Parliament of Tanzania

Mkutano wa Nane wa Bunge waanza Mjini Dodoma

Mkutano wa Nane wa la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza leo Jumanne tarehe 5 Septemba, 2017 na untarajiwa kumalizika tarehe 15 Septemba 2017 Mjini Dodoma.

Shughuli ya kwanza iliyofanyika katika kikao hiki cha kwanza ni ya Waheshimiwa Wabunge saba wa Chama cha Wananchi (CUF) walioteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi hivi karibuni kula kiapo cha Uaminifu. Wabunge hao wapya walioapishwa na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai ni pamoja na;

1 Mhe. Alfredina Apolinary Kahigi

2 Mhe. Kiaza Hussein Mayeye

3 Mhe. Nuru Awadhi Bafadhili

4 Mhe. Rukia Ahmed Kassim

5 Mhe. Shamsia Aziz Mtamba

6 Mhe. Sonia Jumaa Magogo

7 Mhe. Zainab Mndolwa Amir

Aidha, katika Mkutano huu wa Nane wa Bunge jumla ya Miswada mitatu inatarajiwa kusomwa kwa hatua zake zote. Miswada hiyo ni

a. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 3 wa Mwaka 2017 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3) Bill, 2017)

b. Muswada wa Sheria ya Reli wa Mwaka 2017 (The Railways Bill, 2017)

c. Muswada wa Sheria ya Madaktari, Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa Mwaka 2016 (The Medical, Dental and Allied Health Professionals Bill, 2016)

MAAZIMIO

Aidha, Katika Mkutano huu wa Bunge Maazimio matano yanatarajiwa kuridhiwa. Maazimio hayo ni:-

i) Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Afya ya Mimea, Usalama wa Wanyama na Chakula (The East African Community Protocol on Sanitary and Phytonisanitary (SPS) Measures).

ii) Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Amani na Usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (East African Community Protocol on Peace and Security.

iii) Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba ya kuanzisha Kamisheni ya Pamoja kati ya Tanzania na Malawi kuendeleza Bonde la Mto Songwe (Convection of Establishment of Joint Songwe River Basin Commission between Tanzania and Malawi).

iv) Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba (Intergovernmental Agreement – IGA) baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Uganda kuhusu Mradi wa Ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki. (East Africa Crude Oil Pipeline – EACOP) kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania).

v) Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Nyongeza ya Tisa ya Mwaka 2016 ya Katiba ya Umoja wa Posta Duniani.


TAARIFA YA KAMATI

Bunge pia linatarajia kupokea Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo kuhusu uchambuzi wa Sheria Ndogo.

MASWALI

Katika Mkutano huu jumla ya maswali ya kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge wastani wa maswali 16 ya papo kwa papokwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa pia siku za Alhamisi.

TAARIFA ZA KAMATI MAALUM

Katika Mkutano wa Saba wa Bunge la Kumi na Moja Mheshimiwa Spika aliunda Kamati Maalum mbili (2) kwa ajili ya kuchunguza biashara ya Madini aina ya Tanzanite na Almasi. Kamati hizo zilizopewa siku 30 zimekamilisha kazi hiyo na zitawasilisha taarifa zao kesho tarehe 6 Septemba 2017 katika hafla fupi itakayofanyika katika viwanja vya Bunge na kuhudhuriwa na viongozi wa Kitaifa. Katika tukio hilo, Mhe. Spika atapokea taarifa hizo na kuzikabidhi kwa Mhe. Waziri Mkuu. Matangazo ya hafla hiyo yatarushwa moja kwa moja katika Channel ya Bunge.

Ratiba yote ya Shughuliza Mkutano wa Nane wa Bunge inapatikana katika Tovuti hii ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz.


Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's