Parliament of Tanzania

SPIKA AWAAPISHA WABUNGE 19 VITI MAALUM CHADEMA

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai amewaapisha wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha, Spika wa Bunge alieleza utaratibu wa kikatiba uliotumika kuwapata wabunge hao pamoja na utaratibu wa kikanuni wa kuwaapisha katika kipindi ambacho hakuna Mkutano wa Bunge.

Aidha, aliwaahidi wabunge hao kuwalinda na kuwapa ushirikiano wa kila namna licha ya uchache wa Bungeni.

“Nawapongeza sana na mimi kama Spika jukumu langu ni kuwalinda walio wachache, hivyo naahidi kuwalinda na kuwapa ushirikiano wa kila hali wakati wa kutekeleza majukumu yenu,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge wenzie, Mheshimiwa Halima Mdee alimshukuru Spika kwa kuwapokea na kuahidi kufanya kazi kwa bidiii kuwatumikia Watanzania.

Waheshimiwa Wabunge waliokula kiapo ni Halima Mdee, Grace Tendega, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Esther Bulaya, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.

Wengine ni Agnesta Kaiza, Nusrat Hanje, Asia Mohamed, Felister Njau na Stela Fiyao.


Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament