Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi. Mheshimiwa Mpango, wakati anatuletea Mpango wa Miaka Mitano mara tu baada ya Serikali kuingia madarakani, mojawapo ya mambo ambayo Serikali ilikuwa imetutangazia na kutuahidi kwamba itayafanya ni pamoja na masuala ya demokrasia na utawala bora ambayo yanapatikana katika ukurasa wa 111 katika kitabu hiki cha Mpango wa Miaka Mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mojawapo ya mambo ambayo aliyasema alisema kuhakikisha usawa wa kiuchumi, demokrasia na uvumilivu wa kisiasa katika jamii. Ukomavu wa demokrasia na ushiriki wa wananchi utazidi kuimarishwa kupitia, akaelekeza mambo gani yatapitia jinsi gani itakavyoimarishwa. Mojawapo alisema kuwekeza zaidi katika kuboresha mfumo wa uchaguzi na kufanya kuwa wa kisasa zaidi pamoja na kuzidi kupanua uhuru wa kujieleza, uwazi, upatikanaji wa habari; kuna mambo mengi sana alizungumza katika mpango wa miaka mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunapozungumza tunakwenda kumaliza kipindi chetu kama Wabunge, Madiwani na kama Mheshimiwa Rais, lakini haya mambo yote ambayo Mheshimiwa Mpango alikuwa ameahidi katika mpango, Serikali ilituhakikishia kwamba itaimarisha demokrasia tukianza moja baada ya jingine katika kipindi cha miaka mitano, kila kitu hapa kimedorora. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna uwazi wa vyombo vya habari, hakuna mfumo mzuri wa uchaguzi, hakuna mfumo wa kidemokrasia. Mara tu tulipoingia Bungeni hapa, kitu cha kwanza tulizuiwa mikutano, tukazuiwa Bunge live. nataka nimuulize Mheshimiwa Mpango huko ndio kuimarisha ambako alikuwa anatuambia wakati akituambia miaka mitano? Kwa sababu wamezuia Bunge Live, wamezuia mikutano wakasema Wabunge sehemu tunazotoka tutaruhusiwa kufanya mikutano na yenyewe wamezuia. Kibaya zaidi walisema wataimarisha chaguzi na hiki tunachokiona sasa katika nchi yetu ya Tanzania ambacho hakijawahi kutokea ni ishara tosha kwamba Serikali yenu haina mpango wa kuimarisha demokrasia na chaguzi huru katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwa bahati mbaya Mheshimiwa Jaffo hayupo hapa, kinachofanyika sasa hivi kwenye Serikali za Mitaa kimsingi Chama cha Mapinduzi wanakunywa sumu. You are just drinking poison, inawezekana isiwaue leo lakini itawaua kidogo kidogo. Hamuwezi kusimama hapa mka-claim kwamba ninyi ni ma-champion and you don’t want to compete; victory inatokana na ushindani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanajiitaje washindi na hawataki kushindana? Katiba yetu inasema kila baada ya miaka mitano tutapambana uwanjani na viongozi bora wanapatikana baada ya ku-compete, hawataki competition, huo ni utawala bora wa aina gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tunapozungumza, Wenyeviti wa Mitaa wote karibu nchi nzima wamefunga ofisi wamekimbia, hawataki kupokea mapingamizi, watendaji wote wamekimbia kwenye ofisi za umma, tunasema tunataka tuzungumzie utawala bora, hawapo wanakimbia... (Makofi)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Waitara.

T A A R I F A

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpe taarifa mchangiaji kwamba hili jambo limezungumzwa jana na leo. Mheshimiwa Spika jana alitoa maelekezo, leo wewe umetoa maelekezo na hapa tunapozungumza Mheshimiwa Waziri hayupo hapa lakini amekwenda Singida akakuta mambo sio kama walivyozungumza humu ndani, ameenda Manyara; tumetuma maafisa wetu wamekwenda kule Moshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nampa taarifa kwamba Mheshimiwa Msigwa tunayo kuanzia jana tarehe 5 na tarehe 6 ya mapingamizi, tunayo tarehe 6, 7 mpaka 9 ya Kamati ya Rufaa; maelekezo yaliyotolewa na Serikali ni kwamba kuna mtu amelalamika kama inavyozungumzwa waandike barua za malalamiko na malalamiko yatafanyiwa kazi, tunao muda mpaka tarehe 9. Kwa hiyo, usianue kwanza matanga kabla msiba haujaisha. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa unaipokea taarifa hiyo?

