United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatile amewasili Dodoma kwa ziara ya siku tatu katika Bunge la Tanzania na baadhi ya maeneo ya Jiji la Dodoma.
Mhe. Donatile aliwasili Juni 9,
mwaka huu na kupokelewa na wenyeji wake Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job
Ndugai, Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, baadhi ya Viongozi na Maafisa wa
Bunge.
Akizungumza kuhusu ugeni huo Spika
Ndugai alisema kumekuwa na mahusiano mazuri kati ya Bunge la Rwanda na Bunge la
Tanzania na mara kadhaa Kamati za Bunge la Tanzania zimekuwa zikienda Rwanda na
kujifunza jinsi wanavyoendesha shughuli zao na sasa nao wamepata fursa ya kuja Tanzania
kujifunza.
Spika wa Rwanda ambaye ameambatana
na wabunge wawili na Maofisa watatu anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo
na Spika wa Bunge, Naibu Spika, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Wabunge
wanawake na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama