United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Agizo hilo limetolewa Mkoani Iringa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Aloyce Kwezi wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa Kupanga, Kupima ardhi wa Igumbilo ambao umetekelezwa na Manipsaa ya Iringa kwa kutumia fedha hizo za mkopo walizopewa na Wizara ya Ardhi.
‘‘Kimsingi kazi ya upangaji miji
ni jukumu la kila Halmashauri na siyo Wizara hivyo ni lazima mtambue kwamba
Wizara iliwasaidia katika kutekeleza majukumu yenu ya msingi kuwakopesha fedha
na ndiyo maana mkopo huo haukuwa na riba ili mkapange, mpime na mmlikishe
wananchi ardhi kwenye Halmashauri zenu’’ alisema Kwezi.
Kwa upande wake Mhe. Angelina
Mabula Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
aliishukuru Kamati hiyo ya Bunge na kusema nia ya Serikali kupitia Wizara ni
kuona kila kipande cha ardhi nchini kinapimwa na hivyo Wizara iliamua
kuziwezesha Halmashauri zenye dhamana ya upangaji miji katika maeneo yao kwa
kuzikopesha kiasi cha fedha ili zitumike katika utekelezaji wa kazi hizo za
upangaji,upimaji na umilikishaji ardhi na kisha kuzirejesha.