Parliament of Tanzania

Spika Ndugai aahidi kudumishi ushirikiano na CPA-Afrika

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai ameahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na Umoja wa Mabunge wanachama Jumuiya ya Madola-Kanda ya Afrika (CPA Africa Region) ili kuimarisha umoja wa Afrika hususani katika kupigania maswala ya Kibunge.

Mhe. Ndugai aliyasema haya Jijini Dar es Salaam wakati akifunga Mkutano wa Kamati Tendaji ya Umoja wa Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Madola-Kanda ya Afrika uliofanyika Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa amekuwa Kiongozi ndani ya Umoja huo na ameshiriki kwa muda mrefu katika shughuli zake na hivyo anaelewa mchango wa CPA-Kanda ya Afrika katika kusaidia kusukuma mbele ajenda za Bara la Afrika katika Jumuiya ya Madola.

“Nipo pamoja nanyi na nimefanya kazi pamoja na Vingozi wengine katika Umoja huu kuanzia ngazi ya Tawi hadi Kanda ya Afrika katika kuzipeleka mbele ajenda za Bara la Afrika katika Jumuiya ya Madola,” alisema Mhe Ndugai.

Spika Ndugai aliongeza kuwa kwa kadri ambavyo Wabunge wapya wamekuwa wakichaguliwa ni vyema Wabunge hao wakaendelea kuelimishwa juu ya umuhimu wa Vyama vya Kibunge ikiwemo Umoja wa Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Madola ili waweze kusaidia katika kusukuma mbele ajenda za bara la Afrika katika Vyama hivyo.

“Ninawahakikishia pia ushiriki wa Wabunge kutoka Bunge la Tanzania katika shughuli mbalimbali za Umoja huu ikiwemo Mkutano ujao wa 62 wa Umoja wa Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola,” alisema Spika Ndugai.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati Tendaji wa CPA-Kanda ya Afrika Mhe Lindiwe Maseko alimshukuru Mhe Ndugai kwa ushirikiano ambao Bunge la Tanzania limeendelea kuonesha katika shughuli mbalimbali za CPA.

“Tunashukuru kwamba Bunge la Tanzania limeendelea kuwa mwanachama hai wa CPA-Kanda ya Afrika na nimatumaini yetu kuwa mtaendelea kudumisha moyo huo,” alisema Mhe Maseko.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's