Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

Hon. Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi ningependa kushukuru sana kupata nafasi hii kuweza kuchangia hoja hii ambayo ni muhimu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ningependa kumpongeza sana Waziri na Naibu wake pamoja na Katibu Mkuu na watendaji wote; kazi ambayo wanaifanya kwa kweli ni kubwa sana na inahitaji kupongezwa. Nakumbuka wiki iliyopita nilikuwa na Waziri kwenye kijiji change kimoja ambacho aliloa tope kabis akutokana na mvua, lakini aliweza kudiriki kuweza kuwasha umeme kwenye baadi ya vijiji. Nakushukuru sana, na namshukuru pia Naibu Waziri ambae ni mwenyeji sana Muheza na tumempa kadi pale kwa hiyo karibu sana na wametembelea sana Jimbo langu la Muheza.

Mheshimiwa Naibu Spika, REA awamu ya tatu Muheza tulibahatika kupata vijiji 19 lakini nasikitika kusema, na Naibu Waziri na Waziri wana habari kabisa kwamba mkandarasi ambaye yuko pale Radi ni mkandarasi ambaye ni mbovu sijawahi kuona. Kati ya vijiji 19 katika muda wa miezi 10 ameweza kuwasha umeme kwenye vijiji vitano tu. Kwakweli inasikitisha lakini Mheshimiwa Waziri nilikumbuka na nilikuambia kwamba tafadhali sana naomba vijiji vingine ambavyo vingekuja labda kwenye awamu ambayo itakuja Awamu ya Pili, REA III vijiji 28 basi uweze kuniwekea na uweze kunitafutia mkandarasi ambaye kwakweli ni mzuri. Nitakushukuru sana endapo utatimiza ahadi hiyo. Isipokuwa nakushukuru sana kw ajuhudi za kuweza kum-force huyu mkandarasi aweze kuweka umeme kwenye sehemu mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vizuri kwenye Awamu ya III ya REA round ya pili hii mikataba ya hawa wakandarasi ikaangaliwa vizuri; na ni vizuri kama masuala ya transformer, masuala ya nguzo na nyaya basi ikanunuliwe moja kwa moja kwenye makampuni ambayo yanahusika badala yake kunakuwa na mikataba mingi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo ningependa kujikita sasa kwenye mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia (LNG), mradi huu ni mkubwa na muhimu sana, Mheshimiwa Waziri na Wizara yako ni vizuri sasahivi mkajielekeza kwenye gesi asilia kwenye huu mradi wa LNG. Serikali haijaipa uzito unaostahili mradi huu. Mradi huu ni muhimu sana, na mimi nakumbuka kabisa kwamba mradi huu unaweza ukainua uchumi wa nchi hii kwa nafasi kubwa sana. Makampuni ambayo yalikuwa kwenye huu mradi baadhi yao wameshaondoka na wamekwenda Msumbuji.

Mheshimiwa Waziri, Msumbiji, mradi huu wa LNG sasahivi Msumbiji wanauzindua mwezi ujao tarehe 18, iko kwenye press, na mradi utakuwa ni plant moja kubwa sana katika Afrika na Ulaya. Sasa hatuwezi kuacha hiyo nafasi tukaanza kucheza mradi huu. Nakuomba kabisa Mheshimiwa Waziri elekeza nguvu sasa kwenye huu mradi wa LNG tuweze kuinua huu uchumi kwa bidii sana…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Kengele imeshagonga Mheshimiwa. Ahsante sana.

MHE. BALOZI. ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)