Parliament of Tanzania

Mkutano wa Pili wa Bunge la 12 waanza Jijini Dodoma

Mkutano wa Pili wa Bunge la Kumi na Mbili umeanza tarehe 2 Februari 2021 Jijini Dodoma na unatarajiwa kufanyika hadi tarehe 12 Februari, 2021.

Aidha, kabla ya kipindi cha Maswali na Majibu, Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai aliwatambulisha Waheshimiwa Wabunge ambao waliapishwa kwa nyakati tofauti nje ya Ukumbi wa Bunge.

Wabunge hao ni Wabunge watano walioteuliwa na Mhe. Rais, Wabunge wanne kutoka ACT Wazalendo na Wabunge 19 wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Pamoja na mambo mengine Shughuli zitakazofanyika katika Mkutano huu ni kama ifuatavyo:-

1. Maswali

Katika Mkutano huu wastani wa maswali 125 ya kawaida na Maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa na Wabunge kwa mujibu wa Kanuni ya 45 (1) na 44 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Juni, 2020.

2. Hotuba ya Rais

Kwa mujibu wa Kanuni ya 36 (3) ya Kanuni za Bunge, Toleo la Juni, 2020 Waheshimiwa Wabunge watapata fursa ya kujadili Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Ufunguzi Rasmi wa Bunge la Kumi na Mbili.

3. Kamati ya Mipango

Katika Mkutano huu, Bunge litakaa kama Kamati ya Mipango ili kujadili na kushauri kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2021/2022.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 113 (2) ya Kanuni za Bunge, Toleo la Juni, 2020, Bunge hukaa kama Kamati ya Mipango katika katika Mkutano wa Mwezi Oktoba – Novemba kila mwaka isipokuwa kwa Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya. Kwa kuwa Mkutano wa Novemba, 2020 ulikuwa wa Kwanza wa Bunge hili, hivyo Bunge litakaa kama Kamati ya Mipango katika Mkutano huu wa Pili.


Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament