Parliament of Tanzania

Mkutano wa Bunge la Bajeti waanza Mjini Dodoma

Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge umeanza Jumanne tarehe 3 Aprili 2018 na unatarajiwa kumalizika tarehe 29 Juni 2018 Mjini Dodoma. Mkutano huu utakuwa ni mahususi kwa ajili ya mijadala na kupitisha Bajeti ya Serikali pamoja na kujadili Hotuba ya hali ya Uchumi wa Taifa itakayowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango.

Aidha katika mkutano huu, Bunge litajadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara zote kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 na Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/19.

Shughuli nyingine zitakazofanyika katika Mkutano huo ni kama ifuatavyo:-

KIAPO CHA UAMINIFU

Kutakuwa na Kiapo cha Uaminifu kwa Waheshimiwa Wabunge wawili waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni ambao ni:-

i.

Mhe. Maulid Abdallah Mtulia

- Kinondoni

ii.

Mhe. Dkt. Godwin Oloyce Mollel

- Siha

UCHAGUZI WA WENYEVITI WA BUNGE

Katika Mkutano huu, Bunge litafanya uchaguzi wa Wenyeviti watatu wa Bunge. Uchaguzi huu ni kutokana na Wenyeviti waliokuwepo kumaliza muda wao kwa Mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge.

MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI.

Vilevile katika Mkutano huu wa Bunge, jumla ya Miswada ya Sheria miwili itawasilishwa Bungeni ambayo

ni:-

(i) Muswada wa Sheria ya Fedha za Matumizi wa Mwaka 2018 (The Appropriation Bill, 2018).


(ii) Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2018 (The Finance Bill, 2018)

MASWALI.


Katika Mkutano huu jumla ya Maswali ya kawaida 515 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge wastani wa maswali 72 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa kwa siku za Alhamisi.


MAAZIMIO.

Pia katika mkutano huu, Bunge litajadili na kupitisha Azimio la Kuridhia Makubaliano ya Paris kuhusu Kuboresha Utekelezaji wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's