Parliament of Tanzania

Contributions By: Hon. Mahmoud Hassan Mgimwa

All Contributions

Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016/2017 – 2020/2021

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anazozifanya. Naomba nimpongeze Dkt. Mpango kwa uwasilishaji wake mzuri.
Naomba kuishauri Serikali katika mambo yafuatayo:-
Ni vyema kuweka wazi mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika Mpango wa Kwanza 2011 – 2016 ili tujue tatizo ni nini? Serikali imeamua maamuzi yapi kwa yale mambo ambayo bado hayajakamilika.
Mpango huo ulilenga kutanzua vikwazo vya kiuchumi na kupunguza umaskini na kuimarisha upatikanaji wa huduma za jamii.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukuuaji wa pato la Taifa 6.7% - 7% unalingana na upatikanaji wa huduma za jamii kama afya, maji na elimu.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukuaji wa uchumi uende sambamba na kupunguza umaskini.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri alipaswa kuweka wazi vigezo vilivyotumika kujua uchumi wa Taifa unakua, income per capita peke yake hatoshi kwa sababu upatikanaji wa income per capita unajumuisha matajiri sana na maskini sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, mfumuko wa bei unasababishwa mara nyingi na cost push inflation na demand pull inflation. Naipongeza sana Serikali kwenye eneo la demand pull inflation ni muda mrefu sasa tumeweza kuhimili mahitaji ya chakula ndani ya nchi lakini kwenye cost push inflation.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri ametaja eneo la mafuta, ni vyema Serikali ikajipanga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana na wa bei nafuu. Serikali ihakikishe umeme wa makaa ya mawe, maji na upepo unapatikana ili kupunguza adha ya umeme.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia Serikali ihakikishe barabara za uhakika maeneo yote yenye kilimo cha uhakika kwa lengo la kupunguza gharama pia reli ianze kufanya kazi kwenye maeneo yote muhimu.
Mheshimwa Spika, eneo lingine ni kuhusu thamani ya shilingi ambayo inashuka na haiko stable.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni vyema sasa Serikali ikaweka mkakati wa kuondoa matumizi ya dollarization ambayo nchi nyingi duniani zimedhibiti eneo hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunauza kidogo nje ya nchi kuliko tunavyonunua. Ni vyema sasa tujidhatiti kuongeza kuuza nje ya nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kilimo; asilimia sabini na tisa ya Watanzania inategemea kilimo, ni vyema tukajipanga katika eneo hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote naomba nichukue fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu ambaye amenijalia kusimama leo hii mbele ya Bunge lako Tukufu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya kipekee naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya ya kizalendo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Dkt. John Pombe Magufuli anafanya kazi nzuri ya kusimamia uwajibikaji na uadilifu katika Serikali yetu. Pamoja na kazi nzuri bado anaendelea kutumbua majipu ndiyo maana leo hii wenzetu wa upinzani wameamua kuweka mpira kwapani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, waswahili wanasema mwenye wivu ajinyonge, tutaendelea kumpongeza Dkt. John Pombe Magufuli na tutaendelea kumuunga mkono kwa kazi anayoifanya katika nchi hii. Kwa namna ya kipekee naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu kwa hotuba yake nzuri na kwa kazi nzuri anayoifanya kuisimamia Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa Jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kunirudisha tena katika Bunge lako Tukufu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu nitaanza kwa kujielekeza katika ukuaji wa