Parliament of Tanzania

MHE. SPIKA AWAAPISHA WABUNGE WAWILI WALIOTEULIWA NA MHE. RAIS DESEMBA 5 MWAKA HUU

SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai amewaapisha Waheshimiwa Wabunge wawili walioteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Desemba 5 mwaka huu.

Wabunge hao walioapishwa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma ni Dkt.Dorothy Gwajima na Mhandisi Leonard Chamuriho.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha wabunge hao, aliwapongeza kwa uteuzi na kuahidi kuwapa ushirikiano huku akiwataka Wabunge wote waliapishwa kuendelea na shughuli zao popote walipo.

Aidha, alimpongeza Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Sharrif Hamad kwa kuapishwa kutumikia nafasi hiyo huku akisema uapisho huo unadhihirisha yale yaliyoelezwa na Rais Magufuli kuwa uchaguzi umekwisha.

Mheshimiwa Spika pia alizungumzia maneno yanayozungumzwa na baadhi ya watu kwamba amefanya kosa kuwaapisha Wabunge wa Viti Maalum 19 kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema).

Alisema yeye kazi yake ni kuapisha Wabunge wote ambao analetewa majina yao kutoka Tume ya Uchaguzi (NEC) na ameshafanya hivyo na kwamba kama kuna walakini Mahakama ndiyo inaweza kumuambia hatua za kuchukua na si vinginevyo.

Awali akimkaribisha Mheshimiwa Spika, Naibu Spika, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson aliahidi kuwa Bunge litawapa ushirikiano Wabunge Wateule ili waweze kutekeleza majukumu yao.

Mheshimiwa Naibu Spika pia alimpongeza Mheshimiwa Ndugai kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya sheria ambazo zimekuwa zinawanufaisha Watanzania.

Naye Dkt. Gwajima alisema amepokea uteuzi alioufanya Rais kwa uaminifu na kwamba anatambua kazi iliyo mbele yake ni kubwa, ni kazi inayotaka uzalendo, ujasiri, umakini na ushirikiano.

Kwa upande wake Dkt. Chamuriho alisema anatambua majukumu aliyopewa ni makubwa na mazito hivyo anaomba ushirikiano ili aweze kuyatekeleza kama inavyotarajia kwa uaminifu, uadilifu na kwa kuwaajibika.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament