Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na kuhusu mipaka, Jeshi limekuwa linapiga na kuvunja na kubomoa nyumba za wananchi, kuchukua sheria mkononi kwa Jeshi siyo kitu sahihi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, fidia za wananchi kwa maeneo yao ina suasua kabisa na ikibidi kama ikishindikana warudishiwe maeneo yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viwanda Jeshini, kuingia uchumi wa viwanda ni vyema tukawekeza katika viwanda vilivyoanza vya Jeshini kwani ni nguvu kazi iliyo tayari na ya uhakika lakini ukosefu wa fedha na kuwarudisha nyuma vifaa chakavu vinakwamisha ufanisi wao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ulinzi wa mipaka, Jeshi lipatiwe vifaa na pesa zaidi ili kuhakikisha mipaka yetu inakuwa salama kama uwepo wa boti za doria na helkopta za ulinzi, ujenzi wa madaraja ya kupitisha vifaa vizito nyakati za dharura ni muhimu sana.