mimi naamini tungefanya kazi vizuri katika eneo hili. Eneo lingine kama nilivyosema pale mwanzo, ni uranium na graphite. Tanzania, watu wengine wamesema hapa tunaweza kuwa katika kumi bora wa matumizi ya graphite. Graphite imekuja kama akiba yetu, kama hamadi kibindoni ambayo tunaweza tukaitumia ili nchi tuweze kusimama sawa sawa. Lakini kama nilivyosema mwanzo kama hatujakuwa na strategic mineral policy ambayo itatuongoza namna ya kuzuia vitu vyetu hivi basi hatutafika mbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, jana nilisikia wazo ambalo nililipenda kidogo, wazo la STAMICO. Tunawekeza sana katika STAMICO, na dada mmoja hapa amesema, sehemu nyingine walizonazo STAMICO ziruhusiwe kwa wachimbaji wadogo wadogo; lakini lilikuja wazo zuri hapa. Wazo lenyewe ni kwamba badala ya STAMICO kung‟ang‟ania kuwekeza na kushindana na makampuni makubwa, kwa nini tusibadilishe format, STAMICO ikawa inanunua shares ambazo zitakuwa zina uhakika, kwa hili wazo ililtolewa na upande wa upinzani ambazo zitaweza ku-maintain hii kuliko kung‟ang‟ania kitu ambacho STAMICO hiyo enzi na enzi haijatutoa popote pale na bado tuko pale pale tulipo. Wazo hilo nimelipenda na ningependa Waziri alifikirie.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni kuhusiana na suala la gesi. Ni kweli kama nchi tunajipanga kwamba tunataka kutumia gesi ikifika mwaka 2023. Lakini tujue tunajipanga, tuna majirani zetu Mozambique nao wana gesi ambayo inaweza ku-equal na kile ambacho tumekipata hivi sasa. Kwa hiyo, tujue tutakuwa na ushindani wa karibu, tena maeneo ambayo yamekaribiana. Kwahivyo mtu anaweza akachagua kuja Tanzania au kwenda Mozambique kwa sababu kijiografia ni maeneo yako karibu na kwahivyo kama hatujajipanga sawa sawa hatutaweza kufaidika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ningeshauri, suala la LNG lingetazamwa mapema na namna ambavyo tutafaidika kwa sababu watu wote waliopata gesi wametoka. Qatar, Norway na wengine wote lakini kwa ambavyo mara nyingi naona katika nchi yetu tunaweza kuwa na gesi lakini bado tutakuwa maskini kwa sababu umaskini wa Tanzania kwa sehemu kubwa ni umaskini wa kujitakia. Ndiyo maana nakubaliana na hoja ya Kamati ambao wamesema, Serikali iandae mpango mkakati wa usimamizi wa gesi asilia pamoja na kutafuta masoko mapema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, dunia ya ushindani, tujipange kwa muda mrefu. Gesi na vitu vingine vinaweza kututoa lakini kama sivyo tunaweza tukabakia hivi badala ya kuwa economically giant tukawa economically dwarfs.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa mara ya kwanza nimeitwa jina ninalolipenda la Albeto.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo machache ya kuzungumzia na kwanza nitaanza na mjusi, Wajumbe wengi humu wamepiga kelele juu ya mjusi kwamba, kwa nini harejeshwi Tanzania! Mimi ni katika wale ambao wanaunga mkono arejeshwe, lakini najiuliza kama tuko tayari kumpokea na tunaweza kumtunza; lakini kumrudisha tunaweza. (Makofi)
Mheshimmiwa Mwenyekiti, tayari kuna international precedents nyingi zimetokea za mali ambazo zimechukuliwa katika nchi na zikarudishwa. Mfano wa karibuni kabisa ni wa Ethiopia, kuna mnara unaitwa Obelisk, umri wake ni karibu miaka 1700 na una urefu wa mita kama 24, ulikuwepo Italia kwa miaka 68. Baadaye Ethiopia wameweza kuurudisha na upo nchini kwao na ni sehemu ya utalii wao. Sasa inategemea kama Serikali tunaweza ku-negotiate tukaweza kumrudisha. Hata hivyo, kabla ya hapo ningependa sana tutengeze mazingira ili mjusi huyo asije akaozea kwetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni suala la utalii nitalizungumza kwa undani kidogo kwa sababu ni area ambayo naielewa vizuri zaidi. Kwanza, ningetaka kusema kwamba, tuna haja ya kushambulia emerging markets, emerging markets, markets mpya hizi za China, Urusi, India, Arabia, ni sehemu ambazo zinatengeneza pesa sana na hata ukilinganisha namna ambavyo wanatengeneza mamilionea per day wao wako mbele. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni namna gani utatumia kuwavutia kuja kwetu? Nitatoa mfano mdogo wa namna ambavyo kama tutaweza kufaidika na emerging markets, mfano nitakaotoa ni wa Mauritius. China katika mwaka 2011 walipeleka watalii 15,000 Mauritius. Mwaka uliofuata walipeleka watalii 22,000, mwaka mwingine walipeleka watalii 14,000 na mwaka 2014 wakapeleka watalii 63,000 na ushee. Mwaka 2011 India walipeleka watalii 53,000, ikawa 55,000, ikawa 57,000, ikawa 61,000 na naamini tukisema hivi sasa rate yao itakuwa imepanda. Kwa hivyo, namshauri Mheshimiwa Waziri kwenye Wizara yake ajaribu kwenye emerging markets, hilo la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ni suala la re-branding Tanzania. Tanzania tumepitia process mpya kubwa na ndiyo maana hata tukaona kuna haja ya kufanya katiba mpya kwa sababu kama nchi tumepitia mambo mengi lazima tujitambulishe upya kama Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, branding ambayo tunayo hivi sasa ndiyo ambayo kwa miaka yote imetupa watalii milioni, labda 1,200,000. Hii branding nataka ifanywe upya tujitambulishe tuna vitu gani vya kuuza, vinapatikana wapi, vinapatikana vipi, rates zetu ziko vipi. Kwa mfano, tumetumia brand ya Tanzania, land of Kilimanjaro and Zanzibar kwa miaka yote hiyo, tumepata watalii 1,100,000.