Parliament of Tanzania

Bunge la Tanzania kuanzisha urafiki wa Kibunge na Bunge la UAE

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai ametembelea Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu na kufanya mazungumzo na Spika mwenzake, Mhe Dr Amal Al Qubaisi ambapo amewasilisha mapendekezo rasmi ya kuanzisha Urafiki wa Kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu.


Mhe Spika Al Qubaisi ambaye ni Spika wa kwanza mwanamke katika nchi zote za Mashariki ya Kati kwa niaba ya Bunge la nchi hiyo amekubali mapendekezo hayo na kutoa mwaliko kwa Wabunge wa Tanzania kutembelea Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu Kwa nia ya kuona namna UAE ilivyopiga hatua.

Kabla ya kufanya ziara hiyo ya Kibunge Spika Ndugai alikuwa nchini Nigeria kuhudhuria katika Mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika uliofanyika Mjini Abuja ambapo katika mkutano huo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Maspika na Viongozi wa Bunge katika Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika

Kwa wadhifa huo, Mhe Ndugai ataongoza Maspika wenzake toka Mabunge na Mabaraza ya kutunga Sheria 63 yaliyoko katika nchi 18 za Jumuiya ya Madola kwenye Bara la Afrika. Wadhifa huo ni wa miaka miwili kuanzia sasa hadi mwaka 2019 kutakapofanyika uchaguzi mwingine.

Aidha mara baada ya ziara katika Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe Spika alielekea Tehran kushiriki kuapishwa kwa Rais wa 12 wa Iran ambae kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo, Rais huapishwa Bungeni.

Mheshimiwa Ndugai yuko Tehran kwa mwaliko wa Spika wa Bunge la nchi hiyo akiwakilisha Maspika wa Afrika.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's