Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Madini

Hon. Yosepher Ferdinand Komba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Madini

MHE. YOSEPHER F. KOMBA: Mheshimiwa Spika, machimbo ya dhahabu ya Amani yapo maeneo katika Tarafa ya Amani, Wilayani Muheza ambapo wananchi wa kawaida wamegundua madini katika eneo lile. Ni kwa bahati mbaya sana baada ya kuanza kuchimba Serikali kupitia Halmashauri walisitisha uchimbaji, kukamata watu na kuwaumiza. Mpaka sasa hakuna utaratibu wowote ulioandaliwa kwa wananchi wanaozunguka mradi/mgodi ule. Je Wizara iko tayari kuweka utaratibu mzuri kwa wachimbaji wadogo ili waweze kujipatia kipato? Pia Wizara wana utaratibu gani wa kuwapa mtaji wachimbaji wadogo ili waweze kujikwamua?

Mheshimiwa Spika, Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative; Taasisi hii imepewa jukumu kubwa la kusimamia uwazi na uwajibikaji, lakini kwa bahati mbaya haipati fedha za kutosha kufanya shughuli zake. Napenda kufahamu ni kwa nini Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative haipati fedha zilizotengwa kwa wakati na kwa ukamilifu. Je Kanuni zinazoongoza utendaji wa TEITI zimeshatoka na zimeanza kutumika?

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.