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashindwa kupata watalii zaidi kwa sababu sisi hatutaki kujilinganisha na wengine, sisi tuna vivutio vingi, Mauritius wana vivutio vichache kuliko sisi lakini wao wanatupita, wao tayari 2014 walikuwa wana watalii 1,200,000. Ni kisiwa cha watu 1,500,000 lakini wamepata watalii 1,200,000. Kwa hivyo kuna haja ya ku-re-brand. Lakini hiyo re- branding tusiifanye sisi tuwape watu, mashirika makubwa wanaoweza kufanya re-branding ili tuweze kupata faida. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hiyo hiyo na sasa nataka nizungumzie habari ya re-discovering our pontentials. Watu wengi wamezungumza hapa, kuna watu wamezungumza kwamba, inaonekana kama kuna upendeleo au ndiyo culture tuliyoachiwa, kwamba utalii ni kaskazini. Lakini kuna southern circuit ambayo inaweza ikatusaidia sana. Pia kuna sehemu nyingine za pembezoni, kwa mfano Mara, Arusha wameungana na Kenya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tumejipanga vipi sisi utalii wetu kuungana na Uganda, tumejipanga vipi utalii wetu kuungana na Mozambique, kuungana na sehemu nyingine ambazo tunapakana nazo. Nitatoa mfano wa Kagera, kagera tuko na Uganda. Lazima tuwe na package ambayo inamfanya mtu akienda Uganda baadaye akija Kagera ashawishike. Juzi nilifunuliwa macho na Profesa Tibaijuka hapa aliposema kuna ziwa linaitwa Ziwa Burigi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiambiwa chochote dakika ile ile nakwenda kwenye internet. Pale pale nikaenda kwenye internet nikaona how beautiful that place is. Ni mahali ambapo mtu yeyote angeweza kwenda. Tuna game reserve ya Burigi lakini tuna ziwa, lakini hakuna hata kibanda cha mtalii kufika. Pale kwa nilivyosoma na nimetamani, nimemwambia mama Mwigaje hapa nataka niende nikaone, ile picha niliyoipata Ziwa Burigi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo tunaweza tukamshawishi mtalii kutoka Uganda akaja pale, hali kadhalika southern circuit. Kuna fursa nyingi beach sun mpya za Mtwara na Lindi, mnazitumiaje kama sehemu ya southern circuit. Kwa hiyo, tubadilike katika hilo.
Mheshimwa Mwenyekiti, halafu nataka kuzungumzia juu ya advertising. Nchi kama Malaysia, Indonesia, zimepiga hatua kubwa sana katika utalii, lakini bado wanatangaza costing millions to them. Tangazo lao linapendeza, unalipenda, unalisikiliza. Kwa hivyo lazima tuchukue international firms siyo tunapeleka tangazo kwenye Sunderland ambalo linawekwa tu hivi. Tangazo lazima liwe strategic, idadi ya watu wangapi, tunafaidika vipi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija katika nukta hii hii nataka nizungumzie Walking billboard. Tuna Mbwana Samata anacheza mpira Belgium, kwa nini kama Taifa au kama Wizara tusiingie naye mkataba akifunga goli akiinua jezi tu visit Tanzania, ambayo inaonekana dunia nzima na sio Belgium tu, lakini hatutumii potential tulizonazo. Kwa hivyo, ningependa hili tulitazame. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna sports tourism. Nilizungumza na Mheshimiwa Nape juu ya namna ya sisi kujipanga kama Taifa. Nchi hii hakuna international tournament ya golf, hakuna international tournament ya Tennis, hakuna international tournament ya cycling. Nchi kubwa lakini haijajipanga vyovyote vile kimichezo. Kwa hivyo, ningependa kwamba, eneo hilo pia tulitengeneze ili tuweze kuzitumia vizuri tufaidike. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nataka nizungumzie role mpya ya Mabalozi. Mabalozi wote lazima waelekezwe kwamba, hivi sasa tutengeneze tourism diplomacy kuwe na package, watayarishwe, wawekewe na malengo namna ambavyo wanaweza kukuza utalii wetu; lakini isaidie kwamba, watengenezewe package ili tuweze kufaidika ndani ya nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, nataka nizungumzie suala la kutengeneza mnaso wa community kubwa ya wageni wanaoishi maeneo ya East Africa. Mzungu au expert yeyote ambaye yuko East Africa unamtoza visa sawasawa na ambaye amekuja leo kutoka Marekani. Tuwe na package maalum ya expertise kutoka Rwanda, Kenya, Uganda, tuwe na package maalum washawishike kuja kwetu. Mtu mmoja alisema lazima tuweke rates za kuvutia ili watu waje, baadaye tuweze kubadilisha lakini lazima tu-change katika strategy hizi na kwamba, tunatoza kodi nyingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ni very expensive destination, tusijisifu kwa watu wanaokuja, tungeweza kupata watu zaidi kama tutajitengeneza vizuri zaidi. Sisi ni losers, hatuna haja ya kushindana na Kenya, hatuna haja ya kushindana na Uganda, tuweke rates ambazo zinatufaidisha sisi na ndiyo maana tutawashinda. Ndiyo maana kukitokea matatizo Kenya sisi tunafaidika. Kwa hiyo, tusingojee mpaka Kenya wapigane sisi tufaidike. Pia tunaweza tukaweka rates ndogo ili tuvutie watalii zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia ningependa kuzungumzia habari ya standards. Tunakwenda nchi za wenzetu, tuna hotel higher lakini unaona kwamba, bado tuko nyuma, service mbovu. Ningependa tuhakikishe kwamba, tunakuza sekta kwa kuwa hata na masomo ya degree na tuweze …
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Alberto.