uchumi. Katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema mwaka 2015 uchumi ulikua kwa asilimia 7.1, mwaka 2014 uchumi ulikua kwa asilimia 7. Ni kweli uchumi unakua, lakini ninaomba Serikali inapozungumzia suala la ukuaji uchumi lazima waangalie na hali halisi ya maisha ya Mtanzania. Ukuaji wa uchumi unatakiwa uende sambamba na huduma za jamii kama afya, elimu pamoja na maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika vipaumbele ambavyo amevizungumzia Mheshimiwa Waziri Mkuu vya ukuaji wa uchumi amezungumzia suala la kilimo. Jana katika hotuba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti alisema asilimia 79 ya Watanzania wameajiriwa katika eneo la kilimo, lakini ukuaji katika eneo hili unakua kwa asilimia 3.4 ambao ni ukuaji mdogo sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii Waziri Mkuu amesema wakulima ni asilimia 66.3 ya Watanzania wote ambao wako kwenye eneo hili. Serikali ni kweli imeona kwamba, zaidi ya asilimia 79 ya Watanzania wameajiriwa katika sekta hii ya kilimo, lakini bado Serikali haijaamua kuwekeza kwenye eneo hili, katika eneo hili hakuna Mbunge ambaye haguswi. Tunaiomba Serikali iangalie kwa macho yote katika eneo hili haswa katika mfuko wa pembejeo, ule mfuko wa pembejeo umewekewa hela ndogo sana kulinganisha na pesa ambazo zinatakiwa ziwepo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tutawekeza vizuri katika eneo hili la kilimo nina hakika kabisa hata eneo ambalo tumekusudia kwenda kwenye Mpango wa Pili wa viwanda tutakwenda vizuri, kwa sababu Mheshimiwa Mwigulu pamoja na Waziri wa Viwanda ni watoto pacha, kama tutafanya vizuri kwenye kilimo automatically tutafanya vizuri kwenye viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunaomba sana, kwenye eneo la pembejeo Serikali iongeze mfuko wa pembejeo ikilinganishwa na ilivyo sasa, kwa sababu unawagusa Watanzania karibu wote, aidha inagusa wananchi wa Chama cha Upinzani na wa Chama Tawala, kwa hiyo tunaiomba Serikali iwekeze sana kwenye eneo hili. Lakini la msingi zaidi tunatakiwa tuhakikishe zile pembejeo zinawafikia wakulima kwa wakati, zikiendelea kuchelewa zitaendelea kuwapa matatizo wakulima wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, eneo la kilimo ni eneo very sensitive, Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Kilimo, benki hii ya kilimo ilianza miaka mitatu iliyopita, na tulikubaliana kwamba, benki hii ianze kwa mtaji wa shilingi bilioni 100, lakini jambo la kusikitisha mpaka leo benki hii ya kilimo imepewa shilingi bilioni 60 wanashindwa kumudu na wanashindwa kuwasaidia wakulima.
Hivyo, tunaomba benki hii iongezewe mtaji na kama tulivyokubaliana kila mwaka benki hii ya kilimo iendelee kupata mtaji.
Mheshimwia Mwenyekiti, kwa kifupi bilioni 60 hazitoshi! Tunaomba benki hii isiwepo Dar es Salam tu, iende hadi kwenye site ambako wakulima wapo. Itakuwa bora kama benki hii ya kilimo itakuwepo kwenye mikoa haswa ya kilimo na iwafikie wananchi, utaratibu wa kupata mikopo uwekwe uwe wazi na wananchi wajue ni haki yao kupata mikopo ya riba nafuu. Tukifanya vizuri kwenye eneo hili kama nilivyosema awamu ya pili ya mpango tutakwenda tukiwa kifua mbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ninalotaka kuchangia kidogo ni kuhusu mfumuko wa bei. Mheshimiwa Waziri Mkuu amezungumzia sana mfumuko wa bei na jana Waziri wa fedha alizungumzia mfumuko wa bei. Lakini Waziri wa Fedha jana alizungumza jambo moja kwamba, tukidhibiti eneo la mafuta tutakuwa kwenye hali nzuri ya kuzui mfumuko wa bei.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua kabisa mfumuko wa bei unasababishwa na mambo makubwa mawili, la kwanza Cost Push Inflation na la pili Demand Pull Inflation. Tunapozungumzia Cost Push Inflation ni kweli kwenye eneo la mafuta tunaweza tukawa kwenye eneo hili, lakini hatuwezi kuzungumzia eneo la mafuta peke yake bila kuzungumzia umeme, kama tuta- control bei ya umeme itakuwa iko chini na umeme utapatikana kwa wakati, automatically utapunguza cost of production.