You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Session No Seating No Contribution Date Contribution To
2 5 14 February 2011 Hoja ya Kujadili Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Kufungua Bunge Jipya, 2010
Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Nami nianze kwa kuwashukuru wananchi wa Ngara, kwa kuniamini na kunipa ridhaa ya kuwawakilisha katika Bunge lako Tukufu. Hotuba hii ni muhimu sana. Rais alipokuja Ngara wakati wa kampeni wananchi walimshukuru sana kwa kazi nzuri aliyoifanya katika miaka mitano iliyopita na wakamuahidi kumpigia kura nyingi na kwa taarifa ya Bunge hili Ngara ilikuwa ya kwanza katika Mkoa wa Kagera katika kumpigia Rais kura nyingi na tukawa watano Kitaifa. Mimi I am very proud of that.

Mheshimiwa Spika, wenzangu wamezungumzia vipaumbele karibu vyote 13. Mimi naviunga mkono, vyote ni muhimu sana, nadhani tutakavyoendelea, tutaweza kuzungumzia vipaumbele hivyo.

Mheshimiwa Spika, mimi ni Mwalimu by profession. Naomba nizungumzie elimu, lakini sitazungumzia yale ambayo Waheshimiwa Wabunge wameshayazungumzia. Nitazungumzia jambo lingine muhimu sana tofauti na yale ambayo yameshazungumzwa na Waheshimiwa Wabunge. Najua Waheshimiwa Wabunge katika kuzungumzia elimu wamesema kuna matatizo ya uhaba wa Walimu, maslahi madogo ya Walimu, vitabu vichache, madarasa yanahitaji kuongezwa, lakini mimi kama Mwalimu nimefanya utafiti mdogo kule Ngara kwa kuzungumza na Walimu mbalimbali, nikaona kwamba kuna tatizo la ufundishaji, teaching yenyewe inaweza ikaleta matatizo na kuathiri matokeo ya mitihani ambayo mnayaona.

Mheshimiwa Spika, kabla sijaenda Chuo Kikuu, nilisomea Ualimu Butimba Teacher’s College lakini pia nilipokwenda Chuo Kikuu, nilisoma Elimu pamoja na Management and Administration. Sisi wakati huo tumeingia Chuo Kikuu mwaka 1968 – 1971, tulijizatiti katika psychology of education, philosophy of education na methodology. Mtaalamu mmoja ambaye nataka kumzungumzia sasa hivi kwa kazi yake aliyoifanya alikuwa anaitwa Prof. Benjamin Bloom. Benjamin Bloom alikuwa a great psychologist huko Marekani. Prof. Bloom anasema kwamba wewe Mwalimu unapokwenda darasani ujue kwamba kuna six levels of learning ambazo Mwalimu unatakiwa kuzizingatia. Nizitaje halafu nitafafanua kwa sababu zinazidiana. Hatua ya kwanza ni knowledge, you will impart knowledge to the students or to the pupils. Pili, ni comprehension, lazima kama Mwalimu uhakikishe kwamba watoto wameelewa. Hii nitazungumzia kwa kirefu zaidi. Ya tatu ni application, kuona kama watoto wanaweza ku-apply hizo concepts, principles na hizo theories ambazo wamefundishwa. Ya nne, ni analysis, lazima uhakikishe kwamba watoto unawafundisha namna ya kuchambua mambo, you develop their analytical abilities. Kwa mfano, unapofundisha Katiba ya Tanzania, ukishafundisha unamwuliza mtoto Katiba hiyo imegawanyika katika sehemu gani? Watakueleza sehemu ya Serikali ambayo ni Executive branch, sehemu ya Mahakama ambayo ni Judiciary, sehemu ya Bunge ambayo ni Legislative Branch. Unaanza kuwafundisha namna ya kuanza ku-analyze. To analysis kwa Kiingereza maana yake ni to break something into parts. Ukitoka kwenye analysis unakwenda kwenye synthesis, Mwalimu lazima darasani uhakikishe kwamba mtoto anaweza akayaweka pamoja yale yote uliyoyafundisha. To synthesize ni to put things together, ni tofauti na analyse ya ku-break something into parts. Ya mwisho ni evaluation. Wewe kama Mwalimu lazima uhakikishe kwamba yale malengo uliyokuwa nayo wakati wa kufundisha umeyafikia.

Mheshimiwa Spika, vijana wa siku hizi sijui kama wanakwenda kwa utaratibu huo. Mimi nilikuwa Mwalimu na nilikuwa nahakikisha kwamba nafuata hizo six levels. Baada ya kusema hayo ya knowledge, huwezi ku-impart knowledge kama wewe huna knowledge. Kwa hiyo, Mwalimu lazima aandaliwe vizuri, apewe knowledge ya kutosha. Kama wewe ni mtaalamu wa Chemistry unaweza ku-impart knowledge ya Chemistry?

