Parliament of Tanzania

Bunge laahirishwa hadi Aprili 2

Mkutano wa kumi na nne wa Bunge la kumi na moja umeahirishwa hadi tarehe 2 Aprili, 2019 wakati ambapo Bunge litakutana kwa ajili ya Bunge la Bajeti Jijini Dodoma.

Akisoma hotuba ya Kuahirisha Bunge Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku 21 kwa viwanda vyote vinavyozalisha vileo nchini viwe vimefunga mfumo ukusanyaji kodi kwa kutumia stempu za kielektroniki.

Pia ameziagiza Wizara na Taasisi zote za Umma ziwe zimejiunga na Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji na usimamizi wa maduhuli (GePG) kabla ya Juni mwaka huu.

Waziri Mkuu amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) isimamie uwekaji wa mifumo hiyo na ifikapo februari 28, 2019 kila kiwanda kiwe kimefunga mfumo huo.

“Naielekeza TRA kusimamia uwekaji wa mifumo ya kukusanya kodi za vileo kwa kutumia stempu za kielektroniki kwa viwanda vyote vinavyozalisha vinywaji hivyo.”

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuongeza mapato na kuimarisha usimamizi wa matumizi ya fedha na rasilimali za umma ili kufikia malengo.

Mkutano wa Kumi na Nne wa Bunge la Kumi na Moja ulianza Jumanne tarehe 29 Januari 2019 na ambapo pamoja na mambo mengine kikao cha kwanza cha Mkutano huu kilianza kwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Mhe. Abdallah Ally Mtolea kula kiapo cha Uaminifu.

Aidha, katika Mkutano huu wa Kumi na Nne, wastani wa maswali 125 ya Kawaida yaliulizwa na Wabunge na kupatiwa majibu na Serikali Bungeni.

Kwa upande mwingine katika Mkutano huu ambao ulikuwa mahsusi kwa ajili ya Kamati za Kudumu za Bunge kuwasilisha taaarifa zao za mwaka, Kamati za Kudumu za Bunge 15 ziliwasilisha taarifa hizo kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 117(15) ya Kanuni za Bunge:-

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa; na

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's