United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Y. Ndugai (Mb), anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mhe. Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatare kilichotokea Jijini Dar es Salaam alfajiri ya leo Jumatatu tarehe 20 Aprili, 2020.
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa
taarifa za kifo cha Mhe. Rwakatare. Natoa pole kwa wafiwa wote wakiwemo familia
ya marehemu, ndugu, jamaa, Waheshimiwa Wabunge na Waumini wa Kanisa la Mlima wa
Moto (Mikocheni B Assemblies of God). Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na
subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Mhe. Spika.
Ofisi
ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi
na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali
pema peponi. Amina.