Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi hii na mimi niweze kutoa maoni yangu katika mpango ulio mbele yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipata fursa kwenye Kamati yetu ya Bajeti kuongea na Serikali kuhusu Mpango huu na ninaomba nirejee tena kwa issues nilizozi-raise. Nilikuwa nasema ni ngumu kujua nchi yetu inasimamia uchumi gani na ina mipango gani kwa ujumla wake. Mfano, muhula wa Mheshimiwa Rais Mwinyi alisimamia soko huria na ni kipindi hiki ambacho mashirika mengi na viwanda vyetu vya Serikali vilifungwa. Alipokuja Mheshimiwa Mkapa alisimamia ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma na aliimarisha TRA pamoja na kuzingatia zaidi katika ulipaji wa madeni ya nchi. Kipindi cha Mheshimiwa Kikwete yeye alikuwa na kauli mbiu ya maisha bora kwa kila Mtanzania na alijikita zaidi katika ujenzi wa miundombinu. Muhula huu tulionao sasa Mheshimiwa Magufuli amesimamia uchumi wa viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu nilikuwa najiuliza, core business ya nchi hii ni nini? Mwanafunzi labda anapojifunza uchumi au jiografia ya nchi fulani uchumi wao ni wa nini? Tunatoa mawazo mbalimbali, Wajumbe wengi hapa wanaongelea kuhusu sekta nzima ya kilimo kwamba wananchi wengi wa nchi hii tumesimamia katika ufugaji, uvuvi na kilimo chenyewe au bidhaa za misitu, ndio majority ya wananchi wetu. Katika nchi yetu kila kipindi cha miaka kumi tuna lengo fulani, lakini taswira kubwa ya nchi ni nini? Umaskini upo pale pale na mikakati na mipango hii tunayojiwekea kila wakati huenda ikibadilika na mara nyingi haifikii hata nusu ya malengo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti,tukiangalia katika kitabu chetu cha Mpango kwa ajili ya mwaka huu wa fedha unaotaka kuja, vipaumbele vimewekwa katika maeneo nane. Kati ya hayo, saba ni kwenye sekta ya miundombinu na moja imeongelea kuhusu kusomesha kwa wingi wataalam kwenye fani ya ujuzi adimu, mfano uhandisi, urubani, udaktari bingwa na ufundi. Tunarudi kwenye swali nchi yetu inaenda kwa kutegemea nini? Tunarudi pale pale kwenye sekta ya kilimo. Sasa uko wapi huu mfungamanisho wa kile tunachokifanya na hii sera ya viwanda tuliyona sasa hivi? Uko wapi mfungamanisho wa hii sera ya viwanda na shughuli za elimu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ungetegemea kwamba kwa miaka hii mitano ya muhula huu mpya wa Mheshimiwa Rais Magufuli tunasema kuhusu viwanda, tungeona iko reflected kwenye sekta ya elimu, VETA zinafanya nini, vyuo vikuu vinafanya nini kwa ajili ya viwanda gani? Tungeona mfungamanisho wa sekta ya viwanda na shughuli za kilimo kwa ujumla wake. Pembejeo zikoje, tuna shida ya masoko, vifaa vya ukulima na vifaa ya uvuvi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mabunge yaliyopita kulikuwa na Kamati kuhusu Uvuvi wa Bahari Kuu na tulionyesha ni rasilimali ambayo iko tu hatujaifanyia investment yoyote. Tangu niingie Bunge hili nilikuwa naona kuna mipango inaongelea kuhusu bandari ya uvuvi ili kuijenga sekta ya uvuvi hususan katika bahari kuu, lakini haipo humu ndani, iko silent.(Makofi)
Mheshimiwa Menyekiti, sasa unajiuliza Serikali yetu inataka kusimamia nini? Kwa hiyo, inakuwa ni rahisi sisi kama Wajumbe wako kuweza kuchangia katika Mpango, lakini inakuwa ni kama Q&A, tunatoa mapendekezo majority ya hayo mapendekezo yanakita kwenye sekta ya kilimo, lakini majibu yanayokuja tutarudia pale pale kwenye miundombinu. Miundombinu kwa ajili ya nani na kwa ajili ya nini? Ni wakati gani unatakiwa u-invest katika miuondombinu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaongelea SGR inaenda kihatua hatua kwa fedha za ndani, inaishia Morogoro, itaishia hapa Dodoma and then what? Tunataka lane sita ya kutoka Dar es Salaam, mradi wa Chalinze - Dar es Salaam, ulikuwepo ni mzuri lakini umeishia katikati, tunataka nini? (Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.