Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CUF
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. SONIA J. MAGOGO: Mheshimwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia kwenye hotuba hii ya Waziri Mkuu. Moja kwa moja nitaenda kuanza kwenye suala hili ambalo limekuwa kama ni janga la kitaifa ugonjwa huu wa corona na cosign yangu moja kwa moja itakuwa kwa watu vijijini. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ukiangalia sasa hivi sisi watu wa mijini tunapata hizi taarifa za ugonjwa wa corona kupitia kwenye mitandao na vyombo vya habari, lakini ukitathimini kwenye vijiji vyetu sehemu nyingi hawana access ya hii mitandao. Kwa hiyo, Napata shaka kidogo kwamba nao wanaweza wakawa na ufahamu ama kupata taarifa sahihi kwa kiwango kile ambacho sisi watu wa mjini tunapata.
Mheshimiwa Spika, wakati huo huo mjini tumeona sasahivi maeneo mengi tunatumia maji na sababu kunawa mikono ili kujikinga na haya maradhi ya corona. Lakini kwa vijiji vyetu maeneo mengi wanauhaba wa maji, unakuta haya maeneo mtu hata yale maji kujikimu yale mahitaji ya muhimu anashindwa kuyapata. Sasa sidhani kama mtu anatafuta maji kilometa kadhaa anakuja na ndoo moja kwa ajili ya kupata maji walau ya kupikia kama anaweza akayatumia yale maji kwa ajili ya kusafisha mikono kama tunavyofanya huku mijini. (Makofi)
Mheshimwa Spika, hivyo ningeiomba Serikali iangalie inawasaidiaje hawa watu wa vijijini, kama inawezekana kuwapatia hizi sanitizer ili waweze kuzitumia ziwe mbadala wa maji kule vijijini, kwa sababu tuta-control mjini peke yake na vijijini kukawa bado kuna hiyo loophole ya kueneza huu ugonjwa bado kuna watu wanatoka vijijini wanakuja mjini, bado kuna watu wanatoka mjini wanawenda vijijini. Kwa hiyo maambukizi bado yatakuwa na nafasi kubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pia tumeona kwa Mkoa kama Mkoa wa Dar es Salam sasa hivi bodaboda zimekuwa kama ndiyo kama ndiyo nafasi kubwa sana ya usafiri na wameruhusiwa sasa hivi mpaka kuingia katikati ya mji, lakini wasiwasi wangu unakuja kwenye zile elementi ambazo wanavaa abiria, kwa sababu akivua abiria mmoja anakuja kuvaa abiria mwingine na huwezi kujua kati hao ni nani anaweza akawa na virusi vya corona.
Mheshimwa Spika, kwa hiyo, niombe kama inawezekana walau huu utumiaji wa elementi uzuiwe kwa kipindi ili kuepusha haya maambukizi kuenea kwa kasi. Sambamba na hili nilikuwa napenda kuishauri Serikali, kwa upande wa wauguzi ina maana manesi na Madaktari, ningependa kufahamu Serikali imejipangaje ili kudhibiti haya maambukizi kwa hawa watu ambao wanakuwa direct moja wka moja wanakuwa na direct contact na wale watu ambao wana virusi vya corona. Lakini wakati huo huo tunaona maeneo mengi kuna uhaba wa Madaktari nitolee mfano kwenye Wilaya yangu ya Handeni.
Mheshimiwa Spika, lakini wakati huo huo tunaona maeneo mengi kuna uhaba wa madaktari. Nitolee mfano kwenye Wilaya yangu ya Handeni. Wilaya ya Handeni katika Hospitali yetu ya Wilaya ina madaktari watano na tuna uhaba wa madaktari karibia 24. Hospitali ile imekuwa ikisaidia hadi Wilaya za jirani kama Kilindi na Manyara. Kwa hiyo, ukiangalia huo uwiano wa madaktari ambao tunao pale na ukubwa wa eneo ambalo wanatoa huduma na hili janga la Corona ambalo lipo inatupa mashaka makubwa. Hivyo niiombe Serikali iangalie uwezekano wa kuongeza bajeti kwenye Kitengo cha Afya ili kuweza kuendana na hii hali ambayo tunayo sasa hivi.
Mheshimiwa Spika, suala lingine naomba kuongelea kuhusu miundombinu, miundombinu yetu sasa hivi imekuwa mibaya sana kutokana na hizi mvua ambazo zimenyesha. Ukiangalia hata hapa Dodoma tu maeneo mengine kufikika imekuwa ni tatizo kubwa sana. (Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
SPIKA: Ahsante sana.
MHE. SONIA J. MAGOGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)