Parliament of Tanzania

TANZIA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Y. Ndugai (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Mhe. Dkt. Elly Marko Macha kilichotokea katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu.


Mipango ya Kusafirisha Mwili wa Marehemu kuja nchini ikiwa ni pamoja na taratibu za mazishi inaendelea kufanywa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Familia ya Marehemu.

Kufuatia Msiba huu. Mhe. Spika ameahirisha vikao vya kamati vilivyokuwa vinaendelea leo hadi kesho Jumamosi tarehe 1 Aprili, 2017.

Taarifa zaidi juu ya Msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kadri zitakavyopatikana.

“Mwenyezi

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.” AMINA

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's