Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi name niweze kutoa mawazo yangu katika mapendekezo ya mpango ulio mbele yetu. Nilifikiria kwanza nina dakika 10 au 15 sina uhakika na dakika tano. Basi nitajitadi basi nilikuwa na mambo matano kwa ujumla wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza nilikuwa nataka niligusie ni kuhusu ufuatiliaji na tathmini (monitoring and evaluation) ya mpango wetu ulio mbele yetu. Mpango huu ni proposal ya kumalizia mpango wa miaka mitano 2016/2017, 2020/2021, lakini kwa bahati mbaya kilichoandikwa humu ndani kwenye ule mpango wa miaka mitano ni kwamba tungeweza kufanya tathmini ya mpango huu wa pili wa maendeleo wa taifa wa miaka hii ambayo tunaenda kuimalizia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni ngumu kufuatilia mapendekezo ya mpango wa kwenda kumalizia kama huku nyuma hatujajitathmini. Mpango wa kwanza umeisha na huu unaenda kuisha ukingoni bila kujitathmini tumewezaje kufanyakazi. Kuna umuhimu mkubwa sana wa kufanya tathmini kwa kuwa tathmini ndiyo inakupa dira ya nini tunafanya maelekeo yetu yakoje, kuna mabadiliko ambayo tunatakiwa tuyachukue ili tuweze kuboresha na kuweza kufanikisha malengo yetu.(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, huu mpango wa miaka mitano umeandika vizuri sana, hauna hata kasoro, kwa kweli umekaa technically correct. Sasa shida inakuja kwenye utekelezaji; kwa mfano ukurasa 128 (7.4.4) unaongelea mahususi kuhusu tathmini ya mpango wa pili huu wa maendeleo ambao tunaenda kuhitimisha, na kipengele cha pili pale kinasema kuwa kutakuwa namapitio ya muda wa kati wa utekelezaji;na tumeji-commit katika mpango huu kwamba tutaanzisha Mkutano wa Rais wa Mpango wa Pili wa Maendeleo katika muda wa kati wa utekelezaji ili kuangalia namna bora ya kubadili ama itaonekana ulazima wa kufanyia review. Sasa inakuwa ni ngumu kuendelea kutoa mapendekezo ilhali yale mapendekezo hatuyaoni yanafanyikaje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ambalo ninataka niligusie ambalo linahusiana na tathmini ni kwamba kumekuwa na changamoto nyingi sana ya upatikanaji wa fedha za maendeleo, maendeleo ndio huo utekelezaji wa mpango. Katika wizara na taasisi nyingi tumeshindwa kufika malengo, tuko below 50. Sasa tuna mpango ambao unaendana na nini tumekiamua na bajeti kiasi gani kiweze kutekeleza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona tuna changamoto ya kibajeti katika kutekeleza shughuli za maendeleo. Nilikuwa nategemea kwamba tungekuwa tumefanya tathmini ili tujiangalie ukusanyaji wetu wa mapato na mapungufu yake ni yapi ili tuweze kuboresha. Kwahiyo tunaenda kumalizia huu mpango wa pili lakini hatujui bado tunachangamoto za kimapato. Sasa ingekuwa ni vizuri basi; najua wataalamu wapo na uwezo huo tunao; tukapata huo mchanganuo kwamba setbacks zilikuwa ni nini ili kwamba huu mpango wa miaka mitano tunakwenda kuumalizaje.