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii taarifa siipokei, inaonekana Mheshimiwa Waziri anataka kupotosha na hana information. Mimi kwenye Jimbo langu nina mitaa 192, wameenguliwa watu 185, sasa hivi wapo kwenye Ofisi za Kata zote zimefungwa; what are you talking about? Halafu mnataka kusema mnashinda, mnashindaje? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe mfano, wakati wa segregation kule Marekani Malcom X anatoa hotuba moja naomba ukaisikilize, kulikuwa kuna field negro na house negro. Humu ndani inawezekana wengine ni house negro hawajui tunacho-feel sisi ambao ni field negro kwenye field. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hamjui madhira tunayoyapata, kufanya siasa katika nchi hii imekuwa ni criminal, unahesabiwa kama ni mhalifu kufanya siasa ya nchi hii wakati Katiba inanipa mamlaka/uhuru wa kujieleza (freedom of expression). Ninyi mmekuwa ni house negro kwa sababu ni beneficiary wa mambo haya ndio maana hamuwezi kuyaona. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kuongea na wapiga kura wangu kwenye Jimbo langu na Wabunge wengi wenzangu wa upinzani ni uhalifu katika nchi hii. Tunaambiwa sisi lazima tuombe ridhaa ya kufanya mikutano, wengi wenu ninyi huwa mnaenda kufanya mikutano huko wala hamuulizwi na mtu yeyote. Kwa hiyo, tunaongea mambo ambayo tuna-feel.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nchi hii mnasema tushindane, Katiba inataka kila baada ya miaka mitano tushindane na nyie mnasema chama chenu kimeimarishwa; miaka minne hatujaongea, hatujafanya mkutano, Wenyeviti wa vyama vyetu hawajasafiri, mmesafiri ninyi peke yetu. Television mmezishika nyinyi peke yenu, unasema utawala bora; huo ndio utawala bora mnaotuambia hapa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, television, radio, mikutano ninyi, tunakuja kwenye mikutano seven days, you are running away, halafu mnakuja hapa mnasema tunatengeneza demokrasia, what kind of democracy is this? Mkifika uchaguzi mnakimbia mnasema kuna democracy, what democracy is this?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapokuja hapa kama tunataka tutengeneze nchi yetu tukubaliane kama tumeamua kufuta mfumo wa vyama vingi its well and good, mpo wengi, leteni Muswada wa Sheria hapa kwamba tumefuta mfumo wa vyama vingi tutabanana hukohuko si itakuwa ni sheria, tutabanana hukohuko kwenye majimbo yenu maana yake itakuwa ni sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katiba ya nchi yetu inatupa uhuru kwamba, mtu ana mawazo tofauti na mwingine wala hatugombani, wewe una mawazo yako na mimi nina mawazo yangu, tunashindana kwa hoja, baadaye tunaenda kwa wananchi, huo uhuru uko wapi katika maelezo ya Mheshimiwa Mpango aliyoandika hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye kitabu hicho hicho Mheshimiwa Waziri amesema kuhikisha kuwepo kwa mgawanyo wa madaraka na ufasaha wa mipaka baina ya mihimili mitatu ya Serikali kwa kuimarisha uwezo wa taasisi na rasilimali watu kwa kila mmoja kuwezesha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, democracy ilivyoanza, separation inahitaji balance, tunahitaji ku-balance, mhimili unaojitegemea wenye mamlaka na nguvu. Tunapozungumza, nimezungumza hapa leo Bunge Live lilizimwa, huu ni mkutano wa wananchi wa Tanzania, tunakuja kutunga/ tunapoingia Bungeni hapa tunapanga bajeti ya wananchi milioni 50 waliotutuma tuje tuwatenge hela zao katika bajeti hii, tunazungumzia kuhusu afya zao, kilimo, shule na afya zao, leo tunapozungumza Wabunge tuliotumwa tunakuja hapa tupo gizani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu Kenya ambapo Mheshimiwa Spika alikwenda, wao mpaka kamati zipo live. Tunazungumza separation of powers, nguvu ya mhimili wa Bunge, hawa tunaowasemea mimi sijaja peke yangu na kila mmoja hajaja peke yake, anawawakilisha watu wake. Tumekuja hapa ili wananchi wale waliotutuma wasikilize tunachosema, tunafanya gizani; hiyo ndio separation of power?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanasiasa tunashinda mahakamani kwa kosa la kufanya siasa, sisi sio wezi, hatujavunja nyumba. Ninyi Serikali ya Chama cha Mapinduzi mnapata wapi legitimacy ya kusema watu wasiwe wezi kama nyie wenyewe mnaiba kura, where do you get that? Kama nyie wenyewe mna-rob kura mnapata wapi kwamba watu wasiibe mitihani, mnawaambia watoto wasiibe mitihani kama ninyi wenyewe hizi kura mnanyang’anya kwa nguvu, mnapata wapi kwamba watoto wasiibe mitihani? (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utaratibu.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, where do you get that, where do you get that power?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU ENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utaratibu.