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nina mambo machache ya kuzungumza lakini kimoja nitakisema in passing tu juu ya mwenge. Tusipeane majina wala tusipunguziane uzalendo kwa sababu tu hatuukubali mwenge. Mimi kwa bahati nilikuwemo katika Tume ya Warioba na katika kitu Watanzania walichokikataa na wakasema waziwazi uende makumbusho ni Mwenge wa Uhuru. Kwa hiyo, wanaosema kwamba mwenge upumzike au kama msemaji wa sasa hivi aliyesema tutafute modality nyingine mimi ni mmojawapo na hii hainipunguzii uzalendo kwamba mimi ni Mtanzania na naipenda Tanzania yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, sisi kama Taifa tunaishi katika zama za sasa, hatuwezi kuishi sasa kisha tukabakia kizamani. Sasa hivi dunia imepanuka, kuna technology mbalimbali na kuna njia mbalimbali za kuwasiliana. Wakati njia za kuwasiliana zinapanuka na wakati sisi tunapimwa kwa ajili ya kuwa wawazi kwa wanachi wetu na sisi kuwa huru kujieleza, ndipo sisi tunapofunga milango ya uhuru wa habari na uhuru watu wetu kujieleza. Hii hai-augur well na vipimo ambavyo sisi tunapimwa kama nchi na ndiyo maana ripoti ya Amnesty juzi imetu-condemn na kutushusha sisi katika suala la uwazi na uhuru kwa waandishi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi hii katika upande wa habari, mimi maisha yangu yote ni mwandishi wa habari na nimepita wakati ambapo tulikuwa tunabanwa hata kusema tulikuwa hatuwezi. Wakati naripoti Zanzibar naweza kuiandika story leo nikaenda Dar es Salaam nikakaa siku tatu nasubiri mshindo kule Zanzibar utakuwa vipi, tusiishi tena hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi hii wakati tunapanua demokrasia mwaka mmoja tunapitisha sheria tatu za kubana uhuru na kubana watu namna ya kujieleza, nafikiri hii si sahihi. Hii ni dalili ya woga na dalili ya kuogopa watu wako wenyewe wasiseme. Kiongozi mzuri, Serikali nzuri ni ile ambayo inaruhusu watu wao watoe joto lao, wajieleze ili wajue kuna kitu gani katika Taifa. Kwa hiyo, mimi nafikiri tusijivunie kwamba tunazuia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine tu kwa mfano, leo tumezungumza vitu vingi sana kuhusu wasanii na utamaduni, lakini tumejifungia humu ndani. Tumezuia wananchi wetu wasisikilize na wasipate taarifa juu ya mijadala ya Bunge kwa hofu tu kwamba wakisikia watabadilika mawazo, tusiogope hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho nataka kuzungumzia ni suala la kiswahili, watu wengi wanazungumzia habari ya kiswahili. Kwa wale ambao hawajui, mimi ni mpenzi sana wa Kiswahili na ni mwandishi wa mashairi lakini pia ni mwandishi wa vitabu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, wakati tunajivuna kwamba Tanzania ndiyo mabingwa wa kiswahili lakini kusema kweli Kenya wametutangulia. Graduates wa Kenya kwa kiswahili hatufiki sisi hata one third yao kwa kila mwaka. Sasa hivi katika mashirika mengi ya kimataifa, translators wengi walioko nje, vyuo vingi vikuu, walimu ni kutoka Kenya na siyo Tanzania. Nchi hii ya Tanzania ambayo inajivuna ina kiswahili niambieni kuna literature prize gani ndani ya nchi hii? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kenya katika zawadi ambayo inaongoza duniani kwa kiswahili ni Cornell-Mabati Kiswahili Prize ambapo mimi mwaka huu nime-submit kitabu changu kinaitwa La Kuvunda. Wenzetu hawa wanatoa zawadi kila mwaka kwa miaka mitano sasa na kuna commitment ya kampuni ya Mabati na Cornell University kuendelea kwa muda wa miaka kumi ijayo, hata hili hatuwezi kubuni ku-approach corporate world ya Tanzania ikashirikiana na chuo kikuu kimojawapo kukawa na literature prize kwa kila mwaka? Hii itaibua waandishi, tutabaki tunaimba tu tulikuwa na Ibrahim Hussein, Profesa Lihamba, Profesa Penina, wako wapi watu kama hao, hakuna tena caliber kama hiyo kwa sababu hatuwatengenezi. Tusitarajie tu kwamba watuzuka bila kutengenezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine ni suala zima la culture ya michezo ya kuigiza. Tunazungumza sana habari ya bongo movie lakini moja katika culture nzuri sana ni michezo ya kuigiza ambapo Tanzania imekufa. Nilipokuwa chuo kikuu ilikuwa wakija wale waigizaji Nkurumah Hall inajaa, sasa hivi hata sijui kama kuna michezo ya kuigiza ndani ya nchi hii kwa sababu hata waandishi wa michezo ya kuigiza hawapo tena na hawatengenezwi na hawatayarishwi. Kwa hiyo, namuomba Mheshimiwa Waziri alitizame hili, tuwe na competition za kila mara ili kuweza kukuza jambo hili. Sasa hivi tuna vyuo vikuu vinafika 50, jambo kama hilo linawezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nije katika area ya michezo ambayo naielewa vizuri sana kama ninavyoelewa suala la habari na hapa nitazungumza zaidi kidogo.

