Parliament of Tanzania

Bunge la Bajeti

Mkutano wa Saba wa Bunge la Bajeti unaendela Mjini Dodoma na unatarajiwa kumalizika tarehe 30 Juni 2017.


Kabla ya kuendelea na Shughuli zingine, Kikao cha kwanza Mkutano huu wa saba kilianza kwa kushuhudia kiapo cha Uaminifu cha Mhe. Salma Rashid Kikwete ambaye ameteuliwa hivi karibuni na Rais kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kiapo cha Mhe Salma kilishuhudiwa pia na mume wake ambaye ni Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe Jakaya Mrisho Kikwete.


Aidha katika Mkutano huu, Bunge limefanya uchaguzi wa wabunge Tisa (9) wa Bunge la Nne la Afrika Mashariki (EALA). Uchaguzi huo ulifanyika baada wabunge walipo sasa kumaliza muda wao ambao utaisha mwezi Juni mwaka huu.Mkutano huu wa Saba wa Bunge utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kupitisha Bajeti ya Serikali pamoja na kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara zote kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 pamoja na Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18.


Kabla ya uwasilishwaji wa Bajeti ya Serikali, Bunge litajadili Hotuba ya hali ya Uchumi wa Taifa itakayowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango.

Vilevile katika Mkutano huu wa Bunge, jumla ya miswada mitatu inawasilishwa Bungeni ambayo ni:-

· Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha wa Mwaka 2017 (The Appropriation Bill, 2017).

· Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2017 (The Finance Bill, 2017)

· Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka, 2017 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill 2017.

·

Kwa upande wa Maswali, Katika Mkutano huu jumla ya maswali ya kawaida 515 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge wastani wa maswali 72 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa pia siku za Alhamisi.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's