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuishii kwenye jambo hilo tu, vilevile nilitaka tuzungumzie suala la infrastructure kwa maana miundombinu kama tuna uhakika na miundombinu mizuri automatically tutakuwa tumefanya vizuri. Kwa namna ya kipekee naomba nichukue fursa hii kuipongeza sana Serikali kwenye suala la Demand Pull Inflation Serikali iko vizuri na Watanzania tumekuwa tuna chakula kingi na hatuagizi nje ya nchi. Kwa hiyo katika jambo hili tuko vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo huwa tunalipigia sana kelele hapa suala la dollarization lakini Serikali imekuwa siyo sikivu haisikii kwenye jambo hili. Tunaomba hawa watu ambao wanaendeleza utaratibu wa dollarization kwa njia moja au nyingine ina-affect uchumi wa nchi hii, thamani ya shilingi automatically inapoteza mwelekeo kutokana na dollarization.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekisoma kitabu cha Waziri Mkuu, nimeona haikuzungumzia kabisa suala la uvuvi. Tunatakiwa tuwekeze kwenye eneo la uvuvi, eneo la uvuvi ni eneo muhimu ambalo tunawekeza mara moja na baada ya kuwekeza nina hakika tutakuwa tume-create ajira za kutosha, vijana wengi wanaweza kujiajiri katika eneo hili na tukapata mtaji mkubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatakiwa tuwe waangalifu na tunatakiwa tuwe waangalifu na tuwekeze hasa kwenye bahari kuu ili kusudi tuweze kupata mitaji mikubwa. Kuna baadhi ya nchi hapa duniani kama Sychelles zinaishi kwa uvuvi na sisi hatuna sababu ya kutokupata mapato makubwa kwenye eneo la uvuvi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu nyingine ninayotaka kuzungumzia ni kuhusu suala la maji. Maji ni muhimu sana kwa maisha ya Mtanzania na kwa masikitiko makubwa katika Jimbo langu ambalo lina Kata 11 maji ni tatizo, sina hata Kata moja ninayoweza kuzungumzia suala la maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wetu ile senti 50 ambayo imeingizwa kwenye tozo ya mafuta ingeongezwa ikawa shilingi 100 badala ya shilingi 50 kusudi tuweze kupata maji katika Majimbo mengi na katika maeneo mengi. Tunaiomba Serikali inapoleta bajeti kwenye eneo la maji tuongeze hatuna sababu ya kutochangia kwenye eneo la mafuta badala ya shilingi 50 tuweke shilingi 100 ili mfuko wa maji uendelee kukua. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ningependa kulizungumzia ni suala la miundombinu. Ili tuone uchumi unakua vizuri ni vema tukahakikisha miundombinu yetu ni ya uhakika. Katika eneo langu lina matatizo katika barabara ya Mapanda, Usokami, Ihalimba na Kinyanambo, barabara ya Mtili, Ifwagi, Mdabulo na Ihanu. Tumewaandikia wenzetu wa TAMISEMI kwa vile hivi sasa barabara zile hazipitiki, tumewaandikia kwenye mfuko wa emergency watusaidie katika eneo hili. Wakitusaidia nina uhakika kabisa tunafanya vizuri katika maeneo haya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu eneo la nishati. Tunazungumzia sana sasa hivi nishati ya gesi, tumesahau habari ya makaa ya mawe. Makaa ya mawe ni muhimu sana, ukiangalia wenzetu wa South Africa asilimia 57 ya umeme unatokana na makaa ya mawe. Sisi hatuna sababu ya kutokuwekeza kwenye makaa ya mawe, tulitakiwa tujenge transmission line kutoka Makambako kwenda Songea mpaka Mbinga ambayo gharama yake ilikuwa shilingi bilioni 60 na wenzetu wa SIDA walishakubali kutusaidia kwenye eneo hili. Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba Serikali inasuasua kwenye eneo hili! Kuna uwezekano wa ku-produce megawati 120 kwenye kilowati 210.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tusipofanya hivyo kwenye eneo hili tutakuwa tunawaonea watu wanaotoka kwenye maeneo hayo.

