Parliament of Tanzania

Kamati yaishauri Serikali kuwasaidia Vijana wanaokaa karibu na Migodi

Kamati yaishauri Serikali kuwasaidia Vijana wanaokaa karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita

Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeishauri Serikali kuangalia upya namna ya kuwasaidia vijana wanaozunguka Mgodi wa Dhabu wa Geita kwa kuwapa maeneo ya uchimbaji.


Ushauri huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dkt Dalali Kafumu wakati Kamati yake ilipotembelea Mgodi wa dhahabu wa Geita.


"Nafikiri serikali iangalie namna ya kuwasaidia wachimbaji wadogo hao kwa kuwatafutia maeneo ya uchimbaji badala ya kutegemea miamba taka(magwangala) ambayo hayana dhahabu.


" Najua kuna mradi wa Benki ya Dunia ambao unasaidia wachimbaji wadogo huo ndio ungeongezewa nguvu zaidi badala ya kufikiria kuwapa masalia ya mgodi" alisema Dkt Kafumu.

Dkt Kafumu pia ameshauri Serikali kusimamisha mradi huo wa miamba taka kwa kuwa kwa kuweka kukaribu na wanachi ni kuchafua mazingira na kuhatarisha maisha ya wachimbaji hao wadogo.


" Kuendelea kuweka magwangala hapa kunachafua mazingira badala ya kusaidia wananchi,angalieni mradi huu ikiwezekana muusimamishe"


Aidha, Dkt Kafumu alisema Kamati imeridhishwa na namna Mgodi wa Dhahabu wa Geita unavyotunza mazingira hasa kwenye uhifadhi wa taka zenye kemikali.


"Tumeona jinsi wanavyodhibiti taka zenye kemikali kwa namna kwamba hakuna maji yanayotoka nje, lakini mmeweka pia vituo vya kutazama maji yanayochujwa. Kwa namna fulani wabunge wameridhika jinsi Mazingira yanavyotunzwa mgodini hapa" alisema Dkt Kafumu.


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, na Mazingira imetembelea Mgodi wa Dhahabu wa Geita ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kukagua miradi ya mendeleo ya Wizara/Idara zinazosimamiwa na Kamati husika.


Kwa upande mwingine, Kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara, Uwekezaji na Mazingira imeitaka Serikali kulipa deni la dola million 11, inayodaiwa na mgodi wa Wiliamson Diamonds.

Akitoa maagizo hayo , Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk. Dalay Kafumu alisema deni hilo linatokana na tozo ya ongezeko la thamani (VAT) la tangu mwaka 2009.

Dkt Kafumu alisema Kamati yake itafuatilia ili fedha hizo zilipwe na kumuwezesha mwekezaji kufanya shughuli zingine za maendeleo.

“Utaratibu ni kwamba mwekezaji ambaye ni kampuni ya Petra analipa kwanza VAT kisha Serikali inarudisha fedha hizo, sasa tangu mgodi ulipe, Serikali haijalipa. Kupitia Kamati hii tutafuatilia ili waweze kulipwa fedha hizo na Serikali” alisema Dkt Kafumu.

Mbali na deni hilo mwenyekiti huyo alizungumzia pia changamoto ya kuwepo mamlaka nyingi za Serikali ambazo zote zinafanya ukaguzi katika mgodi huo jambo ambalo ni linazidisha gharama za uendeshaji kwa mgodi huo.

“Mamlaka hizo zinaingiliana katika kufanya kazi, hali hii inasababisha uwajibikaji kuwa mdogo, tutaishauri Serikali kuhusu suala hili,” alisema.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya Williamson Diamonds Limited, Arlen Loehmer alisema kuwa wamekuwa wakipata hasara katika uendeshaji na na kushindwa kufikia malengo kwa kuwa tangu waumiliki mgodi huo mwaka 2009 hawajawahi kulipwa fedha za VAT na serikali.

Alisema changamoto nyingine ni kuwepo kwa mamkala nyingi zinazofanya ukaguzi katika mgodi huo na kuiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza mamlaka hizo kwani zinaupa gharama kubwa mgodi huo.

Naye Meneja uzalishaji, Ayoub Mwenda alisema tangu mwaka 2009 mpaka sasa wameweza kuwekeza kiasi cha Dola milioni 137.

“Mapato kwa sasa yameongezeka kutoka Dola millioni 41.9 hadi Dola milioni 78.9 kuanzia mwaka 2012 hadi 2016 na bado mgodi una uwezo wa kuzalisha zaidi ya miaka 50 ijayo”alisema Mwenda.

Pia alisema kuwa mgodi unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kukatika kwa umeme wakati mwingine kukosa nguvu hivyo mitambo kushindwa mitambo kuwaka, kupungua kwa bei ya Almas soko la dunia na wavamizi hasa vijana wasiokuwa na kazi (wabeshi).

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's