Parliament of Tanzania

Serikali yawasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/18

SERIKALI imewasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti kwa mwaka wa Fedha, 2017/18 ambapo imepanga kutumia Sh. Trilioni 31.6.

Taarifa hiyo imewasilishwa Bungeni leo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango katika Mkutano wa Wabunge wote kwa mujibu wa Kanuni ya 97 ya Kanuni za Bunge.

Dk. Mpango alisema kati ya kiasi hicho kilichopangwa kutumiwa, fedha zinazotokana na Mapato ya Ndani ni Sh. Trilioni 19. 9 sawa na asilimia 63 huku washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia Sh. Trilioni 3.9 sawa na asilimia 12. 6 na fedha nyingine ni mikopo kutoka soko la ndani.

Aidha, alisema Serikali inatarajia kutumia Sh. Trioni 19.7 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh. Trilioni 11. 9 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Akibainisha baadhi ya maeneo ya kipaumbele katika bajeti ya mwaka 2017/18, Dkt. Mpango alisema ni pamoja na ujenzi wa reli ya kati, kuhuisha Shirika la Ndege Tanzania, ujenzi wa mgodi wa chuma na Kiwanda cha Chuma Liganga Njombe na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma.

“Vipaumbele vingine ni uanzishwaji wa Kanda Maalum ya Kiuchumi Tanga, Bagamoyo, Kigoma, Ruvuma na Mtwara, kuendeleza Mradi wa Liquified Natural Gas, kuhamishia shughuli za Serikali Kuu Makao Makuu Dodoma na kuendeleza Shamba la Kilimo na Uzalishaji Sukari Mkulazi,” alisema.

Kwa upande wake Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai aliiagiza Kamati ya Bajeti kuyafanyia kazi mapendekezo hayo yaliyowasilishwa na Serikali na kuzishauri Kamati za Bunge za Kisekta na Serikali.

“Vilevile mara baada ya kupokea mapendekezo haya, Kamati zote ziandae ratiba ya kuchambua Bajeti za Wizara wanazozisimamia na kazi hii imalizike kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Saba wa Bunge kwa kuwa haiahirishiki,” alisema.

Aidha, aliwataka Mawaziri, makatibu wakuu na watendaji wa Serikali kuhakikisha wanashilikiana na Kamati katika uchambuzi wa bajeti za wizara zao.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's