Mheshimiwa Spika, pia Mwalimu lazima ajue kwamba darasani kuna watoto wa aina tatu. Wa kwanza ni normal students, wa pili ni bright students na wa tatu ni slow learners. Naomba kama kuna Waziri wa Elimu anisikilize vizuri. Kuna tatizo la slow learners ambalo linaweza kusababisha matatizo makubwa katika mitihani. Hizi syllabus tunazozungumzia na curriculum, zinatengenezwa kwa ajili ya normal students na sisi Walimu tunasema a normal students ni yule ambayo ana IQ ya 100, Intelligence Quotient ya 100. Bright student’s wanakwenda beyond 100, slow learners wako kwenye 75 au 80. Kwa hiyo, Mwalimu lazima ajue matatizo hayo na aweze ku-address tatizo la slow learners. Nashauri Wizara ya Elimu, kwa kuwa tatizo la slow learners ni kubwa sana, watafute wataalam ambao wanaweza kuendesha semina za (TOT) Training of Trainers, ili hawa watakaokuwa trained waweze kusaidia hawa slow learners. Hilo ni tatizo.

Mheshimiwa Spika, lakini pia kuna three other factors ambazo zina-affect learning. Moja ni personal factors, mtoto umjue vizuri matatizo yake, huko nyumbani anakotoka na kadhalika. Environmental factors na mwisho ambalo nataka kulizungumzia ni language barrier. Kiingereza ni tatizo katika nchi yetu. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani amezungumzia kwamba anafikiri tatizo la language limekuwa ni problem katika kushindwa watoto wengi katika mtihani uliopita.

Mheshimiwa Spika, sisi tulipokuwa tunasoma, tulikuwa tunaambiwa kwa Kiingereza “You must frame examination questions in the examinee language not in the examiners language”. Tafsiri yake ni kwamba “unapotunga mitihani uitunge kwa lugha ya mtahiniwa sio kwa lugha yako kama Mwalimu”. Kwa hiyo, kwa mtahiniwa unatakiwa utumie lugha rahisi. Nimeona nizungumzie tatizo hilo kwa sababu nafikiri Wabunge wengine wamezungumzia matatizo ya Walimu lakini hilo nalo ni tatizo, teaching six levels of learning ni muhimu sana.

Mheshimiwa Spika, katika elimu pia nizungumzie Elimu ya Watu Wazima ,siwezi kuishia kwenye kuzungumzia elimu ya msingi, sekondari na vyuo vikuu, tunahitaji pia kuhakikisha kwamba tunarudisha kisomo cha watu wazima. Mimi nimeshiriki sana katika kisomo cha watu wazima kwenye miaka ya 1970. Wananchi, wazee, kinamama na kinababa wakitoka mashambani walikuwa wanakwenda kujifunza kusoma na kuandika. Tukafikia kwenye level ya literacy ya 95% na tukawa wa kwanza duniani kwenye miaka 1970 na 1980. Wakati huo level of literacy Marekani ilikuwa 85% tulikuwa tunawazidi. Mwaka 1986/87 nilikwenda kusoma Marekani nikawa nawaambia you can be a super power lakini sisi tunawazidi kwenye literacy, sisi 95% ninyi ni 85%. Sasa juzi nimetembelea Idara ya Elimu kwa Njia ya Posta nikawauliza hivi tumetoka 95% tumefika wapi? Wakasema Mheshimiwa Ntukamazina kwa kweli official figure imefikia 68% lakini tu nadhani tuko chini zaidi. Kwa hiyo, naomba Wizara ya Elimu irudishe kisomo cha watu wazima. Jambo hili limejidhihirisha mwaka jana wakati wa uchaguzi. Wakati wa Uchaguzi, watu wengi wazee wameandikiwa majina. Walikuwa wanaulizwa, mnamtaka nani, wakijibu kama wanamtaka Ntukamazina Mawakala wanaandika Rugumyamheto au Banyikwa. Kwa hiyo, unaweza ukapoteza kura nyingi sana kwa sababu illiteracy imeanza kuwa kubwa sana.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ningependa nilizungumzie kwenye elimu ambalo Rais amelizungumzia ni masomo ya sayansi. Tatizo tulilonalo, vijana wanaomaliza Kidato cha Sita kama wamesoma sayansi wengi wanakwenda Udaktari au Uhandisi, wachache wanakwenda kuchukua Bachelor of Science with Education kama zamani. Kwa hiyo, nadhani vijana wahamasishwe wachukue Bachelor of Science With Education ili waweze kwenda kufundisha sayansi kwenye shule mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine kwenye upande wa elimu ambalo nataka niiombe Wizara ya Elimu ilifikirie au Serikali, naomba tumuenzi Marehemu Baba wa Taifa ambaye alikuwa na ndoto nyingi sana, aliona mbali sana, akasema tuanzishe a Science Village. Akatoa fedha na akamteua Marehemu Prof. Shayo aanzishe kijiji hicho lakini bahati mbaya kijiji hicho hakikuanzishwa. Lengo la Marehemu Baba wa Taifa lilikuwa ni kwamba tuanzishe kijiji hicho, tuchukue vijana wenye akili sana, tuwafundishe sayansi kwenye kijiji hicho na kuwepo na library …

Kengele ya pili? Nimalizie kwa kusema tuanzishe institution mbili, National Service pamoja na Leadership College itasaidia vijana wetu…