Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpwapwa
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza samahani sana nilipata dharura kidogo, kwanza nikushukuru sana kwa kunipa nafasi ili nichangie hoja hii ya Wizara ya Ujenzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili nimshukuru Waziri, Naibu Waziri, Watendaji wote wa Wizara hii kwa kazi zuri wanayofanya, na tatu nitazungumzia mambo mawili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza barabara ya Kongwa, Mpwapwa. Kwa kweli naishukuru sana Serikali, imesikia kilio changu imesikia kilio cha wananchi wa Mpwapwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, na leo hapa pasingetosha kwa kweli, lakini nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri, Mungu akubariki sana umenikumbuka. Pamoja na kwamba umenipa fedha kidogo sana, lakini nisiposhukuru hiki kidogo, hata hicho kikubwa nisingeshukuru. Kwa hiyo, nakushukuru sana, sana na naomba hiyo barabara ianze mapema ili wananchi wa Mpwapwa waone kwamba Mbunge wao kweli anashughulikia suala hili la bararaba. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu barabara ni siasa kwa sisi Wabunge, kama umeahidi halafu haitengenezwi, kwa kweli unapata matatizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nishukuru sana daraja la Godegode, hili daraja lilisombwa na maji mwaka huu mwezi wa tatu, kwa kweli nashukuru sana, pamoja na kwamba ilikuwa ni dharura lakini Mheshimiwa Waziri nilikuomba. Kwa sababu daraja hili ndiyo kiungo kikubwa cha Jimbo la Kibakwe na Jimbo la Mpwapwa, na kule upande wa Kibakwe kuna Kata saba, sasa zile Kata saba walikuwa wanashidwa kuvuka pale maji yakijaa. Kwa hiyo, wanazunguka kwenda Kibakwe ndiyo waje Makao Makuu ya Wilaya ambayo ni zaidi ya km 55 na nauli ni kubwa sasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nikushukuru sana, sana Mheshimiwa Waziri umesikia kilio cha wananchi wa Mpwapwa na umenitengea fedha daraja la Godegode nina hakika kabisa daraja hili litajengwa kwa wakati muafaka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo nakushukuru sana, nakushukuru na Mheshimiwa Waziri, ahsante sana. (Makofi)