Mimi nafikiri ni katika wale ambao siamini kwamba Wizara au Serikali ndiyo yenye jukumu la michezo, mimi siamini. Mimi naamini Serikali kazi yake ni kutengeneza sera, lakini corporate world ndiyo ambayo inaweza kusimama na kukuza michezo na mfano mzuri ni huu wa Simbu hivi sasa. Niliwahi kuzungumza na Mheshimiwa Nape wakati akiwa Waziri kwamba tuache kumpa mzigo mtu mmoja kumwambia tunataka shilingi milioni 200 kwenda Olympic au shilingi milioni 500 kwenda Commonwealth, unakwenda kwa mtu mmoja mmoja, uache kila corporate imwambie wewe chukua dhamana ya mwanariadha huyu hapa, wewe chukua dhamana ya mwanariadha huyu hapa, tutafika mbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini watu wanalalamika wanasema hatupati timu kubwa za nje kuja Tanzania, wanalalamika kwamba rank ya Tanzania haipandi kwa sababu hatuchezi na timu kubwa. Kucheza na timu kubwa ni gharama kubwa sana, kuileta Brazil mimi mwenyewe nilijaribu, minimum wanataka dola milioni moja za kucheza uwanjani, mbali ya gharama zao. Kuileta Argentina inahitajika kama dola 800,000 kuwaleta wakacheza uwanjani mbali ya gharama zao nyingine za ndege na kila kitu. Kwa hiyo, kama corporate Tanzania hatujaishirikisha vya kutosha ikaweza kuchangia, hatuwezi kuzileta timu kubwa na maisha yatabakia kule kule zero. Maana yake unataka ulete timu lakini kiingilio unataka uweke shilingi 5,000, unasema eti unawajali watu wadogo, haiwezekani, lazima kimojawapo utakikosa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine watu wamezungumzia hapa habari ya vipaji, vipaji vinatengenezwa na tena siyo Serikali yenye jukumu la kutengeneza academy, ni mimi na wewe. Wabunge pia wana uwezo, wana haki na wajibu wa kutengeneza vipaji kwa sababu vipaji ni biashara, unaweza ukatumia shilingi milioni 100 lakini wakati ukiuza mchezaji mmoja unaweza ukapata shilingi bilioni moja. Kesi ya Samata kwa mfano, mimi nilikuwa involved mara nyingi katika biashara zake, najua namna ambavyo amefikia pale.

Kwa hiyo, watu wajue kwamba kuwekeza kwenye riadha, soka, vipaji inalipa kwa mchezaji mmoja tu ukipata, siyo wawili au watatu, mmoja tu inalipa. Kwa hiyo, Wabunge hilo pia mnaweza kulichangamkia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sikubaliani na msemaji aliyepita hapa kwamba tuwalete wachezaji wengi wa nje wacheze ligi yetu ya ndani. Uingereza wana tatizo hivi sasa hawana timu ya Taifa nzuri kwa sababu wageni ni wengi. Cha kufanya sasa hivi TFF itengeneze kanuni kwamba klabu yoyote kwanza iwe na timu ndogo lakini ilazimike kama vile ambavyo kuna limit ya wachezaji wa nje kucheza watano basi lazima iwe na mchezaji under 20 katika kila mechi yake ya ligi, mmoja, wawili au watatu, hiyo itatusaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kingine naogopa time yangu isiishe nataka nizungumzie juu ya mchezo wa chess. Mheshimiwa Waziri nisikilize vizuri. Chess ni mchezo ambao unaweza kututoa Tanzania kwa haraka sana, kwanza hauna gharama. Mimi ni mshabiki wa chess na nafundisha chess. Ni mchezo ambao ukishapata bao lako la kuchezea, mnakaa watu wawili, ukivaa bukta, kanga, seluni (msuli) unacheza tu. Ni mchezo ambao unaweza kufundishwa na kukuza vipaji vya watoto wetu. Kuna uwezekano pia wa kusaidia kupata masters wa chess wakacheza dunia nzima na tukajulikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi nafikiri tusing’ang’anie tu michezo iliyopo na ndiyo maana hapa nataka kusema Mheshimiwa Waziri lazima hivi sasa tuamue tuwe na priority, iko michezo tumecheza miaka haijatupeleka popote, lakini iko michezo inayoweza kututoa. Kwa hiyo, hata kama utatangaza waziwazi kwamba priority itakuwa ni riadha, soka na kitu fulani na kitu fulani kwa sababu hatuwezi kucheza michezo yote kwa sababu hatuna fedha za kuhudumia michezo yote, lakini lazima tuangalie na hii michezo mingine. Mheshimiwa Waziri tunaweza kushauriana zaidi ukinihitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante nilitaka kuchangia maeneo manne, lakini matatu nimeyaleta kwa njia ya maandishi ambayo ni kuhusu conference tourism, festival tourism na water sports tourism ambayo bado nchi hii haijatilia mkazo na haijawekeza vya kutosha. Lakini eneo ambalo nitalizungumza kwa urefu kidogo na ambalo nina interest lakini ninauzoefu nalo ni sports tourism ambayo hivi sasa inaambiwa ni the still sleeping giant, hii inafaida kubwa duniani na ikitumika vizuri inaweza kusaidia Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa globally sports tourism inatengeneza karibu 90.9 trillion dollars kwa mwaka mpaka 2017. Lakini kutoka 2015 ilikuwa 46.5 trillion dollars kwa hivyo ni biashara kubwa duniani lakini Tanzania bado hatujaitumia vizuri. Lakini hata katika individual sport kwa mfano golf, golf ni biashara kubwa na Kenya wanazungusha a lot of money kwa sababu wamewekeza katika golf. Wana viwanja vyenye kutosha yale mashimo yanayotakiwa vitano ambavyo karibu 35 percent ya watalii