Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Hon. Tabasamu Hamisi Hussein Mwagao

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sengerema

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

MHE. TABASAM H. MWAGAO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Segerema naomba kuchangia mchango wangu katika hotuba ya Waziri wa Ulinzi kama ifuatavyo; nimeusikiliza mchango wa Mheshimiwa katika maombi yake ya kupitisha bajeti, lakini kazi nzuri zinazofanywa na wanajeshi wetu katika ulinzi wa mipaka ya nchi hii, lakini kufanya kazi za kijamii katika nchi hii tunaomba tushauri kama ifuatavyo:- (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba Wizara ya Ulinzi lazima iwe na kitengo cha kisayansi, leo tumekutwa na gonjwa kubwa kama hili la Covid, lakini wanajeshi wetu wangefanya kazi hii, na wao ndio wangekuwa wa mwanzo katika mstari wa mbele kwenye tiba na kila kitu. Tunayo Hospitali yetu ya Lugalo kule Mwanza tunayo Hospitali ipo Pasiansi kule. Lakini wanazo hospitali zao nyingine za kijeshi ambazo zingeweza kutumika katika hali hii ya kupambana na hali kama hii kwa sababu kwa mfano mwishoni mwa mwaka jana hospitali zetu zote zilielemewa, lakini hatukuona jeshi kuchukuwa msaada katika jambo hili wanayo mahema, wana kila kitu sasa inamaanisha kwamba jeshi limeandaliwa kwenda kupigana vita tu, sasa ni hatari sana kuwa na jeshi la namna hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tunahitaji jeshi kama nafasi za kuajiri basi waajiri wataalamu, hii ni jambo ambalo kwenye mpango wenu kama jeshi basi mgeweza kuajiri wataalam na wakapelekwa katika nchi ambazo zimeendelea sana kisanyansi, mfano Cuba, labda India wakapelekwa China, Urusi hawa wangekuja kama madaktari wa akiba wakuja kufanya kazi za kuokoa nchi kama hiko katika hali mbaya kama hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili ambalo nataka kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi, ni kwamba wanajeshi sasa hivi tabia zimebadilika, wanajeshi wetu sasa hivi wanaishi na raia sio kwa ugomvi kama ulivyokuwa mwanzo. Mara nyingi sasa kungekuwa na mikutano hata kama kuna hali ya mipaka, wanajeshi sasa hivi wanakaa na wananchi. Kwa mfano kule kwangu katika eneo la Sengerema wana uwanja wao waliacha kambi ya jeshi ilihamiishwa kutoka Sengerema kuhamia Tabora.

Mheshimiwa Naibu Spika, kambi hii inakuwepo miaka 1980 na 1985 sasa tumesikia tena wanajeshi wanakuja kuchukuwa eneo hilo ambalo lile eneo lilibakia kwa Halmashauri.

Sasa tunamuomba waziri pamoja na kazi nzuri mnayofanya hili eneo letu la Sengerema katika eneo la Nyatukala mnakuwa na eneo lingine katika eneo la Nyamterera eneo lingine mlikuwa kule eneo la Nyamazugo kama sehemu ya mafunzo ya kijeshi na eneo la kambi, kwa sababu maeneo haya mliyakabidhi basi tunakuomba Mheshimiwa Waziri hili lenyewe uliangalie limekuwa ni shida, leo mkitaka kuja kudai maeneo yenu kule, wananchi wameshajenga, Serikali imejenga ofisi ya kata, imejenga ofisi yake ya Idara ya Ujenzi, tunayo shule ya msingi Mweli pale, zote ziko katika eneo ambalo tayari mnadai kwamba mipaka hii ni ya kwenu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunategemea jeshi hili sasa ni Jeshi la Wananchi, likisha kuwa Jeshi la Wananchi basi hebu pelekeni mipango mizuri kwa wananchi, maeneo mengine yapo Sengerema tunayo maeneo ambayo mnaweza mkaja mkachukua kule ambayo yako vizuri sana kwa ajili ya ulinzi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, najua kwamba tuna ujenzi wa daraja kubwa la shilingi bilioni 700 kuna eneo la Kigongo Ferry ambalo kama mlipanga kama jeshi leo na lenyewe lile lina miaka kama 40 halijafanyiwa kazi. Basi ni vizuri Mheshimiwa Waziri katika hotuba yako ukija katika majumuhisho basi uangalie hilo eneo la Kigongo Ferry mwende kiustaarabu na huku Sengerema mje muangalie maeneo mengine Halmashauri inaweza ikawapa, lakini hili eneo la Sengerema Mjini kweli itakuwa ni shida kwa wananchi wa Sengerema. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata mimi kama mwakilishi wao nitakuwa niko katika hali mbaya sana kwa sababu kwanza hatuwezi kubishana na jeshi, kwa nafasi yenu na mamlaka ya ulinzi wa nchi, basi maeneo kama haya yapo nchi nzima, basi ni vizuri mkayapitia upya muone kama kuna maeneo ambayo sasa hivi wananchi wameshavamia wako katika maeneo hayo, basi jeshi linaendelea kutafuta eneo lingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu ndio huo, nakupongeza sana Mheshimiwa kwa usikivu wako na nina imani hili utalisikia kwa ajili ya wananchi wa Sengerema na kwa nchi nzima, ahsante sana. (Makofi)