You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Kitandula, Dunstan Luka[CCM]

Mkinga Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
8 130 INFORMATION, CULTURE AND SPORTS Information 4 July 2012
Mheshimiwa Mwenyekiti namshukuru Naibu Waziri kwa majibu yake ya ufanisi, nina swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa pamoja na kuwepo kwa sheria hizi
zinazohusu usalama wa chakula, Consumer Protection
na usalama kwenye madawa, bado tunaendelea
kushuhudia matangazo mengi yanayopotosha Umma
na hivyo kuwaondolea haki ya kupata taarifa sahihi
watumiaji wa huduma hizi?

Je, Serikali haioni sasa kwamba ni vizuri ikaanzisha mfumo ambao utakuwa ni self regulating kwa kuanzisha chombo ambacho kitakuwa ni advertising standard council ambacho katika nchi 71 Ulimwenguni kimeweza kuleta mafanikio makubwa kuondokana na tatizo hili?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  130  SESSION #  8
mp Answer From Hon.Makalla, Amos Gabriel
INFORMATION, CULTURE AND SPORTS
NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA
MICHEZO:

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nilitaka
niseme kwamba Serikali inapokea ushauri wake na
tutaendelea kuufanyia kazi. Lakini nataka nisistize tu kwamba wamiliki wa vyombo vya habari na magazeti wazingatie sera, sheria na kanuni za uandishi wa habari. Hili ni pamoja pia na kuhakikisha kwamba vyombo hivi vinakuwa na waandishi wenye taaluma na uweledi wa tasnia ya utangazaji. Lakini pia kuhakikisha kwamba wanazingatia maadili na miiko ya utangazaji na uandishi wa Habari.