Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Hon. Ajali Rashid Akibar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

MHE. AJALI R. AKBAR: Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii kukushukuru wewe mwenyewe kwa kunipa nafasi ili kutoa mchango wangu katika Wizara hii nyeti, Wizara ambayo kwa kweli ni Wizara mama ambayo sisi binadamu tunaitegemea. Wizara hii inatokana na unyeti wake kwamba bila ardhi maana yake hakuna dunia na bila dunia maana yake hakuna maisha, kwa hiyo Wizara hii lazima iwe makini katika kuhakikisha kwamba wanasimamia vizuri jinsi ya kupima ardhi na jinsi ya kupanga ardhi hii.

Mheshimiwa Spika, sina shaka na utendaji wa Mheshimiwa Waziri, sina shaka juu ya utendaji wa Mheshimiwa Naibu wake, Katibu Mkuu pamoja Watendaji wote waliopo kule Wizarani. Kwa kweli wanaitendea haki Wizara hii na wanafanya kazi kama ipasavyo; a Leader is a one who finds the way, is the one who shows the way, Waziri yeye ni kiongozi ambaye ametafuta njia na ameonesha njia.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ninachotaka kuzungumza kwamba hao wanaosema kwamba yeye anatembea, nadhani kwamba yeye ndiye kiongozi ambaye anatafuta njia halafu anaonesha wale watu waliopo chini ili wajue nini wanatakiwa kukifanya nampongeza sana Mheshimiwa Waziri katika utendaji huo.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze tena Mheshimiwa Waziri au niipongeze Wizara hii kwa kupunguza viwango hivi vya kodi ya ardhi kutoka asilimia saba hadi asilimia moja, nyingine asilimia mbili kwa maeneo ambayo yamepangwa na 150,000 kwa ajili ya gharama zile za upangaji. Viwango hivi ni vizuri, lakini sijui kama hizi huduma zote zinawafikia wananchi properly, kwa sababu kwa mfano halmshauri ya Wilaya ya Newala ni mji ambao ulikuwa umepangwa siku nyingi sana. Hata hivyo, kwa bahati nzuri wengine wana hati lakini wengine hawana hati. Kwa wale ambao wana hati bahati nzuri ni kwamba vile viwango vya jinsi ya kulipia kodi ya ardhi vinakuwa vimeoneshwa kwenye hati, lakini wale watu ambao wengine maybe hawana hati inakuwa ni tatizo kwamba inakuwa ni majadiliano kati ya Afisa Ardhi pamoja na yule ambaye hana hati.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo watu wengine wanashindwa kwenda kujenga nyumba sababu yale maeneo wanaambiwa mpaka zile kodi ambazo ni za siku nyingi. Kwa hiyo Waziri afanye utaratibu wa kuhakikisha kwamba Wizara inatoa viwango katika Halmashauri za Wilaya zote kutegemeana na wilaya jinsi ilivyo na hivyo viwango vibandikwe sokoni, hospitali na katika majengo ya halmashauri ili kila mmoja hivi viwango avione, badala ya hizi nyaraka ambazo wanakaa nazo wale Maafisa Ardhi badala yake wawe wanakuwa na mjadala wa kujadiliana namna gani. Kwa hiyo mtu anafikia mpaka milioni tatu, aidha mtu anakimbia anashindwa kujenga au baadaye unampa kidogo inapungua mpaka kufikia 200,000 au 300,000. Kwa hiyo ninamwomba Mheshimiwa Waziri aondoe loopholes kama hizi, hivyo viwango viwe wazi.

Mheshimiwa Spika, la pili ni kwamba, kuna maeneo Wizara imekiri kwamba maeneo mengi hayakupimwa. Naona sasa umefikia wakati Mheshimiwa Waziri aangalie hili jambo la kupima au kupanga miji yetu liwe ni jambo la kisheria. Kila halmashauri ihakikishe kwamba inapima hayo maeneo yake ili kupanga hiyo miji ili isiwe ni miji ambayo imekaa hovyohovyo. Katika karne ya leo tunazungumzia mambo ya squatter, kwa kweli nashangaa sana.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niombe kama inawezekana Mheshimiwa Waziri ahakikishe kwamba yale maeneo ambapo halmashauri wanashindwa kupima, basi wawe na utaribu hawa wapima binafsi waende katika kila halmashauri wafanye makubaliano rasmi ili kuhakikisha yale maeneo wanayapanga na hatimaye kuyapima ili kuepuka hizi squatters, kwa kuwa Mheshimiwa Waziri amesema maeneo mengi hayakupangwa wakati huo.

Mheshimiwa Spika, lingine, kuna huu utaratibu ambao nilikuwa nategema majiji mapya kama kwa mfano yalivyo Dodoma, tulitarajia kwamba katika miaka 30 inayokuja kusiwe tena na squatter katika Jijiji la Dodoma. Kwa hiyo niombe sana zile halmashauri ambazo zinazunguka Mji wa Dodoma kwa mfano Chamwino na labda Bahi na Halmashauri ya Mji zote hizi ziingizwe katika jiji ili kuhakikisha kwamba hayo maeneo hayawi na squatter tena. Kama yatakuwa yameingia katika jiji maana yake kwamba kutakuwa na mpango, leo nimepita pale katika ule Mji wa City kilometa moja kuanzia pale Mheshimiwa Waziri watu bado wanaendelea kujenga bila kupanga, ni mambo ya ajabu sana. Kwa hiyo maana yake baada ya miaka 25 pale sasa Serikali itabidi iwalipe fidia wale watu wote halafu tuhakikishe tena tunaanza kupanga tena upya.

Mheshimiwa Spika, naamini kwamba katika karne hii tusirudi tena Serikali ikaingia katika gharama ya kuwalipa fidia ili tuangalie namna gani jinsi ya kupanga. Sasa ni wakati ambapo tuhakikishe kwamba kila jiji na kila mji unakuwa na Master Plan ambayo itakuwa ya miaka 30 au miaka 50 au miaka 100 inayokuja ili baadaye labda tupate gharama ya kubadilisha tu jinsi ya matumizi, lakini ikiwa hii miji yetu imepangwa vizuri na inakuwa inaonekana na movement zinazoonekana kila sehemu.

Mheshimiwa Spika, si vizuri katika miaka 30 ijayo tuwe na miji ambayo haikupangwa, maana nategemea kwamba baada ya muda fulani hakutakuwa na kila mmoja anaishi ktika nyumba yake ila tutakuwa na majumba makubwa ya Serikali kama wanavyofanya Serikali zingine duniani na kila mmoja hatapewa nyumba ya kuishi kwa wakati huo. Nasema hivyo kwa mfano ambayo kama nimezungumza kwamba hapo Buigiri hapajapima na halmashauri zingine bado wanamiliki, vilevile sisi ni kazi yetu.

Mheshimiwa Spika, lingine, nipongeze kuwa na Ofisi za Kanda, katika Mkoa wa Mtwara hiyo Ofisi ya Kanda kwa ajili ya upimaji wa kwa kweli Mheshimiwa Waziri anaitendea haki, wale wale watu kwa kweli ni watendaji wa kazi vizuri sana. Kama matatizo tunayapata ni baadhi ya halmashauri wao wenyewe wanashindwa kutengeneza zile documents lakini siyo Ofisi ya Kanda kwenda kule wewe ukapata hati ukaa miezi sita. Kwa kweli wale watu wanafanya kazi vizuri sana, Mheshimiwa niombe kwamba kwa kweli wale watu wanaitendea haki Wizara, ila halmashauri zingine bado zinakuwa bado zinavuja, kwa mfano Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ukipeleka document pale inakaa muda mrefu sana, kuna watendaji ambao bado wana matatizo.

Mheshimiwa Spika, ukienda Newala au Mtwara Mjini penyewe wakishaandaa zile documents, zikifika katika Ofisi ya Serikali, basi inakuwa ni muda mfupi sana unapata hati yako. Nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri katika hili. Narudia tena a Leader is a one who finds the way, is the one who shows the way, Mheshimiwa Waziri anatafuta njia halafu anaonesha. Nimpongeze katika hili, aendelee katika utendaji wake.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru, mchango wangu ulikuwa mfupi kiasi hicho. Ahsante sana. (Makofi)