Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

Hon. Dr. Immaculate Sware Semesi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi. Hoja yangu itajikita katika ukurasa wa 25 wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ambayo imeelezea kuhusu kusimamia miradi ya Shirika la Taifa (NHC).

Mheshimiwa Spika, kwa kifupi naungana na maoni ya Kamati kwamba National Housing Corporation imesitisha miradi yake ya ujenzi kwa maendeleo ilhali kwamba iko katika mikopo. Sasa mikopo hii inazidi kukusanya riba inakuwa ni hasara katika uchumi wa nchi. Kwa hiyo, naomba Serikali ijitathmini kwa upya ili kuwezesha shirika hili likaendeleza kazi yake.

Mheshimiwa Spika, suala la pili katika maoni ya Kamati, ukurasa wa 23 inaongelea tishio la kukauka kwa Mto Ruaha Mkuu. Sasa naomba nijikite zaidi katika kulichanganua hili.

Mheshimiwa Spika, mto huu wa Ruaha Mkuu, ni moja ya mito ambayo ni muhimu sana katika nchi yetu. Kwanza, inasaidia katika Sekta nzima ya Utalii ambayo ina-link na sekta nyingine za kiuchumi kwa ujumla wake. Katika hali ya sasa, Sekta ya Utalii ina-contribute 17% ya tunachokipata kama forest contribution takribani sawasawa na Dola bilioni 2.1 kwa mwaka. Kwa hiyo, ni sekta ambayo ikilelewa au ikiangaliwa kwa jicho la ziada inaweza ikatutoa katika hii hali ya umasikini na kwenda kwenye uchumi wa kati.

Mheshimiwa Spika, ni kwa sababu gani inaweza ikatutoa hapa tulipo? Sekta ya Utalii inagusa sekta nyingine mbalimbali. Ni mambo ya hoteli, mambo ya usafirishaji, mambo ya vyakula, mambo ya exchange rate, ina-influence hapo. Kwa hiyo, tuiangalie kwa jicho la ziada kwa sababu
mto huu Ruaha ndio unaobeba, kama Kamati walivyoeleza vizuri, ni roho ya Ruaha National Park. Sasa hii National Park ndiyo kubwa zaidi hapa nchini na inaongoza kwa idadi kubwa ya tembo na simba.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tusiiache tu juu juu jinsi ambavyo inaweza ikatutoa hapa tulipo ilhali sasa hivi huu Mto Ruaha unakaribia kufa. Kwa sababu Mto huu resource yake ni maji, maji haya sasa hivi yamepungua, sasa hivi kunakuwa kuna misimu mirefu ya kuwa hakuna maji. Karibu asilimia 77 ya chanzo cha Mto Ruaha kwenye Bonde la Ihefu na Usangu yameharibiwa. Kwa hiyo mto ule unaenda kufa.

Ya pili, inaenda kuua vyanzo vyetu vya umeme. Tanzania sasa hivi tunategemea takribani asilimia 70 ya umeme kutoka kwenye vyanzo vya maji, ikiwepo Kidatu, Mtera na sasa hivi tuna-propose mradi mpya wa Stiegler’s Gorge. Sasa nini kina-feed katika mabwawa makubwa ni huu Mto Ruaha Mkuu. Mtera karibia asilimia 56, Kidatu karibia asilimia 25 na kwenda Stiegler’s Gorge kinacho-contribute yale maji ni asilimia 25 ya huu mto ambao tayari unakufa.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa nataka pia tutafakari jinsi huu mto ambavyo unaenda kuharibu. Tumejikita kwenye Sekta ya Umeme tunategemea maji. Hivi karibuni tumepitisha mradi wa Stiegler’s Gorge ambao ulikuwa unaleta sintofahamu na nilisimama kwenye Bunge lililopita.

