Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie hotuba hii sehemu mbili; kwanza kwa kuwa vita vya Kagera historia yake haijawekwa vizuri ili vizazi vijavyo viweze kujua jinsi Jeshi letu la Ulinzi lilivyopigania nchi hii na kumwaga damu yao ili kutetea nchi yetu kutoka kwa Nduli Idd Amin, naomba kushauri kwamba historia ya vita hivi iandikwe na kuwekwa kwenye nyumba zetu za makumbusho na pia kwenye library za vyuo vyote vya elimu ya juu. Nakumbuka kazi hii ya uandishi iliashaanza na Mwenyekiti wake akiwa Spika Mstaafu, Pius Msekwa na Katibu wake alikuwa Luteni Kanali Livingstone Kaboyoka kwa vile hawa wote wawili wako bado hai ningeshauri mawasiliano yafanyike ili wasaidie kutoa taarifa muhimu ya vita hivi vya Kagera.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kwa kuwa TARURA inafanyakazi za matengenezo ya barabara mijini na vijijini, ningeshauri Jeshi la Kujenga Taifa lisaidie kuunda vikosi vya vijana hasa vijijini wakiwapa mafunzo ya ukakamavu na kuwasaidia wapate mafunzo ya kutengeneza barabara hasa vijijini ili badala ya kutoa pesa nyingi kwa wakandarasi ambao wakiondoka wanaacha barabara zikiharibika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, JKT ingeweza kufanyakazi na TARURA na kuunda Road Building Brigades ambao wanatokana na maeneo husika. Hizi brigades zingeweza kupatiwa basic equipments kama sururu, majembe, mapanga, mabeleshi na wheelbarrows ili kila mara wakarabati maeneo wanamoishi. Malipo yao yanatokana na michango ya wananchi na magari/pikipiki zinazotumia barabara hizo. Tuna mifano Tanzania ambapo enzi za ukoloni kulikuwa na vituo vya matengenezo ya barabara kila maeneo ya barabara. Kambi hizo zilikuwa zinajulikana kama PWD. Ahsante