Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Hon. Yosepher Ferdinand Komba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi

MHE. YOSEPHER F. KOMBA: Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika Sekta ya Mifugo na Uvuvi inaajiri takribani 50% ya Watanzania ambao ni zaidi ya milioni 25 na inachangia zaidi ya 6% kwenye pato la Taifa.

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Uvuvi; Operesheni Jodari imeacha madhara mengi hasi kuliko chanya, Wavuvi wamepigwa, wamechomewa nyavu, vibali vimekuwa vingi, wamenyang’anywa mitumbwi na kadhalika. Naomba Serikali ifuatilie na kuona madhara yanayotokana na operesheni hii na nini kauli ya Wizara kwa Watendaji waliokiuka sheria na taratibu katika kufanya zoezi hilo na Serikali (Wizara) iko tayari kuwarejeshea wale wote walionyang’anywa vyombo vyao kinyume na utaratibu.

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa kitoweo cha samaki; kumekuwa na changamoto na uhaba mkubwa wa kitoweo cha samaki hasa wanaotoka maji chumvi (baharini) na ukiwauliza wavuvi, wanasema kuna makatazo kutoka Serikalini, ukiwauliza wafanyabiashara na wenye mabucha, wanasema baada ya samaki kutoka nje kukatazwa na wavuvi wetu wa ndani kuvua kwa kificho baada ya Serikali kutoa katazo na kunyanyasa wavuvi hivyo kama mfanyabiashara atabahatika kuwapata samaki wa maji chumvi basi bei huwa juu sana na hivyo hawapati wateja.

Mheshimiwa Spika, naomba Waziri atuambie kwa nini samaki wa maji chumvi wameadimika na nini mkakati wa Wizara kuhakikisha samaki wanapatikana?