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nakushukuru wewe binafsi kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia kwenye hoja hii muhimu, lakini kwa namna ya kipekee naomba nichukue fursa hii kukupongeza sana kwa kazi nzuri unayoifanya ya kuongoza Bunge lako Tukufu.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hii kumpongeza Waziri na Naibu wake wa Fedha kwa bajeti yao iliyokuwa nzuri. Lakini kwa namna ya kipekee naomba nichukue fursa hii kuipongeza Serikali kwa kuanza kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kutenga asilimia 40 ya bajeti ya mradi wa maendeleo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa kuipongeza sana Serikali kwa kuanza kutekeleza ahadi za Mheshimiwa Rais, za kupeleka shilingi milioni 50 kwenye kila kijiji na kwenye Serikali za Mitaa. Naiomba Serikali ihakikishe inatengeneza utaratibu unaoeleweka kusudi zile hela shilingi milioni 50 ziweze kuwafikia walengwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hii kumshauri sana Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri kwamba moja ya majukumu ya Bunge ni kuishauri Serikali, lakini leo hii tumeona Waheshimiwa Wabunge wengi wamezungumzia sana tatizo la maji. Nataka nimwambie Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri, sisi Wabunge tumetumwa maji kwenye maeneo yetu, kwa hiyo tunataka tuone maji yanatoka. Katika eneo hili Wabunge wametoa hadi utaratibu ambao unaweza kutusaidia tukapata hela kwenye maeneo hayo. Kwa hiyo, sioni sababu ya Mheshimiwa Waziri kuanza kusita tumesema tuongeze shilingi 50 kwenye tozo la mafuta kwa maana ya dizeli na petroli. Sisi wenyewe Wabunge ndiyo tutakuwa tuko tayari kwenda kuwasemea wka wananchi kusudi wajue kwa nini tumeongeza pesa hizo, sasa sioni sababu ya Serikali kusita kwenye eneo hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, adha ya maji inaeleweka na wanaopata tabu katika eneo hili ni wakina mama na ndoa nyingi zimekuwa zinamashaka kwa sababu ya tatizo la maji katika mjini pamoja na vijijini. Kwa hiyo, namuomba sana kaka yangu Waziri wa Fedha pamoja na Naibu wake waliangalie hili jambo kwamba moja ya miongoni mwa sera za Chama cha Mapinduzi ni kuhakikisha watu wanapata maji katika maeneo yao. Na hapa sisi kama Wabunge tumetoa commitment kwa kusema tuko tayari kuruhusu tutoe shilingi 50 kwenye mafuta ya dizeli na petroli kusudi tuhakikishe wananchi wetu wanapata maji katika maeneo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tunamuomba sana Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri waliangalie hili jambo watakapokuja kuhitimisha hapa waone asilimia karibu 95 au 96 ya Wabunge wote wanataka kuhakikisha maji yanapatikana katika maeneo yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ya Bajeti wakati inajadiliana na Wizara ilitoa mapendekezo na ilikubaliana na hoja kwamba ile tozo ya shilingi 50 sehemu ya tozo ya shilingi 50 ipelekwe kwenye afya kwa maana ya kuboresha vituo vya afya na zahanati. Kwa hiyo, hatuna sababu ya kutokukwepa kwenye eneo hili. Ni lazima tukubaliane na hii hoja kusudi wananchi walio wengi wapate huduma kwenye afya pamoja na zahanati.
Mheshimiwa Naibu Spika, sababu alizokuwa anazitoa Waziri pamoja na Naibu Waziri kwenye eneo hili, wanasema kwamba kuongeza tozo kwenye eneo hili tutakuwa tumeongeza mfumko wa bei. Siyo kweli, mwaka 2015 bajeti iliyopita tuliongeza tozo ya shilingi 50 kwenye maeneo haya, wakati uli mafuta yalikuwa yana rank kutoka shilingi 2100 mpaka 2500 na sasa hivi mafuta yana rank toka 1600 mpaka 1900 na mfumko wa bei uliendelea kubaki vilevile. Kwa hiyo, ninataka kumwambia Mheshimiwa Waziri asiingie woga kwenye eneo hili, watu wanataka maji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kuomba hela hizi za maji naiomba Wizara ihakikishe hizo hela zinaenda kwa wakati kumekuwa kuna tatizo la kuzichelewesha hizi hela ziende kwa wakati kwenye maeneo haya. Matokeo yake ni kusababisha miradi ya maji kuendelea kuwa ya gharama zaidi, kwa sababu mradi unapochelewa kufanyiwa kazi automatical gharama za maji zinapanda.