wanaokwenda Kenya ni wale ambao wanakwenda kwa ajili ya golf. Halikadhalika na Afrika Kusini nao wamewekeza katika eneo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kwa ujumla golf ni biashara kubwa duniani na wanaongoza duniani ni Ireland ambao wanatengeneza wageni kiasi 165,000 kila mwaka wanatembelea Ireland kwa ajili ya issue ya golf wakati sisi hatujaitumia golf kama mchezo ambao unatusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata kwenye riadha mimi ningetarajia watu wa utalii wangehimiza sana marathon zote ambazo Tanzania wangejitokeza wakazidhamini na wakasimamia, lakini pia wakazikuza. Kuna mchezo kama cycling ambao tuna maeneo ambao unaweza ukatengeneza pengine Dar es Salaam to Tanga tunaona ile Paris mashindano ya baiskeli yanaisaidia sana na yanaitangaza sana nchi ile, Arabuni wanafanya mashindano ya baiskeli lakini sisi bado hatujaanza kutumia michezo katika hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, muhimu ni kwenye individual sports ni rahisi kuwekeza. Kwa mfano Watanzania wote sasa hivi wanajivunia Simbu, Simbu lakini kumbe taasisi za kitaliii zingeweza kutengeneza Simbu wengine kumi kwa sababu kuwekeza katika individual sports ni rahisi kuliko kuwekeza katika team sport. Kwa hiyo, mimi ningewashauri watu wa utalii wawekeze kwa mtu mmoja/mmoja wamdhamini mtu mmoja/mmoja tunaweza tukatengeneza watu hasa watu ambao wanakimbia kwenye marathon.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingini ni kwenye mpira wa miguu na hili tayari naelezea interest yangu nimeshawaandikia TANAPA ni decleare interst nimeshawandikia TANAPA programu ya namna ya kuweza kuileta timu kutoka Ulaya kuja kucheza Tanzania. Eneo la pre-season ambao ni kuelekea kwenye ligu kuu za nchi za Ulaya timu nyingi za Ulaya zinapenda kwenda nje ya nchi zikafanye mazoezi na sisi Tanzania hatujaitumia. Nimekuwa nikisikia kwamba Everton inaweza ikaja hapa lakini tunaweza tukaleta Everton na tukaleta na timu nyingine na nyingine. Kwa hiyo, pia ningetaka watu wa utalii wawekeze katika eneo hili kwa sababu inakuwa na fedha nyingi. Wenzetu Thailand, Singapore na wengine huwa wanafanya kila mwaka na tayari kama nilivyosema nimewapelekea TANAPA pengine wataona kama inafaa wataitumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna timu za ndani hapa tumezoea kuwekeza kwenye Yanga na Simba. Lakini Yanga na Simba at the end of day sio kwa maana ya kuingia watu uwanjani, lakini kwa maana ya kuonekana wanaonekana timu zingine zinaonekana kama timu nyingine katika television hasa Azam Tv ambayo kusema kweli sasa hivi ni globally brand, inafika mbali.

Kwa hiyo, watu wa utalii silazima wawekeze kwenye Yanga na Simba ambao wanapata wafadhili mbalimbali NMB, Sport Pesa na wengine lakini pia wanaweza wakajitokeza kwa mfano timu ambayo najaribu kui-promote timu ya Lipuli au timu nyingine zilizopanda daraja wakawavisha jezi zao wakazi-brand matangazo ya utalii at the end of the day kwa maana ya kuonekana wanaonekana ninety minuties sawasawa wanavyoonekana Yanga na Simba na kwa hiyo, wataonekana dunia nzima. Kwa hiyo, ningependa hiyo pia mlifanyie kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najiuliza tuliambiwa hapa kwamba tulikuwa tunatangaza kwenye klabu za timu za nje hasa ilikuwa Sunderland lakini suala hili liliulizwa mwaka jana halikupata majibu ya kutosha. Na kwa hiyo bado kuna haja ya kutumia matangazo ya nje lakini very strategical, mwaka jana nilishauri kuhusu Samatta siju limefikia wapi lakini…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante,

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Wizara ijitazame kuchachua utalii katika maeneo yafuatayo:-

(i) Festival Tourism: Nchi lazima ijipange vyema kuanzisha matamasha mapya na kuimarisha yaliyopo. Nionavyo kama Taifa tutimize na ku-advertise Busara Festival na Zanzibar Film Festival, kwa sababu ya effect yake, tunaweza kuwa promoted katika kiwango cha Taifa. Ni kosa kutotangaza as part of National Tourism Campaign.

(ii) Songkran Festival ya Thailand ambayo ni ya siku tatu huingiza US Dollar 428.08 million. Afrika Kusini 35 percent ya utalii wake ni matamasha ya utamaduni. Tuwe na matamasha ya sanaa na mengine.

(iii) Nyingine ni Conference Tourism ambayo inatarajiwa kuipa Rwanda US Dollar 76 million mwaka huu na kupandisha utalii kutoka US Dollar 1.2 million kwa 2014 hadi US Dollar 1.3 million hapo mwaka 2015; na mapato kutoka US Dollar 318 million to US Dollar 400 million kwa kipindi hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vema sana kwa kuwa Dar es Salaam imepumua kuwa Capital City, sasa tukielekeza jiji hilo kuwa hospitality and commercial city na conference tourism ipigwe jeki kubwa kuifanyia matangazo. Tuhimize uwekezaji wa Multipurpose Convention Centers na hii itaendana vizuri na ujio wa uwanja wa ndege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, water sports ni muhimu pia.

