Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nipende kumshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Mwigulu Nchemba Waziri wa Fedha kwa hotuba yake nzuri ya mpango ambao tunaujadili kwa sasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kwenye mpango huu naomba nizungumzie jambo moja tu ambalo linahusu sekta ya michezo; na mimi ni mdau wa michezo na nimekuwa kiongozi wa michezo kwenye nchi hii. Kwa leo naomba niitakie kila la heri timu ya Simba Sports Club kwenye mchezo wake pale Misri, na ninaamini kwamba hata wanayanga wenyewe wanaendelea kutuunga mkono kama ambavyo imekuwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye michezo naomba nizungumzie mambo kadha wa kadha. Ninaanza na jambo suala la sheria namba moja kwenye kanuni 17, sheria 17 za mpira wa miguu ambazo zinahusu mambo ya viwanja vya mpira.
Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania tumebahatika sana, takriban kila mkoa tunaviwanja vya mpira wa miguu. Serikali kwa muda mrefu lakini pili sisi kama Chama cha Mapinduzi kwenye ilani yetu kwa muda mrefu tumekuwa tukiweka kwamba tunauwezo na tunafursa ya kuviendeleza viwanja vyetu vya mpira wa miguu. Ukienda ukurasa namba 30, 245 kwenye ilani ya mwaka huu inazungumzia ujenzi wa viwanja kwenye Taifa letu.
Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tulibahatika Mwalimu Nyerere alijenga viwanja maeneo mazuri na viwanja vikubwa ambavyo hadi leo kizazi hiki inavitumia. Hata hivyo sijaona mpango wa moja kwa moja kwa Serikali na Chama cha Mapinduzi ambao ni wamiliki wa viwanja hivi kuendeleza viwanja vya mpira wa miguu. Tumeishia kulalamika kwamba viwanja sio bora, sio vizuri lakini hakuna hatua ya moja kwa moja ambayo Serikali imekuwa ikifanya na kuichukua kwa kuhakikisha kwamba inaviendeleza viwanja hivi.
Mheshimiwa Naibu Spika, niiombe na niishauri Serikali. Viwanja vipo maeneo mengi na maeneo potential, viwanja kama Sokoine, CCM Kirumba, Ali Hassan Mwinyi – Tabora, vinahitaji tu fedha ya kuweka hata carpet tu mpira uchezwe kwa sababu majukwaa Nyerere alishatujengea, yako imara na yako vizuri, kinachohitajika ni fedha tu zitengwe kwa ajili ya kuweka hata carpet.
Mheshimiwa naibu Spika, niunganishe moja kwa moja, tunahitaji kuwa mpango wa moja kwa moja. Sisi wote hapa tunafurahia leo, kwamba timu zinacheza vizuri, Timu ya Simba, timu ya taifa zote zinacheza vizuri, lakini ikifungwa tunaanza kulaumu. Hata hivyo kusudi na malengo ya moja kwa moja ya Serikali kuendeleza michezo hatujaiona. Tunazungumzia viwanja hivi lakini hadi sasa hatujaona Serikali ikitoa kodi kwenye vifaa vya michezo. For instance, hizo carpet ambazo tunazizungumzia, ingetenga hata mwaka mmoja kwamba huu ni mwaka wa exemption kwenye vifaa vya michezo kwa ajili ya kutandika carpet kwenye nchi yetu; hata viwanja viwili viwili tu kwa kila mwaka, kwa muda wa miaka mitano tunaviwanja 10 vimetandikwa kapeti mpira wetu unachezwa na watoto wanaweza kupata sehemu ya kuchezea.
Mheshimiwa Naibu Spika, niiombe Serikali iondoe kodi au iweke tax exemption kwenye vifaa vya michezo; kuanzia jezi lakini pia hizo carpet ambazo tunaweza tukazitandika kwa ajili ya viwanja vyetu hapa nchini.
Mheshimiwa Naibu pika, jambo linguine, zamani wakati tupo na timu ya taifa tulikuwa na shule nyingi ambazo zinazilisha wachezaji; mathalani shule kama ya Makongo, ambayo ilizalisha wachezaji wengi ambao tulikuwa tunawasifia wakina Kaseja na wachezaji wengine. Tunaomba mpango wa makusudi wa Serikali kujenga shule maalum kwa ajili ya michezo kwenye taifa hili. Shule ambazo either zinaweza zikawa za zonal kwa maana ya kanda kama Dodoma, Mbeya, Mwanza na hata Kusini wajenge shule angalau 10 au tano za michezo tu ambazo zitakuwa zina- feed timu yetu ya taifa na vilabu vyetu vya Tanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa muda mrefu wachezaji wetu ambao tunao hapa hawana uchezaji wa mpira ambao umepitia kwenye darasa, wengi wametokea mitaani, hawana shule maalum kwa ajili ya taifa letu ambazo zinasimamiwa ama na TFF ama na Serikali. Tunahitaji kuwa mpango wa muda mrefu kuhakikisha kwamba michezo ya taifa hili inakuwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimuombe sana Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha, yeye ni mdau wa michezo wa moja kwa moja. Leo hii yeye ni Waziri wa Fedha; aone haja ya moja kwa moja kuinua soka la nchi hii. Amekuwa na club ya Singida United na amewaona jinsi ambavyo ni ngumu kuiendesha; ni kwa sababu timu nyingi hazina fedha. Je? haoni sasa kuna haja ya Serikali, kama nilivyosema, kuondoa kodi kwenye hivyo vifaa? Na isiwe tu kuondoa kodi kwenye hivyo vifaa, lakini pia kampuni, kama betting companies, ambazo zipo ndani ya nchi hii zizonafanya kazi za betting nchi hii haziwezi kujiendesha kama si mpira, maana yake wananufaika moja kwa moja na mpira wetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, je? Serikali haioni fursa kwa sasa, kwamba kampuni zote za betting ziwekewe angalau sheria au utaratibu? Kwamba kila kampuni ya betting iwe na uwezo wa ku-finance au kuchangia au ku-sponsor timu yoyote ya ligi kuu? Ziwe za wanawake au timu ya taifa, au timu hizi ambazo tunazo kwa sasa?
Mheshimiwa Naibu Spika, tuione fursa ili betting companies ziweze ku-support kwenye mpira wa Tanzania kwa sababu nazo existence yake, uwepo wake hapa nchini ni kwasababu ya mpira wetu. Kwa hiyo nimuombe Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Serikali muone haja ya kuweka mazingira salama kwa ajili ya timu zetu kuweza kupata fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuendesha timu za ligi kuu ni kazi ngumu sana, vijana hawa hawana hela, hawana fedha, tunahitaji hatua za makusudi kuwa-support, na kuwaunga mkono.
Mheshimiwa Waziri wa Fedha nikusihi na nikuombe, tax exemption kwenye vifaa vya michezo lakini pili hizi kampuni zingine za betting; lakini si kampuni za betting tu. Tuchukue hata utaratibu ule wa Zambia kipindi cha Kenneth Kaunda kwenye kampuni ya migodi; aliamua kutangaza wazi kama kuna kampuni ipo tayari ku-finance vilabu vya ligi kuu vya nchi yetu; ile KK11 ilikuwa financed na makampuni ya migodi, kwamba tutawaondolea sehemu ya kodi hiyo kodi ipelekwe kwenye michezo; fanyeni hivyo ili msa-port michezo ya nchi yetu hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo lingine ambalo nataka nizungumzie, sitazungumza kwa muda mrefu sana; ni jinsi gani ambavyo tunaweza kulinda wawekezaji kwenye michezo yetu? Nataka hapa niweke case study ya Simba Sport Club na hata Young African wanatuunga.
Mheshimiwa Naibu Spika, Simba imepata uwekezaji ambao wanahainga nao na upo kwenye public na Serikali imeingilia kwamba inasimamia ule mchakato uende salama, the same to Young African, wana uwekezaji ambao mchakato wake wameshauanza. Sasa, je wawekezaji wetu wanalindwa? Hawalindwi, intimidation na frustration kwa wawekezaji wetu zimekuwa ni kubwa kwa kiwango ambacho wawekezaji wakati mwingine wanataka hata kukata tamaa. Simba leo ambao tunajivunia, kila mmoja anajikonga kifua kwamba ni Simba kwa sababu inafanya performance ni kwa sababu muwekezaji yule ameweka fedha pale, ameweka fedha lakini kuna watu wanajitokeza wanawa-frustrate kati kati ya mapambano.