Mheshimiwa Spika, wenzetu wa Kenya jirani, asilimia 65 ya chanzo cha umeme wao ni kutoka kwenye jotoardhi (Geothermal) na sisi Tanzania tuna hiyo potential ya ku-top umeme wetu ambao tuna uhakika nao kutoka kwenye Geothermal. Nafikiri Mkoa wa Songwe au Mbeya wana uwezo huo. Tuna Rift Valley ambayo ni source ya hiyo Geothermal.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, investment ambayo tunaweza tukaiweka katika kutafuta umeme katika nchi hii ambao unaweza uka-boost sekta zote including utalii ni umeme wa uhakika. Kwa hali ilivyo sasa mtakumbuka kwa wale wahenga wenzangu, mwaka 2006 Mtera ilikauka. Tulikosa umeme kwa muda gani? Kwa hiyo, mabadiliko ya tabia nchi, uharibifu wa mazingira, mito yetu iko katika hali mbaya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Makamba atani-support kwenye hilo, yaani hapa naomba tusifanye ubishani wala tusifanye siasa. Nchi yetu ina hali mbaya katika Mito yetu, mmojawapo ni Mto Ruaha, Mto Ruaha ndiyo huo umebeba utalii, ndiyo umebeba sekta ambayo inaenda kukuza huo utalii including umeme.

Kwa hiyo, naomba tutafakari kwa upya. Hata kama sasa tumeamua kuendelea hivyo hivyo na tumelazimishia kufanya Stiegler’s Gorge, basi Wizara sekta husika iangalie jinsi ya kufufua hii mito iweze kutiririsha maji. Kama ikiwa too late, basi turudi nyuma tena tujitathmini. Kama kweli tunahitaji kutumia Stiegler’s Gorge kama chanzo chetu cha maji wakati kinaenda kuharibu utalii Ruaha, kinaenda kuharibu utalii Selous Game Reserve. Yaani kunakuwa na sintofahamu iliyopitiliza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba kwa hali ya pekee bila kuleta ushabiki, naomba tujitafakari kwa upya kama kweli tunataka kukuza sekta yetu ya utalii ambayo tuna uhakika katika kuimarisha uchumi wetu. Sisi wenyewe pia tujitafakari kama kweli ile engine ya kuleta maendelea ambayo ni umeme, basi tuangalie vyanzo vingine vya umeme tusitegemee Hydroelectric Power.

MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Basi kama hatutaki kutoka hapo, tuangalie means mbalimbali za kuweza kuimarisha upatikanaji wa maji katika mito yetu.

TAARIFA

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Spika, sielewi anani-support point yangu au alikuwa anakinzana na point yangu, sijaweza kupata conclusion. Naomba niichukulie positive kwamba tusitegemee chanzo kimoja cha umeme maji ambacho kina sintofahamu kubwa kwa sababu ya uharibifu wa mazingira, kwa sababu ya shughuli za kiuchumi. Nimetoa mfano kwamba chanzo cha maji cha huu Mto Ruaha ni katika Bonde la Ihefa, si ndiyo!

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, bonde hili limeharibiwa kwa asilimia 77 kwa sababu ya shughuli za kiuchumi, kilimo cha rice farming, kwa hiyo lazima tu-balance kwani ukiwa na diversity kubwa ya vyanzo vya umeme una uhakika na upatikanaji wa umeme, lakini tusitegemee 70 percent ya umeme wetu iwe chanzo chake ni maji, ambacho kina sintofahamu.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa niende kwenye Kamati ya Kilimo, Mifugo, Maji na Uvuvi, naomba nijikite katika ukurasa wa 64, nakubaliana na maoni ya Kamati ambayo tunasema lazima tufufue Shirika letu la Uvuvi Tanzania na nataka nisisitize kwamba sio tu kulifufua Shirika hili, bali tutengeneze na miundombinu rafiki ya kufanya hili shirika liweze kufanya kazi. Tununue meli za uvuvi, tujenge bandari ya uvuvi na iweze pia kuziwezesha zile taasisi ambazo zitakuwa zinategemeana na Shirika hili ikiwa ni pamoja na Tanzania Fisheries Research Institute. Tunaita ni Taasisi ya kufanya Research lakini Taasisi hii, haijawezeshwa kufanya kazi kwa kukosa rasilimali fedha, Wataalam tunao lakini hatuna rasilimali fedha katika taasisi hii ili kuweza kukuza sekta ya uvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa ….

SPIKA: Ahsante. Muda wako umekamilika.