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, uchangiaji wangu utakuwa na theme kwamba nchi hii inahitaji mabadiliko ya fikra kwa sababu hapa tulipo tumegota. Kama kilimo tunakipa asilimia chinjo kila mwaka, kama kilimo kinapata asilimia tatu tu katika maendeleo, wakati huo tunasema tunataka maendeleo ya kilimo na maendeleo ya kilimo haya tunataka yaungane na viwanda, nafikiri tunahitaji fikra mpya. Hapa tulipo tumegota. Miaka 53 ya nchi hii haiwezekani tusiweze kujilisha au kusimamia wakulima wetu. Nafikiri tumegota na tunataka mabadiliko ya fikra katika kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tulipo hivi sasa, nchi hii ina ardhi ya kutosha, ina maziwa ya kutosha, ina mito ya kutosha, ina ukanda wa bahari wa kutosha, lakini ni kitu gani tunajitosheleza? Je, tunajitosheleza kwa chakula? Tunajitosheleza kwa uvuvi? Tunajitosheleza kwa mazao ya nyama au maziwa? Sifikiri katika yote hayo kama tunaweza kuyatimiza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukisema hivi mara nyingi tunakuwa tunalaumiwa, lakini nafirikiri badala ya kwenda mbele kwa kilimo tunarudi nyuma. Kwa sababu baada ya miaka 53 haiwezekani kwa mfano, Kenya ambao sisi tunawapita kwa idadi ya ng’ombe kwa zaidi ya mara mbili ya mifugo wana maziwa ya kutosha sisi hatuna au nchi nyingine nyingi ambazo tunapakana nazo. Kwa hiyo, katika utewekezaji wetu wa kilimo, tumeshindwa kupima muda, fursa na rasilimali zetu. Kwa sababu hiyo, ninaamini kwamba tunahitaji fikra mpya, hapa tulipo, tumegota. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tulipo hivi sasa, nchi hii, kwa mujibu wa Ripoti ya Benki ya Dunia ni kwamba tuna ekari ambazo ni arable na ambazo zinalimika ni milioni 13,500,000; tuna ukanda wa bahari wenye maili 1,400; tuna eneo la mikoko ambalo lina hekta za mraba 115,000 lakini kwa mfano kwenye bahari mpaka hivi leo hatujaweza kuvuna rasilimali za bahari na wanaokuja kuwekeza tunawakamata, tunawashitaki na tunawanyang’anya vyombo vyao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna utaalamu ambao hautaki tena kuvumbua; nchi za Philipines Cambordia, Malaysia na nyingine zinatumia mikoko ambao sisi tunaihifadhi tu, lakini kina kitu kinaitwa mud crab farming, yaani ufugaji wa kaa katika mikoko ambao una utajiri mkubwa sana, lakini bado hatujautumia. Naamini tumegota katika fikra na tunataka tupate mapinduzi ya fikra. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine nashangaa katika nchi hii ambayo asilimia 52 ni misitu. Tuna eneo la maji ambalo linaweza kuzalishwa kwa kilimo ni zaidi ya hekta za mraba 61,500; lakini haielekei kama kuna connectivity baina ya Serikali yenyewe na Wizara kwa Wizara, kwa sababu kama kuna connectivity ingekuwa hadi hivi leo isingewezekana rasilimali zote tulizonazo tusiweze kuzitumia vya kutosha. Nafikiri tunataka fikra mpya, sasa hivi Serikali inaonekana kama imeshindwa katika eneo la kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuje katika leather industry. Tanzania ni ya tatu kwa ng’ombe Afrika; ni ya 11 kwa ng’ombe duniani. Ina asilimia ya ng’ombe asilimia 1.67 ya dunia. Tumefaidika nini katika leather Industry? Kama hatuna leather Industry, ina maana hakuna maana ya kufuga ng’ombe maana hatupati maziwa ya kutosha, hatuna viwanda vya maziwa, ngozi yetu hatuitumii vya kutosha. Kwa hiyo, haina maana ya kufuga. Nafikiri tumegota, tunataka fikra mpya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kwenye mazao ya chakula, tumebaki katika yale yale ambayo ni traditional; na vile vile mazao ya biashara ambayo ni traditional. Sasa hivi sisi tunajifunza, tuna hali ya hewa nzuri sana au ya kila namna; ipo joto kidogo, baridi kidogo, ipo ya mchanga kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mazao mapya ambayo tunaweza kuyavumbua, tumeingia kwenye vanilla kidogo kwa Kilimanjaro na Kagera. Hivi sasa bei ya vanilla ni dola 500 kwa kilo moja. Sisi kama nchi tumehiza vipi zao hili? Kuna mazao kama zafarani (saffron) ambayo kilo moja ni dola 4,000. Tumefunguka vipi kama nchi? Nafikiri tumegota na tunataka mapinduzi ya fikra. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna masoko yamejifungua chungu nzima. Tuna Vietnam wamekuja kuingia mkataba na sisi, tuna Wachina, tuna Waturuki; tumefikiria vipi juu ya mazao? India peke yake inaweza kumeza kwa siku 15 mazao yote ya choroko ya Tanzania, kunde zote za Tanzania. Tumewafunza vipi watu wetu kutumia soko hilo? Tunataka mabadiliko ya fikra, tunafikiri CCM mmegota kimawazo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi hii pia hatuoni upya wa mambo ambayo tunayafanya. Walisema kwamba walitaka wamtue mwanamke ndoo, walisema wanataka wamnyang’anye mkulima kijembe cha mkono, lakini kwa miaka kadhaa hivi leo bado ni tradition farming. Niambieni nchi hii, wapi kuna shamba la kilimo la kisasa la mwekezaji ambaye analima kwa maelfu ya heka kuitoa nchi hii katika njaa? Nafikiri mmegota na inabidi tupate mabadiliko ya fikra. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nafikiri kuna haja kubwa ya mabadiliko. Kwa fikra zangu, nadhani sasa hivi irudisheni agenda kwa wananchi, mwaambie wananchi kwamba katika kilimo, mifugo na uvuvi, mmeshindwa; ili baada ya bajeti hii turudi tena kwa wananchi tujadili jambo hili. Kwa sababu nafikiri kunahitajika mapinduzi ya fikra na fikra hamwezi tena kuitoa ninyi kwa sababu mmeshindwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni Wizara muhimu kwa uhai na mustakbali wa nchi yoyote, bado naafiki Jeshi halisi la JKT kimuundo. Ningependa Jeshi letu liende katika usawa kivifaa, lakini imeonekana Jeshi kwa sasa halina powerful public branding ili kusimama kama taasisi yenye chapa ya Kitaifa. Wananchi hupata public relations ya Jeshi only wakati wa sherehe tu, na si vinginevyo na hivyo Jeshi hubakia katika obscurity. Bila shaka mazoezi ya kijeshi ni moja ya njia hizo kama ile amphibious iliyofanywa Bagamoyo. Ningependa Jeshi liji-brand pia kwenye kufanya kazi za dhamana mara zinapotokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa kuna dharura za mvua/upepo lakini Jeshi halijitokezi kikamilifu. Kazi hizo hufanywa kwenye matukio ya big magnitude tu. JKT inapaswa ipitie upya jukumu lile la kujenga uzalendo ambalo linaonekana limeshindwa hata katika hili, inafaa JKT ijitathmini upya.

