Parliament of Tanzania

Mkutano wa Kumi na Nne wa Bunge waanza Jijini Dodoma

Mkutano wa Kumi na Nne wa Bunge la Kumi na Moja umeanza leo Jumanne tarehe 29 Januari 2019 na unatarajiwa kumalizika tarehe 8 Febuari, 2019 Jijini Dodoma ambapo kikao cha kwanza cha Mkutano huu kilianza kwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Mhe. Abdallah Ally Mtolea kula kiapo cha Uaminifu.

Shughuli nyingine zinazotarajiwa kufanyika katika Mkutano huu ni pamoja na;

MASWALI

Katika Mkutano huu wa Kumi na Nne, wastani wa maswali 125 ya Kawaida yanatarajiwa kuulizwa na Wabunge. Aidha, wastani wa Maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa kwa siku za Alhamisi tarehe 31 Januari, na 7 Febuari, 2019.

MISWADA YA SERIKALI

Katika Mkutano huu, Bunge linatarajia kujadili na kupitisha Miswada Mitano (5) ya Sheria ambayo itasomwa kwa hatua ya Pili na ya Tatu. Miswada hiyo ni:-

• Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018 (The Political Parties (Amendments) Bill, 2018)

• Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wa Mwaka 2018 (The Tanzania Meteorological Authority Bill, 2018)

• Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini wa Mwaka 2018 (The Land Transport Regulatory Bill, 2018)

• Muswada wa Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa mazingira wa Mwaka 2018 (The Water Supply and Sanitation Bill, 2018).

• Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 4) wa Mwaka 2018 (The written Laws [Miscellaneous Amendments](No. 4) Bill, 2018)

TAARIFA ZA KAMATI

Katika Mkutano wa Kumi na Nne wa Bunge, Kamati za Kudumu za Bunge 15 zitawasilisha Taarifa za Mwaka za kazi za Kamati hizo kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 117(15) ya Kanuni za Bunge:-

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria;

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa; na

• Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Ratiba ya Mkutano wa Kumi na Nne wa Bunge

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's