Parliament of Tanzania

Mhe Spika apokea msaada wa vitabu 950 kwa ajili ya Ofisi ya Bunge

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai amepokea msaada wa vitabu 950 vya kada mbalimbali vilivyotolewa na Asasi ya Kiraia ya TAN. TRUST kwa ajili ya matumizi ya Bunge.

Halfa hiyo ya kukabidhiana vitabu hivyo ilifanyika Mjini Dodoma katika Ukumbi wa Mhe Spika huku ikishuhudiwa na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Ofisi ya Bunge.

Akizungumza mara baada ya kupokea vitabu hivyo, Mheshimiwa Ndugai alitoa shukrani kwa Asasi hiyo kwa kulikumbuka Bunge na kwamba vitabu hivyo vitasaidia kuongeza tija katika shughuli mbalimbali zinazofanywa na Bunge.

“Mtusaidie pia kupeleka shukrani zetu kwa wafadhili kwa kutupatia vitabu ambavyo vingine msingi wake ni masuala ya sheria na kama mjuavyo Bunge kazi yake pia ni kutunga sheria mpya na kurekebisha sheria nyingine.

Hivyo vitabu hivi vitawasaidia wabunge, wafanyakazi na wanafunzi wa vyuo wanaokuja Bungeni kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo katika utendaji kazi wao,” alisema.

Aidha, alisema vitabu hivyo pia vitasaidia kuboresha maktaba ya Bunge na hivyo kuwavutia watu wengi zaidi kuitumia.

“Bado tunahitaji vitabu vya Nyanja nyingi zaidi, tunaahidi hivi mlivyotuletea leo tutavienzi na kuvitunza ili vikae kwa muda mrefu uwezekanavyo,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa PEN. TRUST, Ndugu Mungwe Athuman akizungumza kabla ya kukabidhi vitabu hivyo alisema msaada huo kwa Bunge lengo lake ni kuboresha utawala bora.

“Vitabu tunavyotoa leo ni vya aina nyingi na Nyanja mbalimbali, ni tegemeo letu kwamba vitakuwa chachu na nyenzo muhimu kwatika kuwajengea uwezo Waheshimiwa Wabunge wetu wa kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi,” alisema.

Alisema tangu mwaka 2004, Asasi hiyo imeshatoa msaada wa vitabu zaidi ya 400,000 kwa shule, hospitali, vyuo na taasisi mbalimbali nchini kupitia kwa wafadhili mbalimbali.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's