Parliament of Tanzania

Kamati za kudumu za Bunge zaanza kukutana Jijini Dodoma


Vikao vya Kamati 14 za Kudumu za Bunge vitaanza Jumatatu tarehe 22 Oktoba na kuendelea hadi tarehe 04 Novemba 2018, Jijini Dodoma. Shughuli zote za Kamati katika kipindi hicho zimepangwa kwa kuzingatia Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016. Shughuli hizo ni kama ifuatavyo:-

(i) Uchambuzi wa Taarifa mbalimbali za Msajili wa Hazina kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma katika Mashirika na Taasisi mbalimbali Nchini.

(ii) Uchambuzi wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu za Mwaka 2016/2017

(iii) Uchambuzi wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Hesabu zilizokaguliwa za Serikali za Mitaa za Mwaka 2016/2017.

(iv) Uchambuzi wa Taarifa za utekelezaji wa majukumu ya Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali.

(v) Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa tarehe 10 Septemba, 2018 wakati wa Mkutano wa Kumi na Mbili wa Bunge.

Bofya hapa kupata ratiba zote za Shughuli za Kamati za Bunge

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's