The Legal Aid Bill, 2016

Mheshimiwa Ally Saleh Ally, Mheshimiwa Anatropia Lwehikila Theonest ajiandae. Tutamalizia na Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa.
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nianze kwa kusema kuna msemo wa kiingereza unasema kila kitu kinakuja kwa sababu zake na leo asubuhi tulipoanza hapa tulianza na swali kuhusu mambo ambayo yametokea Zanzibar ambayo ya upigaji, uoneaji, unyanyasaji wa wananchi na tukashuhudia Serikali ikisema hata haijui kwamba hayo mambo yanatokezea na ikasema kwamba mambo hayo hata hayajawahi kuripotiwa polisi na kwa hivyo wao hawajui chochote kinachoendelea.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini only two hours later tunaletewa Muswada wa Msaada wa Kisheria kwamba upande mmoja haki zinavunjwa, watu wanakoseshwa haki zao, wananyanyaswa, wanapigwa, hakuna kinachoendelea lakini upande mwingine wanajitengenezea mazingira ya kulinda wananchi wake. Kwa maana hiyo tunaambiwa kwamba kuna raia wa namna mbili nchi hii. Kuna raia wa Zanzibar ambao ni haki yao kuonewa na Serikali kila siku kukataa na asubuhi nilisema hapa Bunge hili imefika wakati iundwe Tume, Waziri akakwepa hakujibu kabisa, lakini upande huu mwingine wanatengenezewa haki ya ku-access justice. Upande ule kule justice is denied to them. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ni Mjumbe wa Kamati hii ya Katiba na Sheria na natahasaf kusema kwamba Muswada huu ni Muswada muhimu sana kwa ajili ya Tanzania na ningetamani Muswada kama huu baadaye uwepo Zanzibar. Umuhimu wake ni kwamba unatengeneza mazingira ambayo watu wetu kwa miaka wamewekwa nyuma sana, elimu ya uraia, elimu ya haki haijafikishwa kwao kiasi ambacho wengi wanadhulumiwa, wanaonewa bila ya kujua waende wapi au wafanye nini.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mbunge mmoja asubuhi hapa alimwambia Waziri wa Katiba na Sheria kwamba alikuwa wapi siku zote, lakini kila kitu kinakuja na wakati wake. Kila kitu na zama zake. Hata hivyo, mimi mwenyewe nilimwambia Mheshimiwa Waziri kama kwamba Muswada huu utakuja vizuri, utamjengea legacy yeye kama Waziri kwamba ameweza kuleta Muswada huu ambao unahitajika sana na Watanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna tatizo moja ambalo litatukabili. Muswada huu unakiuka utaratibu wa Muswada wa mwaka 1969 ambao tulikuwa tunazungumzia masuala ya jinai peke yake. Hapa sasa tunakwenda pia masuala ya madai. Hapa maana yake tunafungua wigo mkubwa sana. Wenzetu Kenya hawakufungua kwenye suala la madai, wenzetu Malawi hawakufungua kwenye suala la madai, lakini sisi tumefungua kwenye suala la madai, maana yake sasa administration itakuwa kubwa, kazi itakuwa kubwa ya kufanya, elimu itahitajika kubwa sana, wakati ukweli kwa mujibu wa watu wenye uzoefu wa legal aid ni kwamba sehemu kubwa yale mashirika makubwa sana yanasimamia kesi kumi mpaka kumi na tano kwa mwaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi tuna mashirika machache sana ambayo yanafika sehemu kubwa. Tuna paralegals ambao watafika au wanafika mpaka vijijini. Hata hivyo, kuna tatizo hilo la kufungua upana mkubwa sana, wanasheria wanaweza wakasema flood gates sasa sijui kama nia yetu tutaweza kuitimiza kuchukua madai na jinai pamoja lakini maadam sheria inawekwa, wacha tuone itafanya kazi vipi, itasimamiwa baadaye. Hilo moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, sheria hii is not the best that we could have done, ingeweza kuimarishwa kwa sababu tumepata bahati hatuku re-invent the wheel. Mheshimiwa Tundu Lissu leo hapa amezungumzia historia ya Marekani ya miaka mingi ya legal aid, lakini tusiende mbali twende hapo Kenya tu, kama tungeweza kwenda ndani wenzetu wamefanya nini, wamekwama wapi? Nafikiri tungeweza kufanikiwa, lakini sheria hii imekuwa katika mchakato kwa zaidi ya miaka kumi hivi sasa, kwa bahati mbaya hawa Kamati ya Katiba inayosimamia hivi sasa haikupata fursa ya kujifunza wenzetu wengine wanafanya nini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, wenzetu waliokwenda Afrika Kusini na kwengine kwenye Kamati hii wote wameondoshwa kwenye Kamati hii, kwa hivyo, hawakutuwezesha kupata uzoefu wowote ule ambao wameupata huko walikokwenda kufanya study.