Mheshimiwa Naibu Spika, Simba leo ikibeba klabu bingwa Africa, Tanzania itatangazwa all over the world. Si hivyo tu pia tutafungua nafasi kwa mawakala wa wachezaji kuja kufuatilia soka letu la Tanzania. Je, wawekezaji wetu wanalindwa? Serikali ione haja, watu ambao wana- frustrate wawekezaji, kama Mheshimiwa Rais alivyosema, wawekezaji wasibughudhiwe. Yule mwekezaji si mwizi, mchakato upo open kabisa, uko wazi lakini amekuwa frustrated kwa muda mrefu. Akifanya hiki huyu anaingia anasema hivi, akifanya hiki huyu anaingia anasema tunakata bilioni 20. Bilioni 20 hasa hasa kwa Simba Sport Club? Kwa posho ya mwaka huu is over one billion, posho tu. Mwekezaji anaweka over 1.5 billion ruzuku, what is bilioni 20 kwa Simba iliyookolewa hapa.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuombe uwezekano wa Serikali kulinda wawekezaji ambao wanaingiliwa, hasa kipindi kama hiki ambacho Simba inaenda kuchukua ubingwa na kuweka historia kwenye taifa letu. Kwa hiyo lazima tuwalinde.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunalisema hili kimasihara, lakini niseme wazi, Simba inaenda kuandika historia nyingine. Je, hii historia inayoenda kuandikwa inalindwa? Simba inaenda kwenye robo fainali mtu mwingine anajitokeza anatoka billioni 20, billioni 20 za nini? mshahara wa Chama, mshahara wa Bernard Morrison ni zaidi ya billioni 20. Mtu kaamua kuwekeza kwa maslahi na mapenzi ya soka Tanzania, ni vema akapewa heshima na akalindwa. Serikali ione haja ya kuwaita pembeni watu ambao wana-frustrate na ku-intimidate na kuwaambia kwamba huu mchakato haujaisha na si mchakato wa wizi, ni mchakato uko wazi na wanasimba wameridhia kwenye mkutano mkuu wao.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuombe, Serikali iendelee kulinda. Vilevile na Dar Young African tunawatakia kila la heri, tunajua nanyi mnaenda huko, mnatufata sisi, tunaamini mtafanikiwa. Sasa na ninyi mkiruhusu michakato hii watu kuingilia wawekezaji watakata tamaa, GSM watajitoa pale Yanga kwa sababu watu hamlindi wawekezaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo lingine ni kuhusu suala la kusaidiwa kwa TFF. TFF ni chombo chetu ambacho tunacho, kinafanya kazi, lakini mzigo wa TFF ni mkubwa. Ninaishukuru Serikali ya Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Kikwete aliamua kuchukua sehemu ya mishahara ya bench la TFF, akasaidia kuibeba TFF, kwa maana ya kulipa makocha.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuisaidie TFF, TFFkwa pale walipofikia bajeti yao ni ndogo sana. Timu ya taifa tunatamani ifanya vizuri, kufanya vizuri kwa timu ya taifa ndivyo taifa letu linavyoendelea kutangaza kimichezo na kuendelea kufungua fursa. Serikali inaweza ikachukua jukumu hata la kulipa mishahara tu ya makocha ikasaidia TFF. TFFyetu pale tukiangalia ofisi zao hazina hadhi. Somalia kuna vita lakini wana ofisi nzuri kuliko hata ofisi yetu ya TFF. Ni kitu ambacho kinatia aibu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ione haja ya hata kuishauri TFF wajenge majengo yenye hadhi nzuri, lakini si hadhi nzuri tu bali pia muipokee mzigo, mzigo wa TFF ni mkubwa, wamejitahdi kwa level yao. Leo hii tuna timu za wanawake na tuna timu ya taifa zinafanya vizuri na vile vile kuna vilabu ambavyo vinafanya vizuri. Basi Serikali ione sasa, kwamba hawa wenzetu wanapambana kwa level hii lakini kuna majukumu mengine tuwapunguzie, miongoni ni suala la mishahara, wapunguziwe mishahara TFF, Serikali ione haja jinsi kuingilia na kuwasaidia.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini zaidi ya hapo tuseme tu, Serikali muendelee kuiunga mkono Simba, inaenda kuandika historia ya tofauti kwenye Taifa hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.