Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana kwa kunipa hizi dakika tano. Mara nyingi tumeambiwa kwamba upande huu hatusifu, nianze sasa kwa kutoa sifa zifuatazo. Kwanza, nimshukuru sana Mheshimiwa Mkuchika alikuja akatoa Semina nzuri ya Maadili ya Utumishi wa Umma ambapo vijana wengi pale Iringa waliifurahia. Sijui nani watakaorithi kuendelea na utaratibu ambao Mheshimiwa Mkuchika aliufanya maana wafanyakazi wengi waliufurahia. Hayo ni mambo mema ambayo tunapenda yatokee katika nchi kwa sababu ni mazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, nimshukuru sana Waziri wa Afya na Naibu wake pale ambapo Mkuu wetu wa Mkoa ali-demoralize spirit ya watendaji kazi katika Manispaa ya Iringa, alim-harass sana Daktari wetu ambaye ni Bingwa ambao tumewasomesha vizuri, lakini walihakikisha yale mambo wameyaweka calm yakaenda vizuri na Daktari anaendelea vizuri. Hilo niwashukuru sana ni mambo mema mnayoyafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la tatu ambalo napenda nishukuru tena katika Manispaa ya Iringa ni pale ambapo Mkuu wa Mkoa alivyofika tulikuwa na machinjio; Kamati ya LAAC walifika na waliona tuna machinjio nzuri sana, ilikwama kwa sehemu na wakaiona, wakatutia moyo. Ilipaswa iwe imeanzishwa miaka mitatu, minne iliyopita lakini kukawa na vikwazo vya kisiasa, wakatupa ushauri lakini kuna mambo mengi tulivyotaka kuanza kulikuwa na taabu sana, Mkuu wa Mkoa kajiapiza kwamba akiwa yeye Mkuu wa Mkoa hataruhusu hela yoyote ije. Niwashukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Jafo, jana Meya wangu wamesaini, Serikali imekubali ku-release shilingi bilioni 1 ambayo itasaidia kufanya hayo machinjio iweze kufanya kazi. Haya ni mambo mema ni lazima tupongeze na kama mwakilishi wa watu ni lazima niyapongeze. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niombe Wizara kama nilivyomsifu Mheshimiwa Mkuchika tufanye kazi kwa utaratibu na Maadili ya Umma kutokana na sheria inavyosema. Hawa Wakuu wa Mikoa wengine kwa kweli wanapagawa sana, hawamjali mtu yeyote. Naomba kama inawezekana kwa mujibu wa utaratibu Mheshimiwa Waziri Mkuu na Waziri wa TAMISEMI, tuendelee kusaidiana, muendelee kuwalea hawa vijana wenye mihemko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haya mambo ya kuwekaweka watu ndani ina-demoralize utendaji wa kazi. Lile wiki alilokuja Ndugu Hapi Iringa Mjini wafanyakazi wote walikuwa down lakini kwa sababu na mimi nilikuwa na misuli ya kutosha, nilihakikisha napandisha ile morale ya utendaji kazi ili turudi kwenye utendaji kazi na kufuata masharti ya utumishi wa umma. Watendaji hawa wateule, Wakuu wa Wilaya, wanatumia vibaya madaraka yao. Hili ni Taifa la wote, tunatakiwa tufuate taratibu, kanuni na miongozo.

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, nilishamuona Mheshimiwa Waziri Mkuu, kuna Bwana mmoja alikuwa ni Mkurugenzi wetu aliondolewa Iringa kwa siasa, Iringa kuna siasa nyingi sana. Hata hivyo, tunafanya kazi kama nilivyosema tunaongoza kwa kukusanya mapato, tunaongoza kwa usafi na tunapata hati safi mfululizo. Misingi hii aliyetuwekea ni Bwana mmoja anaitwa Ahmed Sawa, mmeenda kum-dump sijui wapi huko Mkoani kwa kosa ambalo hana. Watumishi kama hawa hata asiporudi Iringa mtafutieni sehemu nyingine afanye kazi kwa sababu ni mchapakazi, ni mbunifu, haya mambo tunayoyapata leo ni kwa sababu ya utendaji wake mzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana, nimeona nitoe haya kwa sababu mimi ni mwakilishi wa watu na watu wengine hawayajui, watu wengine wanaonewa sana katika nchi hii kwa makosa ambayo hawajayafanya.

Mheshimiwa Spika, Nikushukuru sana.

T A A R I F A

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, nilitaka nipokee tu taarifa yake kwamba haya matatizo ya Wakuu wa Wilaya na Mikoa yako maeneo mengi. Kwa hiyo, Waziri Mkuu na Serikali mnasikia, sisi Wabunge tunataka tufanye kazi na wateule wa Rais kwa kupendana siyo kwa kushindana. Mtu anakuja ametukuta pale tunafanya kazi, haya mambo hayakuzuka kuna watu walifanya kazi.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)