Leo hii sisi Wabunge wa CCM ndio tupo ndani tunajadili, kwa hiyo tunamwomba sana Waziri wa Fedha akubaliane na hoja hizi kwa sababu ndizo zinazowagusa wananchi waliokuwa wengi. Tutaonekana Wabunge wa CCM tumetoa maamuzi mazuri kwa maslahi ya Taifa hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nataka kulizungumzia ni suala la kilimo. Katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, alisema asilimia 67 mpaka 72 ya Watanzania wanategemea kilimo, na yeye mwenyewe, wakati anazungumzia suala la mpango alizungumzia asilimia 67 ya Watanzania wanategemea suala la kilimo. Kulikuwa hakuna sababu ya kutokuongeza ruzuku ya pembejeo katika eneo hili. Kwa hiyo, tunamuomba Waziri aliangalie hili jambo.
Mheshimiwa Naibu Spika, yeye mwenyewe Mheshimiwa Waziri amekuja hapa ametuambia tuna kwenda kwenye mpango wa Viwanda, tunaendaje kwenye mpango wa viwanda kama malighafi hatuwezi kupata kutoka kwenye kilimo? Tunamwomba Waziri kusudi tuweze kupata malighafi ya kutosha, lazima tuhakikishe wakulima wanapata pembejeo kwa bei rahisi na wamesaidiwa katika eneo hili. Kwa hiyo, nataka nimuombe ndugu yangu aliangalie na hili jambo la kuongeza mfuko wa pembejeo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la Benki ya Kilimo, hili ni suala very sensitive na ni nyeti sana, kwa hiyo tunaomba kwenye benki hii waongezewe mtaji, na ifunguliwe matawi yote katika nchi hii ya Tanzania kusudi wale amabo tumewakusudia waweze kusaidiwa katika maeneo husika. Tuna kwenda kwenye uchumi wa viwanda, lengo kubwa ni kuhakikisha tunapata mapato ya kueleweka na tunapata ajira. Serikali inajitahidi kuwashauri wawekezaji wa ndani na nje kwenye eneo hili waje kuwekeza. Na wawekezaji wanawekeza kwa nguvu kubwa sana, itakuwa ni kosa kuendelea kuzitoza malighafi katika eneo hili. Kwa hiyo, nilikuwa namuomba Waziri anapokuja atuambie kwa nini ameamua kutoa tozo ya crude oil kutoka sifuri kwenda asilimia kumi. Tayari watu wameshawekeza hela zao pale na tayari kuna ajira ya uhakika katika eneo hili. Ni vyema aangalie ni utaratibu gani utakaotusaidia kupata kodi, kwenye eneo la wafanyakazi Pay As You Earn na kwenye kodi za kawaida. (Makofi)
Eneo lingine ambalo nataka kulizungumzia ni eneo la utalii. Katika bajeti iliyopita utalii ulichangia asilimia 17 kwenye Pato la Taifa na ilikuwa utalii inaongoza kwenye kuchangia katika Pato la Taifa lakini leo hii tunaweka...
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Awali ya yote napenda kuwapongeza Wenyeviti wote waliowasilisha leo mada zao hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa majukumu makubwa ya Bunge letu Tukufu ni kuishauri na kuisimamia Serikali, lakini kumekuwa kuna tatizo hapa. Tutazungumza, tutasema, lakini hayo tutakayokuwa tumeyazungumza na kuyasema na kuwashauri wenzetu wa Serikali watakuwa hawayafanyii kazi kama siku za nyuma. Kwa mfano, katika bajeti iliyopita sisi Waheshimiwa Wabunge wote kwa kauli moja tulishauri tuongeze tozo ya maji kutoka sh. 50 kwenda kwenye sh.100 na Wabunge wanajua matatizo yaliyopo kwenye majimbo yao. Cha kusikitisha kabisa Serikali ilikataa hili jambo na hela ambayo inafanya kazi sasa hivi ni hela ya Mfuko wa Maji, hela iliyokuwa kwenye bajeti kuu haipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nawashawishi Waheshimiwa Wabunge wenzangu ili hoja ambayo tulikuja nayo kwenye bajeti tuendelee nayo na yawe ndiyo maazimio ya Bunge ili hiyo sh. 50 iongezwe ili kwenye bajeti ya safari hii tusiume maneno; kwamba tozo ya maji imetoka kwenye sh.50 kwenda kwenye sh.100 ili tuendelee kupata maji katika maeneo yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ninalopenda kushauri katika Wizara hii ya Maji ni suala la mita; tuwe na mfumo wa prepaid kama ilivyokuwa umeme, kwa sababu miongoni mwa watu wanashindwa kulipa maji kwa wakati matokeo yake Sekta hii ya Maji inashindwa kujiendesha. Kwa masikitiko makubwa taasisi nyingi za Serikali zimeshindwa kulipa na ndizo zilizoweka mzigo mkubwa sana kwenye taasisi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba sekta hii kutengeneza hifadhi, kuchimba mabwawa ya kutosha ili maji yawe ya uhakika kwa muda mrefu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo la kilimo. Asilimia 67 mpaka 72 ya Watanzania ni wakulima na Serikali imesema kwamba inataka kwenda kwenye uchumi wa viwanda, tutaendaje kwenye uchumi wa viwanda kama hatujawekeza vya