Mheshimiwa Mwenyekiti,katika hili, kama tungekuwa tumefanya tathmini tungeweza kujionesha kwamba tumeutekeleza kwa asilimia ngapi katika sekta mbalimbali. Sasa hivi ni vigumu kusema kwamba sekta ya kilimo ina perform kiasi gani. Moja ya mfano, katika sekta ya kilimo ambayo ndiyo uti wa mgongo wa nchi yetu tunaoimba kila siku, ambao unaweza sasa kuubeba huo mpango wetu wa kusema uchumi wa viwanda. Tulijiwekea target kwamba tunapomaliza miaka hii mitano ya mpango kilimo chetu kingekuwa kimefikia kukua kwa asilimia 7.6 japokuwa huku pia huku pia napo inasomeka asilimia kumi naa! Hata hivyo ukiangalia kwa miaka hii mitatu iliyopita ile asilimia imeshuka, na huu mwaka ulioishia kilimo kimekua kwa asilimia 5.3. Sasa tulikuwa tunategemea kwamba tunapokaa hapa kama kamati tunatokaje ili kupandisha viwango hivyoambao tulijiwekea katika hii miaka mitano.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu na ambalo naomba niligusie ni kuhusu masuala ya ardhi. Imeandikwa pia vizuri sana katika kitabu chetu cha mpango ambapo sekta ya ardhi tumeona kwamba ni key katika maendeleo ya kiuchumi kwasababu ni rasilimali ambayo tunaiishi na tunaweza kuzalisha katika hiyo ardhi. Hata hivyo kumekuwa na migongano mingi ya jinsi ambavyo tunaweza tukaitumia ardhi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama unaweza ukarejea, ukurasa wa 110 kumekuja na njia mbalimbali na maboresho mbalimbali katika usimamizi wa matumizi bora ya ardhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika IV, V, VI, Serikali iliji- commit kuimarisha mfuko wa fidia wa ardhi ili kuondoa ucheleweshwaji wa malipo ya fidia baada ya kufanyiwa tathmini. Namba tano tuliji-commit kwamba kuna haja ya kufanya mapitio ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na.4 na Sheria ya Ardhi Na. 5; na commitment ya sita tuliweka kwamba kuhakikisha mipango sahihi ya matumizi bora ya usimamizi wa ardhi. Sasa tusipo-invest kwenye matumizi bora na usimamizi bora wa ardhi; tumeongea katikakamati yetu hata hotuba yetu ya Kambi ya Upinzani Bungeni imeongelea hiyo component;inabidi sasa tuwekeze. Tunasema tu tunaenda kufanya mambo ya viwanda, shughuli yoyote ya rasilimali yoyote lakini kama ile ardhi ina shida hatuwezi kuvuka; kama tunavyokwenda kuboresha miundombinu. Tumeona kuna tensions nyingi katika kutengeneza miundombinu ili kukuza uchumi lakini unaleta shida ya fidia kwa wananchi. Tumeona migogoro mbalimbali ya rasilimali kama ni kilimo au wafugaji kwenye masuala ya ardhi. Tumeona jinsi matumizi mabaya ya ardhi yanavyoleta matokeo ya mafuriko na kadhalika, yanaenda kuturudisha nyuma badala ya kusonga mbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nilikuwa naomba Serikali iangalie hili kwa upya. Kwamba kuna umuhimu sasa wa kuwekeza katika matumizi bora ya ardhi, tuwe tuna properplanning ya ardhi ili kuweza kutuvusha hapo na isiwe kikwazo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala langu la nne nafikiri, au ni la tano, linauhusiano moja kwa moja pia na ardhi. Mimi niko kwenye Chama cha Wabunge ambacho kinapigania masuala ya kutokomeza Malaria (TAPAMA). Moja ya issue ambayo tunaizungumzia, imekuja sasa wiki hii katika majadiliano yetu, ni jinsi mambo ya sekta ya afya yanavyo link moja kwa moja na sekta ya ardhi. Mfano bora ni kwenye masuala ya malaria. Serikali inatumia gharama kiasi gani katika kudhibiti malaria au katika kuleta tiba ya malaria.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ukiangalia, kinachosababisha Serikali inawekeza sana katika tiba katika afya ni kwasababu tunakosa matumizi bora ya ardhi; na wengiambao wanaguswa na kutokuwa na matumizi bora ya ardhi ni watu wa kima cha chini, na hawa watu wa kima cha chini ndio watu walio more prone kwenye magonjwa kama ni ya mlipuko au ni malaria. Sasa tukiwa tunamaboresho ya matumizi bora ya ardhi plus kuboresha makazi ya hawa wananchi basi tunaweza tukatokokeza haya magonjwa ambayo yanaturudisha nyuma kama wananchi kwasababu magonjwa haya yanaenda kutu- affectakili katika utendaji kazi na kutumia rasilimali kubwa ya nchi. Kwahiyo naomba Serikali iangalie jinsi yaku–link up matumizi bora ya ardhi na shughuli za kiuchumi na shughuli za kiafya na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti,…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante sana Dkt. Sware
MHE. DKT. IMMACULATE S. SWARE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi, ahsante.