Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia hotuba ya bajeti kuu ya Serikali. Nianze kwa kusema kuwa, natambua zipo sekta mbalimbali zinazochangia katika ukuaji wa uchumi wa wananchi na pato la Taifa, zikiwemo sekta za madini, mawasiliano, fedha, kilimo na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ya kilimo ndiyo inachangia kwa asilimia kubwa na kutoa ajira kwa wananchi kwa wingi na hivyo kuondoa hali ya umaskini kwa wananchi. Hivyo basi, ni vyema Serikali ikawekeza kwenye kilimo kwa kutenga bajeti ya kutosha, bajeti ikiwa ni kubwa, mambo yafuatayo yataweza kutekelezwa:-
(a) Kufanya tafiti ya ardhi gani inafaa kwa zao lipi katika kila mkoa;
(b) Kufanya tafiti ya mbegu bora ili kuongeza uzalishaji ulio bora;
(c) Kuajiri Maafisa Ugani ili watoe elimu kwa wakulima ili walime mazao yenye viwango vya juu kwa ajili ya export na viwanda vya ndani; na
(d) Kuwekeza kwenye Taasisi ya Zana za Kilimo - CAMARTEC ili kukuza kilimo cha kisasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, tukiweza kuwekeza kwenye kilimo ndipo viwanda na sekta zingine zitakua.