Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kongwa
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JOB Y. NDUGAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Halmashauri za Miji Midogo; za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji kuna kanuni za uendeshaji ambazo zinapelekea kuwepo kwa vikao vingi sana kwa mwaka. Kamati ni nyingi mno na malipo ni ya mara kwa mara kwa kila Diwani na zaidi kwa Wenyeviti/Mameya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia wawakilishi hawa ni wengi sana, hivyo ipo haja ya kuangalia kama Kongwa unahitaji Madiwani 30 waliopo plus miji miwili midogo ya Kongwa na Kibaigwa ina Wenyeviti wa Mitaa 30 pia. Kwa Mkoa wa Dodoma kwa mfano, Halmashauri ni Kondoa Vijijini; Kondoa Mji; Chemba; Bahi; Dodoma Jiji; Chamwino; Mpwapwa; Kongwa; Mpwapwa Mji Mdogo; Kibaigwa Mji Mdogo; Kongwa Mji Mdogo, jumla ni 10. Kama wawakilishi ni 30 tu kwa kila Halmashauri kwa kikao kimoja cha Madiwani hao 30 x 10 = 300 na kila mmoja hulipwa shilingi 240,000 kwa kikao, jumla ya kikao kimoja tu ni shilingi 72,000,000 (hii ni minimum). Wajumbe wa Bodi za Afya kila Wilaya ni 100 x 240,000 = 24,000,000. Madiwani wajumbe wa Kamati za Fedha na Mipango wanakaa mara 12 kwa mwaka, kwa vikao vya Kamati hiyo tu na hao hao ni wajumbe wa Kamati nyingine kwa hiyo wanalipwa each siyo chini ya mara ishirini kwa mwaka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja hapa ni kwamba vikao vipunguzwe kwa idadi na malipo yapungue. Patolewe mwongozo maana malipo haya ni kwa fedha za ndani za Halmashauri. Kipaumbele kinakuwa ni vikao vya Madiwani, fedha za maendeleo zinakosekana.