Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

Hon. Saada Salum Mkuya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipatia nafasi hii na naunga mkono hoja na nazipongeza Serikali zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuona kuna nia ya dhati kabisa ya kutatua changamoto za Muungano. Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri tunawapongeza pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa ni dakika tano, itabidi niende haraka haraka. Katika kitabu cha Mheshimiwa Waziri, ukurasa wa 14 ameelezea kuhusiana changamoto ya ongezeko na gharama za umeme ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imehakikisha kwamba changamoto hii inaondoka na tunaipongeza sana kwa hilo. Hata hivyo, changamoto hii ya VAT si kwamba inakwenda moja kwa moja kuondoa gharama za umeme kwa mwananchi wa kawaida wa Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba Mheshimiwa ukiwa mwenye dhamana ya kuratibu masuala ya Muungano, Wizara ya Nishati ihakikishe kwamba yule Consultant ambaye amepewa kazi ya kuangalia gharama za umeme anamaliza kazi hii mapema zaidi ili wananchi sasa waweze kunufaika kutokana na kupungua kwa gharama hizo. Hii VAT imeondoka lakini haijaondoa hizo gharama kama vile ambavyo tulitarajia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, Mheshimiwa Waziri amejikita zaidi sasa kuendelea kutoa elimu. Mchangiaji aliyemaliza kuongea Mheshimiwa Genzabuke amesisitiza jinsi gani Wizara iangalie hii elimu inapelekwa katika shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu. Naamini Mheshimiwa Waziri wakati hilo linaendelea mimi nadhani elimu kuhusu Muungano ianzie humu ndani katika Bunge letu Tukufu kwa sababu bado tunaona hata baadhi ya Wabunge ile concept ya Muungano haijatuingia sawasawa. Ndiyo maana hata baadhi tu ya kauli zinaweza zikawa zinatoka ambazo unahisi kwamba huyu mtu bado hajafahamu hasa nini maana ya Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo hata katika ngazi ya watendaji linatokea. Changamoto zinazoonekana ni kwa sababu ya issue za Muungano hazijawa mainstreamed. Kama tumeweza ku-mainstream issue za HIV, gender na mazingira, Muungano ni issue ambayo inatakiwa kuwa mainstreamed, wether iko kwenye eneo ambalo taasisi zetu zinafanya kazi kwenye Muungano au katika taasisi ambazo siyo za Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaloliona sasa hivi Mheshimiwa Waziri anayeshughulika na Muungano yeye ndiye anakuwa responsible kuangalia masuala ya Muungano lakini Wizara ambazo tunaziona tu kikawaida kwamba siyo Wizara za Muungano lakini moja kwa moja lolote linalofanyika katika Wizara zile linaathiri upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo, Muungano huu siyo Muungano ambao anausimamia Mheshimiwa January Makamba ni Muungano ambao sote tunakiwa tusimamie katika maeneo yetu tunayofanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kumekuwa na utaratibu Mawaziri ambao wanachaguliwa katika Taasisi za Muungano mara moja wanakwenda Zanzibar, wanamwona Mheshimiwa Rais na viongozi wengine lakini I do hope hilo haliishii kwenye kwenda kumuona Mheshimiwa Rais, linatakiwa liwe katika kazi zetu za kila siku. Bahati mbaya wale ambao wameji-term kwamba Wizara zao siyo za Muungano hatuwaoni kwenda Zanzibar labda siku ya Sherehe za Mapinduzi, tunaomba sana hii nchi yetu ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ukurasa wa 16 wa hotuba ya Mheshimiwa Waziri ameeleza mambo mengi yaliyopatikana ikiwa ni pamoja na gawio la Benki Kuu. Tunashukuru sana Benki Kuu ya Tanzania imeendelea kutoa gawio. Hii ni taasisi ya Muungano na inasimamia fedha za Serikali lakini bado Mheshimiwa Waziri kuna taasisi za Muungano na gawio halitolewi. Kuna taasisi ambazo zina operate katika Muungano lakini hatuoni gawio kwenda Zanzibar. Kwa mfano, Mashirika yetu kama TCRA, AICC, NIC, TTCL, bado gawio haliendi Zanzibar. Hizi ni taasisi za Muungano na inatakiwa gawio linatolewa kwa Serikali ya Jamhuri na Zanzibar ipate.

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango mzuri.

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja. (Makofi)