You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Mdee, Halima James[CHADEMA]

Kawe Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
8 107 FINANCE AND ECONOMIC AFFAIRS Finance/Treasury 29 June 2012
Mheshimiwa Spika
nashukuru. Kwa kuwa Serikali imechukua zaidi ya miaka
mitatu kuweza kujua kama washtakiwa wana kesi ya
kujibu ama la, na kwa kuwa utaratibu huu ukiachwa
ukiendelea maana yake kesi ya msingi inaweza
ikachukua zaidi ya miaka mitatu mpaka minne, na kwa
kuwa suala la DECI linahusu maslahi ya Watanzania
wengi maskini.

Je, Serikali haioni kwamba baada ya kujulikana
kama kuna kesi ya kujibu ama la, kuweka muda
maalum ambao kesi ya DECI inatakiwa iishe?

La pili, mwaka 2009 aliyekuwa Waziri wa Fedha
Mheshimiwa Mkulo alikiri kwamba kuna vigogo wa
Serikalini wanaohusika na DECI, lakini vile vile kuna
fedha za umma ambazo ziliingizwa kwenye DECI kwa
malengo ya kuvuna ili kile kiasi cha Serikalini kirudishwe
Serikalini. Lakini kwa taarifa ambazo tunazo, kesi
iliyopo inayohusika na DECI ni ya wale wachungaji
watano. Nilitaka Serikali iniambie kufuatia tamko lile la
Mheshimiwa Mkullo, ni vigogo wangapi wa Serikali
wameshachukuliwa hatua ambao walihusika na suala
hili la DECI kwa mantiki ya kuweka fedha za Umma.
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  107  SESSION #  8
mp Answer From Hon.Mbene, Janet Zebedayo
FINANCE AND ECONOMIC AFFAIRS
NAIBU WAZIRI WA FEDHA:

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala zima la kuwa
washutumiwa wana kesi ama hawana hiyo itabidi
Mahakama yenyewe iamue na ndipo hatua
zinaotakiwa kuendelea za kisheria zitaendelea
kufanyika.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na kuiwekea
Mahakama kikomo cha kesi hii isikilizwe kwa muda upi
naamini hiyo ni juu ya Mahakama yenyewe, sisi kama
Serikali hatuwezi kuingilia muhimili huo na
kuwashurutisha wafanye hiyo kazi kwa shinikizo letu sisi.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na vigogo wangapi
waliochukuliwa hatua, naomba nikiri kuwa sina taarifa kuwa kuna vigogo waliohusika. Lakini naamini kutokana na kesi kuwa ipo Mahakamani hata wao
watachukuliwa hatua zinazopaswa kufuatana na
sheria zinavyosema.