Parliament of Tanzania

Mhe Spika awashukuru UNDP kwa ufadhili wa Mradi wa kuwajengea uwezo Wabunge (LSP)

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai amewashukuru Washirika wa Maendeleo kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNPD) kwa kufadhili Mradi wa Kuwajengea Uwezo Wabunge (LSP).

Mheshimiwa Spika alitoa shukrani hizo ofisini kwake Mjini Dodoma jana alipotembelewa na wageni kutoka Nchi za Jumuiya ya Nordic ambao ni wafadhili wa mradi huo.

Alisema asilimia 70 ya wabunge wa Bunge la 11 ni wapya na kwamba hawana uzoefu na shughuli za kibunge hivyo kupitia mradi huo wabunge hao wamekuwa wakipewa semina mbalimbali za kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ili waweze kutekeleza majukumu yao.

“Mradi wa LSP umesaidia sana kuwajengea uwezo wabunge wetu katika masuala mbalimbali hasa katika jukumu lao la kuisimamia Serikali na mchakato wa kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa bajeti ya Serikali,” alisema.

Alisema anatambua kwamba Mradi wa LSP unaingia awamu ya Pili na kwamba awamu hii itawasaidia wabunge hasa wale wapya pamoja na wafanyakazi wa Bunge ili waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi.

“Bado tunahitaji kuwajengea uwezo wabunge kuhusiana na masuala ya jinsia. Vilevile tunataka kuwajegea uwezo wafanyakazi wa Bunge katika masuala ya IT (Tekenlojia ya Habari) ili Bunge lifanye kazi katika mfumo wa E – Perliament (Bunge Mtandao).

Kwa upande wake Mkuu wa Msafara huo, Alvaro Rodriguez alisema ujumbe huo ulikuja kwa lengo la kuangalia maendeleo ya mradi huo pamoja na kuimarisha zaidi mahusiano katika mradi unaokuja.

Alisema wamependezwa na malengo ambayo Tanzania imejiwekea ya kufikisha idadi ya asilimia 50 ya wabunge wanawake katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mpango wa kulibadilisha Bunge katika Mfumo wa Bunge Mtandao (E Perliament).

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's