kutosha kwenye eneo la kilimo? Tuna matatizo kwenye eneo la pembejeo, naiomba Serikali katika eneo la pembejeo tuangalie kwa nafasi kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka ya nyuma tulikuwa tuna eneo kubwa la kutoa ruzuku katika eneo hili, lakini cha kusikitisha ruzuku inayotoka safari hii ni ndogo kuliko iliyokuwa siku za nyuma, mfuko wa ruzuku katika eneo hili umepungua. Kwa hiyo, waongeze mfuko wa ruzuku tofauti na uliokuwepo miaka iliyopita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwa, Serikali imekuwa hailipi pesa za mawakala, kwa hiyo wametengeneza gap kubwa kati ya mawakala na wakulima wetu waliokuwa kijijini. Serikali inadaiwa zaidi ya bilioni 64, huu mwaka wa tatu na baadhi ya mawakala wameuziwa nyumba zao na baadhi ya mawakala wamekufa kutokana na shock walizokuwa nazo katika maeneo. Kwa hiyo, tunaiomba Serikali ijiangalie na iwalipe hawa mawakala kusudi waweze kufanya kazi zao mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja kwenye eneo la ukame. Hapa kwenye eneo la ukame kuna tatizo. Naishauri Serikali ipeleke mbegu ambazo zinahimili ukame katika maeneo husika, lakini vilevile katika yale maeneo ambayo kwenye ripoti yetu tumeyasoma leo, zile halmashauri 55 ambazo zina matatizo ya chakula tunaiomba Serikali ipeleke chakula haraka iwezekanavyo. Kwa sababu tunaweza tukashindwa kupeleka chakula kwa wakati tukasababisha inflation, chakula kitakuwa kiko juu kwa sababu ya demand pullinflation katika maeneo yale,kwa hiyo hata ule mfumuko wa bei tunaouzungumzia kwamba tunaweza tukau-control, tatizo la chakula likiendelea kuwepo katika maeneo husika automatically inflation itaongezeka katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwa tunaiomba Serikali iondoe kodi kwenye mbegu zinazozalishwa hapa nchini. Unakuta mbegu zinazotoka nje ya nchi hazina kodi lakini mbegu zinazozalishwa na Watanzania zina kodi. Haya ni masikitiko makubwa sana, waziondoe hizo kodi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tunaomba Serikali iongeze mtaji kwenye Benki ya Kilimo, mtaji uliopo sasa hivi hautoshi. Kwa hiyo, wakulima wetu hata kama wanataka kufanya kazi kwa ajili ya kuisaidia hiyo sekta ya viwanda ambayo inataka kuja hatuwezi kupata kwa sababu benki katika sekta hii haipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nizungumzie kidogo kuhusu ranchi. Tuna tatizo, kuna baadhi ya ranchi zilichukuliwa na watu binafsi na zinaendelea kumilikiwa na watu binafsi. Hatuna sababu ya zile ranchi kuendelea kumilikiwa na watu binafsi ikiwa hawazitumii kwa yale makusudi tuliyoyakusudia; matokeo yake mifugo mingi inazurura kwenye hifadhi za Taifa na kuleta kero ambazo hazina sababu. Kwa hiyo wale watu ambao wanatumia ranchi zile ambazo hazina sababu ya kutumiwa wanyang’anywe zirudishwe Serikalini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ninalotaka kuzungumzia kidogo ni suala la maliasili. Nataka kuzungumzia suala la VAT kwenye maliasili. VAT inapokuwepo automatically unaongeza gharama za utalii, kwa hiyo Serikali yetu badala ya kupata mapato tunayostahili kupata, hatuwezi kupata mapato yale kwa wakati, kwa hiyo Serikali iliangalie upya suala la VAT. Wenzetu wa Kenya tulikwenda nao kwa kauli moja, lakini ilipofika wakati wa utekelezaji Wakenya wakaji-withdraw kwenye hili jambo wakatuacha tukakaa peke yetu, kwa hiyo utalii wa hapa nchini ukawa gharama zaidi kuliko wa kwao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la miundombinu. Miundobinu ya utalii katika nchi yetu ni dhaifu, kwa hiyo tunatakiwa tujiangalie kwenye hili eneo, tuboreshe miundombinu katika maeneo ya utalii na tujenge nyumba za bei rahisi kwenye hifadhi zetu ili watu wa kawaida waweze kwenda kutalii. Kwa hiyo kuna haja ya kutunza utalii wa ndani katika nchi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ardhi. Maafisa wengi wa ardhi, hasa maafisa wa mipango miji wamekuwa wana matatizo makubwa sana katika maeneo yao, hawafanyi kazi zao ipasavyo matokeo yake watu wanaendelea katika ujenzi holela.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo machache, naunga mkono hoja. Naomba yale maazimio yote ambayo yametolewa na Kamati zilizohusika tuyapigie kura na yaweze kutekelezwa na Serikali.

