Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Hon. Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii, ili niweze kuchangia kwenye hotuba ya Wizara ya TAMISEMI iliyopo mbele yetu. Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ni kwa upendeleo wake tu kwamba tunaendelea kuwa salama, akizidi kutupa baraka zake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pili, niipongeze Serikali, kwa hotuba iliyopo mbele yetu, ni hotuba ambayo inatutia matumaini, inatutia matumaini kwenye maeneo mengi. Kwenye eneo la elimu sisi wengine tukisia kwamba zinakwenda kujengwa sekondari za kata, kwenye kata ambazo zilikuwa hazina sekondari kwetu wengine ni faraja kubwa. Hongereni sana Serikali kwenye sekta ya afya mmesema mengi, hongereni. (Makofi)

Mhesimiwa Spika, lakini niseme machache, nianzie TARURA ambayo wenzangu wengi wamesema, wote tunakubaliana kwamba kiasi cha fedha kinachopelekwa TARURA ni kidogo na kwamba lazima tutumie maarifa mapya ili kupata vyanzo vya kuongeza mapato ya kupeleka fedha kwenye eneo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, yametoka mawazo mengi, naomba Serikali iwe sikivu, tuongeze fedha hizi twende tukazijenge barabara za vijijini. Maana barabara hizi, zinahusiano wa moja kwa moja na ukuaji wa uchumi lakini vilevile kuondoa umaskini kwa watu wetu. Lakini wakati tukizungumzia eneo la kuongeza fedha, kuna eneo lingine lazima tuliangalie, udhibiti na ufuatiliaji. Ni eneo ambalo naliona kama hatujalizungumzia sana na hapa nitatoa mifano, mifano ambayo inagusa Mkinga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka 2019, Mkoa wa Tanga ulipata majanga ya mafuriko, miundombinu mingi ikaharika, Wilaya ya Mkinga tulipata bahati mbaya madaraja ya barabara za TARURA lakini hata zile za TANROADS. Barabara za TANROADS zilifanyiwa kazi lakini TARURA kipindi kile ilishindikana, tukaambiwa jambo lile linachukuliwa liingizwe kwenye bajeti ya mwaka 2020 ikaingizwa, Mwezi wa Julai, 27 ikifunguliwa zabuni kwa ajili ya kutengeneza barabara zile na madaraja yaliyokuwa yameharibika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tarehe 13 Agosti, 2020, Zabuni ile ikafunguliwa lakini Wakandarasi hawakupatikana. Ikatangazwa tena mwezi Novemba, 2020 akapatikana Mkandarasi, tarehe 03 Machi, 2021 wakaingia Mkataba, Mkandarasi akakabidhiwa eneo la kazi, alitakiwa tarehe 15 Aprili, 2021 awe ameanza kazi, mpaka leo hajaanza kazi. Hii ni dalili mbaya, kwamba Mkandarasi huyu anakwenda kushindwa, akishindwa maana yake tutangaze tena apatikane Mkandarasi, hapa imebaki miezi miwili mwaka wa fedha huu uishe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tangu 2019, watu hawa wa Kuze, watu wa Mhiduro, watu wa Bosha, hawawezi kupitisha mazao yao kwenye barabara kwasababu daraja limevunjika, fedha zipo lakini tunashindwa kuhudumia barabara hizi kwasababu ya taratibu za kirasimu za ununuzi niwaombe sana, tufuatilie eneo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, zinaweza kuwa nitaratibu za kimanunuzi lakini vilevile inaweza kuwa ni uchochoro wa fedha zisitumike eneo hili ziende zikatumike eneo lingine, tusaidieni daraja lile la Kauzeni liweze kushughulikiwa. Lakini hata kwenye allocation ya fedha, TARURA wana mpango wa kutoa fedha za maendeleo zinazokuwa nje ya zile za kibajeti kwenye wilaya hizi ili iweze kusaidia miradi ile ambayo inahitaji fedha nyingi iweze kushughulikiwa. Sisi wa Mkinga tangu mwaka 2013 hatujawahi kupata fedha hizi, wilaya hii ina maeneo ya milima, barabara za kwenye milima ni changamoto kwa hiyo, tunashindwa kutengeneza barabara hizi kwasababu kabajeti ketu ni kadogo. Mtendaji Mkuu wa TARURA alikuja kule, akaiona hali akasema watu wa Mkinga mnastahili kupata fedha hizi mpaka leo, tangu mwaka 2013 mpaka leo, hakuna senti tano iliyokwenda. Hii haiwezi kuwa sawa, tunaomba mtusaidie. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye Sekta ya Afya, nakwenda kulekule kwenye ufuatiliaji, tunaishukuru Serikali imetupatia fedha kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya. Tulipata milioni 500 mwaka wa fedha uliokwisha lakini kwasababu zilichelewa kuletwa mwezi wa Juni fedha zile zikarudishwa. Mwaka huu wa fedha Januari tumepata bilioni 1, tunaishukuru Serikali lakini naomba Serikali mfuatilie, ninashida na utekelezaji wa mradi huu, kwa sababu tumepata fedha Januariā€¦ (Makofi)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Spika, mpaka leo.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Spika, mpaka leo, katika bilioni 1 ni milioni 200 tu zimetumika. Kuna Kamati ya Manunuzi kule ya hovyo nendeni mkafumue kamati ile, haiwezekani miaka miwili mfululizo Serikali inatoa fedha halafu ifike mwezi Juni hapa hakutuweza kutumia fedha zile zirudi serikalini, haiwezekani! Sasa Serikali mtusaidie, msingoje ufike mwezi Juni mtuambie Mkinga hamkuweza kutumia fedha. Nendeni sasa mkasimamie jambo lile. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Sekondari ya Maramba. Tumekamilisha madarasa pale, ya kuipandisha hadhi sekondari ile iwe na kidato cha tano na cha sita. Tunaishukuru Serikali ilileta milioni 300 pale, wananchi wamechangia, Mbunge wao kupitia Mfuko wa Jimbo nimechangia, tumakamilisha mabweni, tumeweka samani, ilikuwa ianze mwaka jana kukawa na tatizo la kuweka bajeti ya chakula kwa sekondari ile ikashindwa kuanza. Naomba kipindi hiki sekondari ile ianze. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Spika, Lazima ianze.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Spika, tunaishukuru Serikali kwa kutoa kibali cha zahanati zetu karibu tano hivi tulikuwa tumeziombea zipate kibali zianze. Kibali kimetoka tumeziweka zahanati hizi kwenye mpango wa bajeti vifaa tiba viende. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini la mwisho na hili Mheshimiwa Waziri wewe unalijua, Mheshimiwa Waziri Mkuu alifanya ziara, akaja Maramba, tukampeleka kwenye Kituo cha Afya cha Maramba. Maramba kuna zaidi ya watu 12,000 tumeomba hospitali ile kwasababu ina hudumia kata saba ipewe hadhi ya kufanya kama hospitali ya wilaya ili mzigo ule wa kuhudumia zile kata sana uishe. (Makofi)