MBUNGE FULANI: Wanatengeneza hao.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, mnapata wapi hiyo nguvu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa. Mheshimiwa Jenista Mhagama, Utaratibu Kanuni.

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nitumie Kanuni ya 68 lakini naomba niende 68(1) lakini niende Kanuni ya 64(1) Kanuni ndogo ya
(a) hiyo inakataza kabisa ndani ya Bunge mtu kutokutoa taarifa ambazo hazina ukweli lakini nitakwenda mpaka Kanuni ya 65. Naomba Mheshimiwa Mbunge kwa kweli asiendelee kulipotosha Bunge kwamba uwepo wetu sisi hapa ndani na uwepo wa Serikali yetu unatokana na vitendo vya wizi wa kura na ndivyo vinavyotufanya tuendelee kuwepo madarakani.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuhuma hii, ni tuhuma kubwa na ni tuhuma ambayo sisi tunaojua Sheria na taratibu ushindi wa mgombea yoyote unatawaliwa na Sheria tulizonazo, Sheria za uchaguzi Katiba ya Nchi yetu na hapa ndani ya Bunge tunatawaliwa na Kanuni katika kuyaeleza hayo. Mgombea yoyote ambaye hajashinda ana uhuru wa kwenda Mahakamani na kwenda kueleza Mahakamani na kule Mahakamani wanaweza wakatoa nafasi ya mgombea yoyote kuthibitisha ama kuweka wazi kile kinachomkera. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, si kweli na nadhani anataka kutudhalilisha anapotutuhumu sisi wote, Serikali nzima, Wawakilishi wote wa Wananchi na hasa kupitia Chama cha Mapinduzi kwamba uwepo wetu hapa ni uwepo ambao si halali jambo hili si sahihi na anavunja Kanuni za Bunge. Kwa hiyo, tunamuomba sana Mheshimiwa Msigwa ama afute kauli hizi ama ajielekeze katika mjadala bila ya kuwa na tuhuma ambazo si za sahihi na hazina ukweli kwa mujibu wa Sheria tulizonazo kwa mujibu wa Kanuni na kwa mujibu wa Katiba.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge alikuwa akichangia Mheshimiwa Msigwa, ametoa maelezo marefu ambayo Mheshimiwa Waziri wa Nchi amesimama kuhusu utaratibu akataja Kanuni ya 68 na akataja Kanuni iliyokuwa ikivunjwa na Mheshimiwa Msigwa Kanuni ya 64(1)(a) ambayo Kanuni ya 64 kwa ujumla wake inazungumzia mambo yasiyoruhusiwa Bungeni na (1)(a) inazungumzia kutokutoa ndani ya Bunge taarifa ambazo hazina ukweli.

Mheshimiwa Msigwa kwa muktadha wa Kanuni zetu ukisoma hii kanuni ya 64 ukiizungumzia taarifa ambazo hazina ukweli itatupeleka kwenye Kanuni ya 63 inayozuia kusema uwongo Bungeni. Sasa kwa muktadha wa Kanuni hizo hizo zinataka hizo taarifa kama hazina uwezo wa kuthibitishwa basi Mbunge apewe fursa ya kufuta hayo maneno yake ili aendelee kuchangia. Kwa hiyo, na wewe nitakupa hiyo fursa ya kufuta hayo maneno yako halafu tutaangalia utaratibu mwingine kama utakubali kufuta, utakuwa umefuta kama hukukubali maana yake nitasimama tena.