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa
Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa
naunga mkono hoja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii
kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano, Dkt. John Pombe Magufuli, lakini kwa namna ya kipekee, naomba nimshukuru sana na kumpongeza
Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba yake. Pia niwapongeze
ndugu yangu Waziri, Mheshimiwa Jenista Mhagama na Naibu
wake kwa kazi nzuri wanayoifanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu
nitauelekeza katika maeneo yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza kuwawezesha
wananchi kiuchumi. Katika kampeni yetu ya uchaguzi ya
mwaka 2015, Ilani ya Chama cha Mapinduzi tuliahidi
kupeleka shilingi milioni 50 kwenye kila kijiji na kwenye kila
Serikali ya Mtaa. Huu ni mwaka wa pili sasa toka tulipotoa
ahadi ile. Ni vyema tukatekeleza ile ahadi. Tumebakia na
mwaka mmoja tu wa kufanya kazi, mwaka 2018, 2019
tutaenda kwenye uchaguzi, tusipotimiza ahadi ambazo
tumeziahidi wenyewe itakuwa vigumu sana mwaka 2019
kuomba kura hasa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri Mkuu nakuomba, kupitia
kwenye Serikali yetu ya Chama chetu cha Mapinduzi
tutekeleze ahadi hii muhimu kwa sababu wananchi
waliokuwa wengi kule vijijini na kule kwenye Serikali zetu za
mtaa walikuwa wanategemea wapate shilingi milioni 50 hizi
kusudi ziweze kuwatoa kwenye stage moja kwenda kwenye
stage nyingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili ambalo nataka
kuchangia ni suala la kilimo. Watanzania kati ya 67% mpaka
70% wameajiriwa katika eneo hili. Tumekusudia kwenda
kwenye uchumi wa viwanda, lakini hawa wananchi ambao
wameajiriwa kwenye eneo hili hatuwapi facilities za kutosha.
Ukiangalia pembejeo sasa hivi ni ghali sana kuliko siku za
nyuma. Kwa hiyo, ule uchumi wa viwanda ambao
tumekusudia kwenda utakuwa mgumu sana kwa sababu
malighafi ambazo tumekusudia kuzipata hatutazipata kwa
sababu wakulima hawa watakuwa hawana uwezo wa
kulima. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namuomba sana
Mheshimiwa Waziri Mkuu aliangalie sana hili eneo la pembejeo hasa mbolea kwa wakulima wetu zisiendelee
kupanda bei. Mheshimiwa Waziri Mwigulu kipindi kilichopita
alituahidi kwamba mbolea itauzwa bei rahisi, itauzwa kama
soda, lakini haya yaliyokuwa tumeahidiwa hayafanyiki na
hatuyaoni. Kwa hiyo, tunaiomba Serikali iliangalie sana eneo
hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo hili hili la kilimo
Mheshimiwa Waziri Mkuu kuna hawa wenzetu mawakala wa
pembejeo ambao wanaidai Serikali takribani shilingi bilioni
68. Huu ni mwaka wa nne wanadai hela zao na hawajalipwa
mpaka leo. Kuna baadhi ya watu wameshaanza kuuziwa
nyumba zao na wengine wanakufa. Kwa hiyo, tunamuomba
sana Mheshimiwa Waziri Mkuu atengeneze utaratibu wa
kuhakikisha hawa watu wanaodaiwa hela zao katika
maeneo haya wanalipwa baada ya kuwa wamehakikiwa
vizuri. Kuendelea kuwaacha na madeni, watakufa na hali
zao zitaendelea kuwa mbaya. Serikali yetu ni sikivu, nina
uhakika hawa watu watalipwa hela zao haraka
iwezekanavyo baada ya uhakiki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nataka
kuchangia ni suala la maji. Maji ni tatizo kubwa na kule
kwenye jimbo langu kuna tatizo kubwa sana la maji. Cha
kusikitisha ni kwamba tatizo hili limekuwa kubwa na
linaendelea kuwa kubwa siku baada ya siku.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi kubwa ya Bunge ni
kuishauri na kuisimamia Serikali. Mwaka jana katika mambo
