You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Kitandula, Dunstan Luka[CCM]

Mkinga Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
10 110 LIVESTOCK AND FISHERIES DEVELOPMENT Forestry/Fishery 8 February 2013
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ambayo hayaridhishi na yamekwepa kujibu swali nina maswali mawili ya nyongeza. Nchi kama Vietnam inaingiza mapato kwa sekta ya uvuvi yanayokaribia dola milioni 5,200 kwa mwaka nchi kama Thailand inaingiza dola milioni 3,300 kwa mwaka. Nchi kama Iran kwa mwaka uliyopita imeingiza dola milioni 400 kwa ajili ya sekta ya uvuvi. Waziri anataka kutuambia kwa majibu yake haya yupo happy kwamba Wizara yake imefanya vya kutosha kuwaondolea umaskini wananchi wa ukanda wa Pwani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Waziri anafahamu kwamba kutengeneza fiber boat moja ni karibu milioni 100 na kwamba bilioni mbili anazozisema ni sawasawa na boti kumi. Wizara iko happy kwa hali ya uvuvi ilivyo mbaya katika nchi yetu na wao wanatuambia wamefanya kitu?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  110  SESSION #  10
mp Answer From Hon.Ole-Nangoro, Benedict Ngalama
LIVESTOCK AND FISHERIES DEVELOPMENT
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI:

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikubaliane naye kwamba tofauti ni kubwa sana kati ya nchi alizozitaja na nchi yetu. Lakini tofauti haipo kwenye sekta ua uvuvi tu, ipo katika kila sekta na nchi zote alizozitaja ni middle income countries na sisi hatujafika huko japo lengo letu kwa mujibu wa dira yetu, (Development Vision 2025 ni kufika huko. Kwa hiyo nimhakikishie tu kwamba tofauti hiyo ipo kubwa lakini tunajipanga tuanze kuelekea kule maana tumetofautiana na nchi hizo katika mambo mengine mengi ya elimu, teknolojia, mitaji na kadhalika.

Swali la pili; nakubaliana na yeye kwamba kiasi cha fiber boats zinazotengenezwa kwa pesa hiyo ya mikopo ni ndogo lakini ni mwanzo na tukijipanga na kuelekea kule kwa uhakika ni lazima tujenge uwezo zaidi wa vifaa hivyo vya kuvulia na uwezo wa watu wetu wanaovua kimitaji na kiteknolojia. Kwa hiyo, sisemi kwamba hapa tulipo tunaridhika lakini hali halisi ni hiyo. Tutaendelea kuwaomba mwongeze Bajeti uwezo ujengwe zaidi, uzalishaji fanyike zaidi, maana tuna potential kubwa katika uvuvi kushinda mataifa aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge.