Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, mwingi wa utukufu kwa kunipa uzima ili nami niweze kusimama hapa leo kuweza kuchangia Kamati zote tatu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza na suala la utawala bora. Nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Rais, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli; nampongeza Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan; nampongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kwa utendaji mzuri wa kazi unaozingatia suala la utawala bora. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utekelezaji wa majukumu ya Rais tangu amekuwa Rais toka mwaka 2015, pamoja na kazi nyingi sana alizozifanya za kuhakikisha kwamba Tanzania yetu inaendelea kupaa kiuchumi, leo hii nitataja baadhi tu ya mambo ambayo ameyafanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kusimamia kwa makini kabisa suala la rushwa; matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za Taifa; amesimamia suala la kuondoa watumishi hewa; na ametoa elimu bure. Mpaka sasa tangu elimu bure imeanza kutolewa ni fedha zaidi ya shilingi trilioni moja ambazo zimetumika. Hongera sana Mheshimiwa Rais. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kuimarisha mikopo ya elimu ya juu. Hakuna malalamiko wala maandamano. Ahsante sana Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Rais amesimamia ujenzi wa Stiegler’s Gorge; zaidi ya pesa trilioni sita zimetolewa; amesimamia vizuri miradi ya maji inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu; amesimamia suala la Vituo vya Afya kuhakikisha kwamba anatoa fedha vituo 352 vinajengwa; ndege nane zinanunuliwa; hospitali 67 mpya; na hospitali za mikoa tano. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais ameendelea kutekeleza majukumu yake. Amekubalika ndani ya nchi, nje ya nchi na Bara zima la Afrika. Ndiyo maana amepata nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Nchi zote 16 za SADC. Tuna kila sababu ya kumpongeza Rais wetu. Haya ni baadhi tu ya mambo machache ambayo Mheshimiwa Rais amefanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumzia suala la utawala bora, sijakusudia kuchoma sindano lakini kwa sababu nasikia sauti za wanawake wenzangu wanachoma choma sasa naenda kuchoma sindano. Tunapozungumzia suala la utawala bora ni vizuri pia tukaangalia hata kwenye vyama vyetu, hali ikoje? Kweli tuko kwenye misingi ya utawala bora au tunapiga kelele tu kwa upande wa pili wakati sisi wenyewe hatuko vizuri kwenye suala la utawala bora?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakwenda kwenye Chama ambacho ni cha Demokrasia na Maendeleo. Chama hiki ukiangalia katika uchaguzi uliopita…
(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Tulieni mpate elimu kidogo. Katika uchaguzi uliopita, viongozi wote waandamizi wa chama hicho wamewekwa kwa maana ya udini; ni Wakristo watupu. Pia, ukienda katika hoja hiyo hiyo, ukiangalia katika Kanda ya Arusha kuna bwana mmoja anaitwa Ali Bananga…
MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utaratibu.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: …aligombea nafasi na akaenguliwa. Huo ni ubaguzi wa hali ya juu. Pia ukienda…
MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utaratibu.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: …kwa Mheshimiwa Sumaye, alifanyiwa kampeni ya kupigiwa kura za hapana. Huo ni ubaguzi wa hali ya juu sana. Vile vile ukienda kwa suala la Mheshimiwa Joseph Selasini aliondolewa kwenye nafasi ya Chief Whip kimtindomtindo tu…
(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Sasa suala la utawala bora hapa likoje? Tunapozungumzia suala la utawala bora, suala la utawala bora likoje?
MHE. ESTER A. BULAYA: Mwongozo wa Spika.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue nafasi hii...
(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)
MHE. ESTER A. BULAYA: Mwongozo wa Spika.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue nafasi hii kusema kwamba tunapozungumzia suala la utawala bora katika huko huko…
MHE. ESTER A. BULAYA: Mwongozo wa Spika.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: …upande huo huo wanaopiga kelele kuna ndoa za jinsia moja. Sasa unapozungumzia…
MBUNGE FULANI: Choma sindano, choma sindano.
(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Au unapofanya vitendo vya ndoa ya jinsia moja…
MBUNGE FULANI: Rudia hiyo ya jinsia moja hiyo!
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni sehemu ya utawala bora?
(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)
MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hatujaskia hiyo ya ndoa. hiyo ya ndoa hiyo!
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Hii sio sehemu ya utawala bora…
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Ndoa za jinsia moja upande huo siyo sehemu ya maadili. Siyo sehemu ya utawala bora.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi za Afrika…
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi za Afrika, Tanzania imetajwa kwamba ni nchi ambayo inathamini na kujali suala la utawala bora. Imeshika nafasi ya juu kabisa…
MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mwongozo.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: …na ndiyo maana wamejitokeza baadhi ya wanasiasa wanakwenda kuropokaropoka hata nje ya nchi, akiwepo Mheshimiwa Zitto Kabwe, akiwepo Mheshimiwa Tundu Lissu na wengine wengi. Akina Mheshimiwa Lema hawa.
(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nizungumzie suala la TRA.
MBUNGE FULANI: Mwenyekiti una double standards.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Naomba nizungumzie suala la TRA.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Jacqueline, malizia dakika moja.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia. tunapozungumzia suala la utawala bora tujiangalie na sisi.
MBUNGE FULANI: Majambazi wako kule, akina Lema.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Majambazi wako upande huo! Ndoa za jinsia moja ziko upande huo! Hii siyo sehemu ya utawala bora. (Makofi)
(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)
MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utaratibu.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji) MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Jacqueline, umemaliza muda wako.