Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

Hon. Riziki Saidi Lulida

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Spika, nikushukuru nami kwa kunipatia dakika chache ili nichangie katika hoja iliyoko mezani. Mwenyezi Mungu aliumba binadamu, aliumba ardhi, akaumba binadamu, wanyama, mito, bahari, wote hawa walikuwa wanategemeana. Nimefurahi kusikia baadhi ya mashamba yamerudishwa Serikalini ili kuwasaidia wananchi waendeleze kilimo, hii maaana yake nini? Niliwahi kuzungumza suala la baadhi ya mashamba ikiwepo mojawapo shamba la Kikwetu lilikaa kwa muda zaidi ya miaka 40 halilimwi, watu wanachukua mikopo benki, mashamba yale wakipewa wananchi, nina imani kuwa tutasaidia wananchi kupata ardhi na kuweza kulima.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna mashamba yalikuwepo Mtwara Kabisela, mashamba yale yalikuwa yamepigwa uzio, huruhusiwi kuingia, matokeo yake kinachoendelea ndani hujui. Huu ni unyonge ndani ya nchi yako, watu wana- monopolize ardhi lakini haitumiki.

Mheshimiwa Spika, nitazungumzia suala la uhifadhi Tanzania; Tanzania kuliwa na GN ambazo zilishawekwa kwa ajili ya uhifadhi kwa asilimia 25, lakini GN hizo zipo katika makaratasi, ukienda kwenye uhalisia tayari wananchi wameshavamia maeneo yale. Narudia tena naomba busara itumike na busara itumike kwa nini? Mle ndani ya zile hifadhi kuna wanyama, kuna korido za wanyama ambao wanatoka katika njia zao wanaingia ndani ya mbuga za wanyama. Kwa mfano, Mheshimiwa Spika mwaka 2005 alikuwa ni mjumbe mwenzangu katika Kamati ya Maliasili na Utalii, tulikwenda Ihefu kuwatoa wafugaji ambao walishaharibu mazingira na nchi ilikuwa gizani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo tunataka kuruhusu bila kufanya utafiti, hili zoezi litakuwa gumu na litaiingiza nchi katika mazingira magumu tena. Wanyama hawa waliandaliwa na Mwenyezi Mungu kupita katika korido zao, leo tumeona Ivory Coast hakuna wanyama sasa hivi, tunaona Burundi hawana wanyama, tunaona Rwanda hakuna wanyama, sasa Tanzania tumevimbiwa na wanyama wachache tunawaona hawa, lakini ni uchumi bora ambao utaifanya nchi iweze kupaa kama tutaweza kuweka mazingira bora. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wanyama tembo, simba, chui anatoka Niassa Mozambique, anavuka Mto Ruvuma anafika Mbarang’andu wananchi wameshavamia eneo, tembo wale wanauawa, hivyo mpaka kufika Selous karibu nusu ya tembo hawarudi tena Mozambique. Tembo anatoka Namtumbo anataka kuvuka kwenda Matambwe kwenda Mikumi tayari watu wanalipa miwa, mnyama hana mahali pa kwenda. Tembo anaingia Mikumi anataka kwenda Mkungunero tayari ameshazuiwa katika. Leo wanapotaka kutoa maamuzi ya kukurupuka, naomba tena tukae chini tuliangalie suala la wanyamapori ama la, nchi itaingia katika hali ngumu na wanyama watatoweka, utalii tunaojivuna nao utapotea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Tanzania tunajuana kwa makabila, kuna makabila wanapenda uhifadhi kama Mmasai, Mmasai hali nyamapori na hakati misitu. Kuna Wamakonde wanatunza misitu ndiyo maana misitu hiyo ilihifadhiwa mpaka leo, leo wafugaji wamekwenda Kusini, Lindi sasa hivi ni jangwa. Tunaona mikoa mingine imeshakuwa jangwa, je, hili zoezi litatusaidia au litatuwekea hali ngumu, nchi ni jangwa, ukiingia Dodoma yote ni jangwa, Singida jangwa, ukiingia Mkoa wa Arusha yote, Monduli jangwa, Shinyanga yote jangwa, tutafakari kabla hatujatoa maamuzi ambayo yataifanya nchi i-paralyze, kurudisha tena hii hali itakuwa ngumu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna baadhi ya wafugaji au makabila, kula nyama pori ni kama kazi yao, kama mtu wa Serengeti kazi yake anakimbizana kuingia ndani ya mbuga kula kimoro. (Makofi)