Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi na pengine nipongeze kazi kubwa ambayo unafanya na wenzetu kuanzia Waziri mwenyewe pamoja na majeshi yote. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ilitaka tu kuongelea kwenye maeneo machache lakini moja wapo wa maeneo nataka kuzungumzia ni mazingira ya kazi kwa wenzetu wa Jeshi la Polisi. Ni vyema Serikali ikatazama kwa kina mazingira yale ya kazi, leo ukiingia kwa OCD au ofisini pale Polisi wakati mwingine mazingira hayatoshi, furniture ni za hovyo. Ni vizuri tukalitazama hilo ili kulipa heshima Jeshi letu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini pili tumeona jinsi ambavyo tumekabidhi dhamana kwa wenzetu wa Jeshi la Polisi, wanafanya kazi kubwa ya usalama wa nchi yetu. Na hili nafikiri Mheshimiwa Waziri ni vizuri ukalitazama vizuri sana hili tutakapokuwa tunapitisha huko baadaye kwasababu haiwezekani Polisi wanafanya operesheni za ulinzi na usalama wa watu wetu na sisi kipaumbele cha kwanza ni ulinzi na usalama wa watu wetu na mali zao halafu OCD, OCS, wanaomba mafuta kwa wadau ambao miongoni mwao watageuka kuwa wahalifu, heshima ya Jeshi iko wapi hapo? Hii sio sawa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka kupendekeza tuweke mkakati mzuri ili kulipa heshima jeshi letu angalau wanapofanya shughuli zao wawe na bajeti ya kutosha. Tunawapa inferiority complex n ahata uwezo wa kusimamia sheria na kanuni inakuwa ni changamoto.
Pili, tunajikuta tunalazimisha vitendo vinavyoitwa rushwa, yue mtu anawapa mafuta kila siku, kesho unakuja kumuambia ni mhalifu, kibinadamu inakuwa ni changamoto kubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa wenzetu wa Jeshi la Polisi iko changamoto kubwa sana kwenye dhamana. Ni vyema mkalitazama nchi nzima kwenye vituo vyetu. Mfumo wetu wa utoaji dhamana ukoje? Kwa nini mtu akikamatwa Ijumaa anakaa mpaka Jumatatu wakati Jumamosi na Jumapili kazi inafanyika, tunafanya haya yote kwa faida ya nani? Ni vyema tukalitazama jambo hili pia kwa kina ili kusaidia watu wetu. (Makofi)
SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa.
MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Spika, ahsante, naunga mkono hoja. (Makofi)