Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia hoja hii katika suala la mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa vijana kwa mwaka 2018/2019 jumla ya vijana 19,895 wa mujibu wa sheria walipatiwa mafunzo kwenye kambi mbalimbali. Aidha vijana 21,966 wamepata mafunzo kwa kujitolea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vijana hawa wakimaliza mafunzo hawapati ajira na huku wamepata mafunzo hata ya kivita. Ningeomba Serikali iweze kuona athari za vijana hawa waliofundishwa kutumia silaha kubaki mitaani bila kazi ya kufanya. Ninashauri Serikali hata kama haiajiri waweke utaratibu au kuanzishwe programu wakishirikiana na VETA ili wawatumie vijana hawa kupata kozi anuai ambazo zitawasaidia kujiajiri na kuweza kukuza uchumi binafsi na wa Taifa, kwa mfano yanaweza kuwepa mashamba na wakapewa mitaji ya kuzalisha malighafi zinazoweza kutumiwa katika viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu nyongeza ya mishahara kwa wanajeshi, ninaiomba Serikali iwape nyongeza za mishahara wanajeshi kama kada nyingine zinavyotakiwa kwani hawajapata nyongeza zao tangu Serikali hii ya Awamu ya Tano imeingia madarakani. Tuwape kipaumbele kwa maslahi yao kwa kuwa kada hii imejitoa kwa gharama ya uhai wao katika kulinda mipaka ya nchi yetu ili iwe salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.