Parliament of Tanzania

TANZIA

Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Y. Ndugai anasikitika kuwatangazia kuwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani( CCM), Zanzibar.Mhe. Hafidh Ali Tahir amefariki dunia saa 9 alfajiri ya kuamkia leo katika Hospitali ya General hapa Dodoma.

Marehemu alizaliwa Oktoba 30, 1953 Dimani Mjini Magharibi na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1972-1978) na amekuwa Mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.

Marehemu pia alikuwa mwamuzi wa FIFA na katika kipindi chote cha Ubunge wake Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir alikuwa Mchezaji mahiri wa mpira wa miguu na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Michezo ya Bunge.

Marehemu Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir ameacha Mke mmoja na Watoto Saba

Mheshimiwa Spika wa Bunge anaungana na Wabunge wote katika kuomboleza msiba huu.

“Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un”

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's