Mheshimiwa Msigwa!

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimezungumza suala hilo ukienda Ndarambo kule kwenye Jimbo la Silinde kura ziliibiwa kabisa mpaka tukaenda…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa, hapo unataka kueleza maelezo mengine, umepewa fursa ya kufuta kauli uliyokuwa ukizungumza, kama hukubali kufuta hiyo kauli uliyokuwa unasema, wewe sema ili nitoe maamuzi, umepewa fursa ya kufuta kauli uliyokuwa ukizungumza kama hukubali kufuta unao ushahidi, wewe utasema, mimi nitaendelea na utaratibu wetu wa Kikanuni. (Kicheko)

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ushahidi wa kuibiwa kura tunao, ninao.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, Waheshimiwa Wabunge kwa mujibu wa hizi Kanuni zetu na mambo ambayo tunaweza kuzungumza humu ndani na sasa tunaelekea kukamilisha hili Bunge letu nataka kuamini kila mtu anaelewa Kanuni zetu matakwa yake ni yapi?

Kwa kuwa Mheshimiwa Msigwa unao ushahidi wa kuibiwa kura, na kwa kuwa huo ushahidi mimi hata ungeniletea hapa sina uwezo wa kujua kama ni wa kweli ama siyo utaenda kwenye Kamati ya Haki na Maadili ili ukathibishe kule hiki ulichokisema hapa. Kwa hiyo, kwa mchango wako wa sasa hayo maneno ya kuibiwa hutarudia mpaka utakapoenda kuthibitisha kule ile Kamati italeta taarifa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa.

MWENYEKITI: Nadhani tumeelewana vizuri, maneno ya kuhusu kuibiwa kura utaenda uthibitishe kule kwenye Kamati.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachosema tunapata wapi legitimacy kama sisi wenyewe hatuwezi kuishi yale tunayoyasema, Mheshimiwa Mpango kwenye Mpango wako.

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Taarifa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, democracy…

MHE. DKT. GODWIN O MOLLEL: Taarifa …

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Democracy ni kitu cha msingi ambacho…

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Taarifa …

MBUNGE FULANI: Taarifa ya nini?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa kuna taarifa. Mheshimiwa Dkt. Mollel.

T A A R I F A

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, kiongozi mwenzangu hapa anajaribu kuzungumzia legitimacy ya kuzungumza mambo ya kiadilifu na kufanya mambo ya kiadilifu. Lakini yeye kwenye Kambi yake, kwa maana ya Chama cha Chadema Wabunge wote sasa hizi wamegoma kuchangia chama kwa sababu ya Mwenyekiti wao kuiba milioni mia sita akiwa yeye ni mbeba mkoba, akiwa yeye ni mmoja wapo wa wabeba mkoba kwenye wizi huo na hata ruzuku haionekani na siasa ndani ya chama chake, ndani ya chama chake haiwezekani kwa sababu hakuna resources na watu wote wamegoma kuchangia na kusaidia chama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa anasema hata huo wizi alitumwa na Chama cha Mapinduzi ufanyike na kwenda kununua hizo shamba Morogoro na vitu vingine ambavyo ni vya kibadhirifu vilivyoumiza chama chake.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa unaipokea taarifa hiyo?

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitegemea utasema naye athibitishe kwa sababu anatuhuma watu kwamba wameiba.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa unazifahamu Kanuni ametoa taarifa, Kanuni inayohusu taarifa ni Kanuni ya 68 na uzuri tumeletewa na Mheshimiwa Spika hapa huna haja ya kubeba makaratasi, fungua Kanuni yako soma ya 68 amesimama kuhusu taarifa, unaipokea taarifa hiyo?

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, siipokei, his house kneegrow anyway.

MWENYEKITI: Eeeh! Halafu Mheshimiwa Msigwa, unajua tangu mwanzo nilikuwa nimekuacha na wewe unafahamu hayo maneno huko kwenye nchi unayoisema yana maanisha nini. Na wewe unasoma vizuri huwezi kuita Mbunge mwingine kama kneegrow, kama wewe unataka kujiita kneegrow ni suala lako wewe.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Haja-complain.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa…

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Haja-complain

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa…

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Ehehe! Hamna aliyelalamika.