Mheshimiwa Naibu Spika, ndio maana asubuhi akapongezwa sana Mheshimiwa Tundu Liissu kwa sababu he is the only surviving na analazimisha kuja kwenye Kamati yetu tu, kwa sababu yeye siyo mjumbe wa Kamati yetu; lakini ametusaidia sana kwa sababu he is the only surviving ambaye alikwenda katika training au kufanya utafiti Afrika Kusini na akabakia kwenye Kamati hii. Kwa hivyo, kwa mfano Kenya, board inayosimamia haikufanywa kuwa governmentally, imefanywa kuwa ni board huru ina muhuri wake inaweza kushtaki na kushtakiwa na haiko moja kwa moja kiserikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kenya wamefanya Mkurugenzi wa Board anagombea kwa sifa; hateuliwi. Kwa hivyo, kuna ule uhuru wa board yenyewe, tumekuwa tuki-force, tunasema kwamba board hii inaweza ikafanya maamuzi ya kutetea watu, tunajiuliza je, ikitokea kwamba inayoshtakiwa ni Serikali au kosa lililopo ni kubwa kama kosa la uhaini, kosa la ugaidi huyu mtu ambaye; hii board ambayo mlolongo wake unakwenda mpaka kwa Katibu Mkuu na tuli-attempt hata katika Kamati hata kutaka kum-distance Katibu Mkuu lakini ikaonekana kama waleta hoja wakaona kama ni ngumu. Tukajiuliza inawezekana vipi katika hali kama hiyo, mtu kama huyu kutetewa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ambacho Kenya wamefanya ambacho mimi mwenyewe nilivunjika moyo, ni kujaribu kufanya ushawishi wa kwamba tuhakikishe tunakuwa na legal aid fund; ama kwa kuwa na sheria nyingine au itajwe kuliko ilivyosema section 37 ambayo inaelezea namna ambavyo pesa zitapatikana. Tunajua kuna shida ya ku-approve pesa hapa kwa mashirika haya ambayo ni kama yako pembezoni. Mwaka jana hapa tulilalamika sana watu wa katiba na sheria na hata tukataka kumtetea Mheshimiwa Waziri kwamba Tume ya Haki za Binadamu iongezewe pesa na mpaka mwaka huu haikuongezewa pesa hata ya kufanya activity moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maana tume mwaka mzima huu, itakuwa imekaa ofisini tu, najiuliza tulete mambo haya mengine, kwa maana nyingine tunaweza tukarudia yale yale tena tusiipe legal entity, fedha za kutosha na kwa hivyo haitofanya kazi za kutosha itakuwa kama ile Tume ya haki za Binadamu. Kwa maana nyingine watakuwa wanawategemea wale legal aid provider‟s ambao hao wanakwenda kuomba pesa kwa wafadhili wetu wa kawaida traditionally founders sijui wa-Sweden, wa- Norway ndio wanaotuendesha hivi sasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivyo ningependa kuona kwamba wale Wabunge wanakuwa serious katika Serikali itakapoleta pendekezo, wale wanaoshangilia hapa kwamba sasa watatetewa, watapata haki za kutetewa na kitu gani waje waishike Serikali koo hapa mpaka hiki chombo kipate fedha za kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine ambacho Kenya wamefanya na sisi tungeweza kukifanya ni kwamba sheria yao iko liberally zaidi. Kwa mfano, wameweka utaratibu kwamba kila kituo ambacho ni holding center kama cha watoto, kama ni polisi au kama ni magereza kunakuwa na form za readymade zipo, mtu akifika kama vile Marekani unaposimamishwa unavyoambiwa haki yako ni moja mbili tatu, basi na hiyo iwepo, kwamba ukifika gerezani, ukifika polisi usomewe haki zako, halafu upewe option uambiwe kuna uwezekano wa kupata legal aid, unataka au hutaki, alafu iwe recorded katika register kwamba huyu kapewa fursa hiyo na ameikataa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivyo Mheshimiwa Waziri akasema lakini hiyo itapita kwenye mamlaka nyingine, Wizara nyingine, tukasema Serikali inasemezana, wasemezane ili hili liwepo tuweze kujua kitu kizuri ambacho wenzetu wameweza kukifanya.
Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ambacho kilitatiza kidogo ni suala la pale mtu anayekwenda mahakamani lakini akashindwa kesi na kwa hivyo hapatakuwa na cost ambazo zitakuwa awarded na Mahakama na kwa hivyo ataondoka pakavu. Sasa sijui Waziri amekuja na pendekezo gani katika hili kwa maana mimi nilipenda statement yake moja alisema issue sio kum- reimburse fully advocate au mtu ambaye anakwenda kumtetea mtu lakini angalau arudie katika hali yake inayofanana kabla hajaenda kule kwa gharama aliyoipata.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri ametuletea amendment hapa inambana Wakili, Wakili atakwenda mahakamani, tunajua sasa hivi aibu kusema hivi sasa anapata kiasi gani, lakini atakwenda mahakamani pengine akishinda kesi, atakuwa awarded cost ambayo tulisema ziwe awarded sio kwa yule ambaye alitetewa lakini ziwe awarded kwa Wakili, lakini akishindwa case anaondoka patupu, sasa huyo sijui hii imefikiriwa vipi kuweza kuhakikisha kwamba inawezekana kuifanyia kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, cha mwisho kabisa ni suala zima la namna ambavyo sasa hivi tulipigania kwamba wale ambao sasa hivi wapo wana-exist sijaona schedule of amendment lakini tumesema wale ambao wana-exist sasa hivi wasiwe labored ku-register upya. Moja kwa moja wachukuliwe kwamba wao automatically ni legal providers na wachukuliwe wawe registered moja kwa moja. Wasiwe labored kuanza tena ku-apply kwa sababu uki-apply ina maana mwenye mamlaka anaweza kukukatalia au anaweza kukubalia.
Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana na nitafurahi kama Muswada huu utatendewa haki ya yale marekebisho ambayo tuli-suggest katika Kamati na naamini utaweza kusaidia sana Watanzania hasa wale wanyonge. Ahsante sana.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's