Parliament of Tanzania

Bunge laahirishwa hadi Aprili 4

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameahirisha Mkutano wa Sita wa Bunge hadi Aprili 4, mwaka huu huku akizungumzia masuala mbalimbali ikiwemo mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya.

Akitoa hojoa yaKuahirisha Bunge, Februari 10, mwaka huu, alisema Serikali itapambana na janga la dawa za kulevya kwa dhati bila kumuonea mtu yeyote na kwamba itatenda haki kwa kuzingatia misingi ya sheria.

“Lengo la Serikali ni kuwasaidia walioathirika na dawa za kulevya na kuwachukulia hatua kali wale waliowaathiri kwa maana ya wauzaji na wasambazaji. Dhamira ya Serikali ni kupambana na janga hili kwa dhahiri na kwa dhati bila kumuonea mtu yeyote na kwa kuzingatia misingi ya sheria na haki,”alisema.

Alisema hadi sasa jumla ya Watanzania 515 wamekamatwa na kufungwa gerezani kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya Dawa za kulevya katika nchi mbalimbali ikiwemo China, Brazil, Iran, Ethiopia na Afrika Kusini.

Akizungumzia hali ya chakula nchini, aliwagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuwahamasisha wananchi kulima mazao yanayokomaa mapema kwa kutumia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi nchini.

“Pia nawashauri wananchi kutumia vizuri chakula walicho nacho na nawasihi wafanyabishara wasifiche chakula bali wasaidie kuchukua chakula kutoka kwenye maeneo yenye chakula cha ziada na kukisafirisha kwenda kuuza kwenye maeneo yenye upungufu,” alisema.

Kuhusu hali ya ulinzi na usalama nchini Waziri Mkuu alisema ni ya kuridhisha na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama viko imara na katika hali ya utayari katika kulinda amani na utulivu.

Alisema Operesheni za kupambana na uhalifu kama vile unyang’anyi wa kutumia silaha, kuteka magari na matishio mengine ya kiusalama vimefanyika katika jitihada za kupambana na uhalifu nchini.

Katika hotuba yake Waziri Mkuu pia alizungumzia masuala mbalimbali ikiwemo usalama barabarani, udhibiti wa silaha, wahamiaji haramu sekta ya elimu , sekta ya ardhi, sekta ya mifugo, sekta ya afya pamoja na shughuli mbalimbali zilizofanyika Katika Mkutano wa Sita wa Bunge la 11.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's