MWENYEKITI: Natoa maelezo kuhusu jambo unalotakiwa kulifanya ndio ninacho…

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Haja-complain…

MWENYEKITI: Naomba ukae, naomba ukae. Siyo suala la yeye ku-complain kazi yangu mimi kusimamia utaratibu hakuna Mbunge anayeweza kuitwa kneegrow humu ndani hayupo.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kasema Mbowe mwizi, kasema Mbowe mwizi, kasema Mbowe mwizi, umenyamaza,

MBUNGE FULANI: Mwizi.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, si umenyamaza alivyosema Mbowe mwizi…

MWENYEKITI: Mheshimiwa, Mheshimiwa Msigwa tusibishane, nimesema nakuelekeza utaratibu, kama unataka kuusikiliza, sikiliza usijibizane na mimi. Nasema hizi maneno hayo kule yanakotumika yana maanisha kitu kibaya sana na wala hakuna mtu anataka kuitwa hayo maneno. Humu ndani hawezi kuitwa Mbunge mwingine hayo maneno kama mtu amelalamika, ama hajalalamika kazi yangu kusimamia utaratibu na nilikuwa nimekuacha tangu mwanzo ili umalize mchango wako halafu nije niseme mwisho ana maanisha nini, sasa kwa kuwa unaendelea kuyasisitiza hakuna Mtu anayeitwa jina hilo humu ndani, naomba uendelee na mchango wako. (Makofi)

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mpango ninachokisema kwenye kitabu chako ulituambia utasimamia democracy, tunaongea miaka mitano sasa tunamaliza kipindi chetu democracy ya nchi hii sasa hivi iko ICU, uhuru wa Vyombo vya habari ni disaster, waandishi wa habari wamekamatwa, wengine wamepotea, wengine hawawezi kujieleza, vyombo vingine vimekamatwa, Wabunge hawawezi kufanya mikutano kwenye majimbo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kubenea kwa mfano miaka miwili hawezi kufanya Mkutano, Mheshimiwa Halima hawezi kufanya Mkutano, Mheshimiwa Sugu hawezi kufanya Mkutano, Wabunge tunakatazwa, hii ndiyo democracy inayosema kwenye Mipango ya miaka yako mitano, na ulivyokuwa unazungumza Bajeti ya mwisho hapa ulinukuu mpaka maneno ya Mungu, ukasema Mungu atusaidie, ukanukuu na vifungu vya Biblia, halafu ukasema wananchi wakachague wagombea wa Serikali za Mitaa wanaotokana na Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo huu uchaguzi ambao unasema wakachague huu wa kupora, wa kupora kwa nguvu, katika nchi ya kidemokrasia, hebu vaeni vitu vyetu nimesema mna hiari mko wengi, leteni Muswada hapa kwamba tunafuta mfumo wa Vyama vingi tusijidhalilishe Duniani kwamba tuna democracy wakati hakuna democracy. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnaogopa, mnaweka mpira kwapani halafu mnashangilia, tumeshinda, tumeshinda… Unaweza kuwa champion bila kushindana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, the finishing line is for the winners, you cannot be a winner without competition, ingizeni mpira hapa, tuweke Wagombea wetu na ninyi muweke, tuone mziki wananchi wanamtaka nani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka mitano mmetuzuia, mmetuzuia muone tutakavyocheza mpira uwanjani, how do you call you self that you’re a champions. Watu wa Turkey, Waturuki wanasema when the fish is rocking it is start from the head. Hizi zote vurugu za Watendaji wa Mitaa na nini, ni matatizo ya Wizara, ni matatizo ya Serikali yenyewe, hiki kiburi cha kufunga Ofisi cha kufanya nini, msitudanganye, ni kwamba mmeona huko nje hali ni mbaya mlisema tumekufa, hatujafa, we are still standing. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mnajiaminisha mnaweza njooni uwanjani tucheze mpira, ili hayo uliyoyasema yathibitike tuweze kuendesha nchi nzuri ambayo Mungu ametupa, tusidanganye hapa, nakushukuru sana. (Makofi)