mengi ambayo sisi Wabunge tuliishauri Serikali kwenye bajeti
iliyopita hayakutekelezwa likiwepo la kuongeza tozo ya
kutoka shilingi 50 kwenda shilingi 100. Tulikuwa na uhakika
kama tungeweza kuongeza tozo kwenye eneo hili Mfuko wa
Maji ungeendelea kuwa mkubwa na hatimaye watu wengi
wangepata huduma ya maji katika maeneo yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sana
kupitia Waziri Mkuu, muwe mnatusikiliza na sisi Wabunge.
Hakuna Mbunge ambaye anataka kero ya maji iwepo katika
maeneo yake. Kwa hiyo, tunaomba sana Waziri Mkuu kwenye jambo hili atusikilize na sisi Wabunge. Sisi Wabunge wenyewe
tumekubali kwamba ile shilingi 50 iende kwenye shilingi 100
na tutatolea majibu kwa wananchi kwa nini tumeamua
kuongeza tozo katika eneo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nilitaka
kuchangia katika sehemu ya maji ni kwamba katika Jimbo
langu la Mufindi Kaskazini kuna vyanzo vikubwa viwili vya maji.
Katika Tarafa ya Sadani kuna vyanzo vya maji vya Mto Kihata.
Hili eneo linahitaji shilingi bilioni mbili tu ili eneo hili liweze
kusaidia kutoa maji katika vijiji 19. Tumeshaleta maombi mara
kwa mara katika Wizara ya Maji lakini mpaka leo
halijashughulikiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini eneo lingine la pili ni
Tarafa ya Ifwagi. Tuna taasisi ya RDO ya watu binafsi
imetusaidia kutoa maji kwa kata takribani tano na wanalisha
vijiji takribani 30. Serikali haijatia mkono wake wowote katika
eneo hili. Ni wakati umefika sasa kwa Serikali yetu kutia mkono.
Kwa masikitiko makubwa kwenye eneo hili inafika wakati
hawa wanatozwa VAT, kwa hiyo, badala ya kuwapa moyo
wanakosa moyo wa kushughulikia eneo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nataka
kulizungumzia ni barabara. Tuna barabara kubwa mbili katika
Jimbo langu la Mufindi Kaskazini ambazo nataka mziangalie
kwa macho mawili. Barabara moja ni kutoka Kinambo A –
Isalavanu – Saadani - Madibila - Lujewa. Mwaka 2010 na 2015
barabara hii iliingia kwenye Ilani ya uchaguzi, kwa maana
ya vipindi vyote vitano imeingia kwenye Ilani ya Uchaguzi
lakini hata kilometa moja haijawahi kutengenezwa. Kwa hiyo,
tunakosa majibu ya kuwajibu wananchi kwenye maeneo
yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamuomba sana Waziri
Mkuu kwenye jambo hili aliangalie. Nakuomba Waziri Mkuu
ufanye ziara katika Wilaya ya Mufindi kwa sababu hakuna
kiongozi yeyote wa kitaifa ambaye amekuja katika Wilaya
ya Mufindi kujionea hali halisi. Nataka nikuambie miongoni
mwa maeneo ambayo tunapata kura nyingi CCM ni Wilaya ya Mufindi. Wananchi wa Wilaya ya Mufindi wasije wakakata
tamaa kwa sababu yale mambo ambayo tumeyaahidi
hayafanyiki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine tulilokuwa
tunaomba mtusaidie ni barabara ya kutoka Johns Corner -
Mgololo na barabara ya kutoka Mchili – Ifwagi – Mdabulo –
Ihanu - Tazara - Mlimba. Barabara hii inaunganisha Wilaya
mbili na mikoa miwili. Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi haina
uwezo wa kuitengeneza barabara hii.
Kwa hiyo, tunaomba sana ipandishwe hadhi na
tumejitahidi kadri ya uwezo wetu kupeleka barua kupitia
kwenye Road Board ya Mkoa, lakini kwa bahati mbaya
mpaka leo Waziri mhusika hajawahi kutujibu kwenye eneo
hili.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Dr. Thomas D. Kashililah

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

Hon. Grace Sindato Kiwelu

Special Seats (CHADEMA)

Supplementary Questions / Answers (5 / 0)

Contributions (5)

Profile

Hon. Dr. Ally Yusuf Suleiman

Mgogoni (CUF)

Contributions (1)

Profile

View All MP's